Biashara ya boda boda

Biashara ya boda boda

Acha kumdanganya jamaa kuwa afanye Kazi ya boda boda mjini Dar es Salaam !!! Boda boda haziruhusiwi !!!
Nenda kule kwenye uzi wako wa udalali wa Rav 4 milion 22, tuondolee mipasho hapa
 
Kuna uzi upo humu ingia,tulichangia vya kutosha,tunaona uvivu kurejea

Ila una haki ya kulinda chombo chako kisheria,hata kumi ilianza na moja,tusidharau hatua ya mwenzetu kwenye maisha.
Kuna watu hata Baiskeli hawana.Changamoto za biashara hii zinaanzi hata kwenye Ushauri,nahapa ndio umeanza nazo,sasa bado za kiutendaji ambazo itabidi ufungue uzi utakua maelezo ya kutosha kwa kadri ya mungu alivyojaliwa wachangiaji.

Ubarikiwe katika hatua yako

asante sana kiongozi. wajasiriamali wanahitaji watu kama nyinyi
 
Mkuu usikubali kama upo kibiashara. wenzio wanafanya hivi;
kama umenunua pikipiki mpya huwa haisumbui so muelewane awe anakuletea bei gani kwa wiki. ikishamaliza mwaka ndo mnaingia mkataba. hapo unakuwa na uhakika wa kurudisha hela yako vinginevyo hutapata faida. ni hayo tu. mia
 
Kuna mfumo tunaanzisha wa GPS za bodaboda, kwamba utafuata mizunguko yote ya dereva wako kwa siku. Natumai hii itapunguza haya matatizo ya uaminifu.
 
Well, mi nadhani uitoe kwa mkataba kiasi kwamba akivunja mkataba inamgharimu yeye dereva.Ni mkataba wa mwaka akimaliza mwaka mmoja bodaboda inakuwa ni yake.

Hesabu kwa siku elf kumi kwa wiki sabini au sitini itategemea na makubaliano yenu aidha kama siku ya saba itaenda service au laa.Hakuna longolongo wee unachotaka ni hela yako tu siku akizingua inamgharimu yeye inakuwa ni amevunja mkataba, unampa vigezo vyako na kumuuliza kama ataweza kazi au laa tena kwa kuandikishiana na umpate dereva muaminifu ikiwezekana unayemfaham uzuri kabisa.

Bodaboda iwe mpya kabisa sio used coz hii inasaidia dereva kuitunza kwa sababu anajua baada ya mwaka tu inakuwa ni yake kwa hiyo ataitunza na kuzingatia kazi yake na hesabu na chombo kwa ujumla.

Kama makubaliano yenu ni elfu kumi kwa siku, hivyo itakuwa ni elf sabini kwa wiki kwa makubaliano mtakayopeana kwa siku hizo za kazi.Hivyo kwa wiki nne za mwezi ni laki mbili na themanini (280,000) ambapo kwa mwaka utakuwa na 3360000.Kwa hiyo hela ukigawa mara mbili utakuwa umeweza kuongeza boda mbili na ile moja ukamuachia dereva wako ikiwa imekuzalishia boda mbili kwa mwaka, mbili zitazaa nne na hivyo kwa kifupi ni uangalizi na usimamizi mzuri tu wa chombo naamini MUNGU ataleta mafanikio.Na pia kila kitu ni kufanya na kupima kiko vipi ila maji hayapimwi kwa miguu miwili kwa hiyo kama mtaji wako ni wa boda nne anza kwanza na mbili mkuu huku pesa nyingine ikiwa kibindoni kiongozi.

Nakutakia kila la heri.
asante sana kwa ufafanuzi kwani hata mm umenisaidia sana kwa huu ushauri mzuri mkuu
 
Mkataba kwa pikipiki uko hivi, unaandikiana kwa veo au m/kiti wa mtaa kuwa unamkabizi kwa miezi flani na kila siku atakukabizi tsh 10 000/ baada ya mda kuisha unamkabizi kadi inakua mali yake, pia ionyeshe:-
1.marekebisho(service)zote anafanya yeye
2.asipo rejesha siku 3 au 4 au 5 mfululizo au ndani ya wiki mkataba unavunjika na anarudisha pkpk na hakuna madai, pia unaweza ongeza na mengine
Inakuaje dereva akiwa mgonjwa
 
Mambo muhimu ni kuainisha ya kwamba service zote ni juu yake,
Upotevu wa Mali utamuhitaji alipe nyingine kwa haraka Sana.
Unaainisha date of start and finish.
 
Naomba nishee uzoefu hapa.

Mimi binafsi nafanya biashara hiyo, nilianza rasmi 24/5/2016. Kwanza kabla ya kununua pikipiki nilianza kufanya utafiti kwa kutafuta vijana waaminifu wanaoendesha bodaboda katika eneo langu (Mbezi Makabe), na utafiti huo nilimtumia jamaa yangu ambaye naye alikuwa ni dereva bodaboda.

Nikaanza na pkpk tatu (Boxer) ambazo nilinunua 2,100,000/= kila moja na bima comprehensive 175,000 hivyo kila pkpk ilinigharimu 2,275,000.

Nikawakabidhi vijana watatu kwa makubaliano ya kuleta 10,000 kwa siku kwa muda wa miezi 11. Katika mkataba tumekubaliana hela yangu ni lazima iletwe kila siku na usipoleta hela kwa siku 7 mfululizo bila maelezo ya kueleweka mkataba umevunjika. Matengenezo yote ni juu na kijana na pia akipigwa fine inayotokana na uzembe atalipa yeye mwenyewe. Pia pkpk ikipotea yeye pamoja na mdhamini wake watawajibika kulipa pkpk mpya.

Nimefungua Acc maalum ambayo hela za pkpk zinakaa na kila siku naingiza hela hizo. Kwa sasa nina pkpk tano, ambapo vina hawa hawa nawatumia kuniletea vijana wengine wazuri ambao wataingia kwenye kampuni yetu. Pia vijana wote watatu wa mwanzo nimewaahidi kuwapa pkpk mpya baada ya kumaliza mkataba, ambapo mmoja nimemuhahidi kumpa umeneja baada ya biashara kuwa kubwa (Yaani tutakapokuwa na pkpk 10 na kuendelea)

Changamoto ndogo ndogo zipo mf. Kuna kijana mmoja alikamatwa na polisi pale Mbezi kwa kutovaa helment na akabishana sana na Trafic akabigwa fine ya 90,000. Kutokana na makosa aliyofanya na mkataba tuliofunga alilipa elfu 50 nikamkopesha 40 tukaitoa pkpk, nikamsema sana na kutishia kuvunja mkataba kama atarudia ujinga huo, mpaka leo anakwenda vizuri kabisa.
Kijana mwingine alikuwa afanyi service on time lakini pia alikuwa abadili oil filter on time so pkpk ikawa inatoa moshi sana. Nikamnyang'anya pkpk kama kwa wiki moja akaomba msamaha naye akaomba nimpe 50,000 atengeneze ili nije kumkata kwenye hesabu, pia atalipa siku tano zote ambazo pkpk haikufanya kazi. Nikafanya hivyo mpaka leo ameshalipa deni lake lote.

Njia nyingine nayoitumia kwa vijana wangu nimeanzisha mchezo wa kuweka hela ambapo kila baada ya siku tano mtu anapokea na tunatoa 10,000 kwa kila jina moja. Nimewashawishi vijana wangu wote wanacheza mchezo na mimi kila pkpk nimeiwekea majina matano, ambapo kila kwenye elfu 70 ya siku 7 elfu 50 inalipa mchezo. Jumla tunacheza majina 30, ambapo kila baada ya siku tano mtu anapokea laki tatu. Na ata huyo kijana aliyeharibikiwa na pkpk nikamkopesha nikamkata kwenye jina lake la mchezo. Next week naongeza pkpk ya sita inshallah.

Kwa hiyo ndugu zangu hakuna biashara isiyo na changamoto, biashara hii ya pkpk hakikisha unatafuta watu wenye uaminifu na unawafanyia utafiti wa kutosha kabla ya kuwapa chombo. Ikiwezekana unawaambia wazazi wao ndio wawe wadhamini kama wapo au mtu wake wa kuaminika sana. Kwa sasa nina list ya vijana watano ambao wamependekezwa kupewa pkpk mpya na naendelea kuwafanyia vetting ili kuwapa vyombo.

Samahani kwa post ndefu ila nimetoa ushuhuda mrefu ili wenye kujifunza kitu waweze kufanya hivyo.
 
Hongera mkuu ila hapo kwenye mchezo kama sijapaelewa
 
mm mpaka sasa nina miliki mbili ila ukimpata kijana mzur raha sana mm nmempata kijana mzur mpaka baadhi ya wiki namuambia asinpe helaa
 
Hongera mkuu ila hapo kwenye mchezo kama sijapaelewa
Mzee hiyo ya mchezo ipo nje ya biashara hiyo ya pkpk. Nimejaribu kueleza kwa sababu nafanya hivyo pia. Ni hivi sababu vijana wengi wa boda boda si watunzaji wazuri wa pesa wazipatazo ndio maana nimewashauri tuanzishe mchezo kama upatu hivi na vijana wangu. Ambapo kila baada ya siku tano kila mtu anatoa 10,000 tunamkabidhi mtu mmoja. Hii niliifanya mahususi kuwasaidia kuweza kupata kipato cha mara moja ambacho kinaweza kuwasaidia kufanya jambo lolote linalowahusu.

Haina ulazima wa kufanya hivyo kama una pkpk moja lakini kama una pkpk nyingi ni nzuri
 
Well, mi nadhani uitoe kwa mkataba kiasi kwamba akivunja mkataba inamgharimu yeye dereva.Ni mkataba wa mwaka akimaliza mwaka mmoja bodaboda inakuwa ni yake.

Hesabu kwa siku elf kumi kwa wiki sabini au sitini itategemea na makubaliano yenu aidha kama siku ya saba itaenda service au laa.Hakuna longolongo wee unachotaka ni hela yako tu siku akizingua inamgharimu yeye inakuwa ni amevunja mkataba, unampa vigezo vyako na kumuuliza kama ataweza kazi au laa tena kwa kuandikishiana na umpate dereva muaminifu ikiwezekana unayemfaham uzuri kabisa.

Bodaboda iwe mpya kabisa sio used coz hii inasaidia dereva kuitunza kwa sababu anajua baada ya mwaka tu inakuwa ni yake kwa hiyo ataitunza na kuzingatia kazi yake na hesabu na chombo kwa ujumla.

Kama makubaliano yenu ni elfu kumi kwa siku, hivyo itakuwa ni elf sabini kwa wiki kwa makubaliano mtakayopeana kwa siku hizo za kazi.Hivyo kwa wiki nne za mwezi ni laki mbili na themanini (280,000) ambapo kwa mwaka utakuwa na 3360000.Kwa hiyo hela ukigawa mara mbili utakuwa umeweza kuongeza boda mbili na ile moja ukamuachia dereva wako ikiwa imekuzalishia boda mbili kwa mwaka, mbili zitazaa nne na hivyo kwa kifupi ni uangalizi na usimamizi mzuri tu wa chombo naamini MUNGU ataleta mafanikio.Na pia kila kitu ni kufanya na kupima kiko vipi ila maji hayapimwi kwa miguu miwili kwa hiyo kama mtaji wako ni wa boda nne anza kwanza na mbili mkuu huku pesa nyingine ikiwa kibindoni kiongozi.

Nakutakia kila la heri.
Mkuu ushauri wako ni mzuri..mimi nimeanza na moja mwezi huu na kila mwezi nitaongeza nataka nione..Sijawahi fanyabiashara hata ya nyanya ila nimeanza na bodaboda moja mpya.Nimempa kijana namuamin tu,ni ya mkatabawa mwaka mmoja.Tumekubaliana mahali pa kwendakufanya service kila week .
 
Nataka Kuingia pia Kwenye Biashara hii Wana JF nilikuwa nataka Ushauri wenu.. maeneo nilipo Kwa Utafiti Nilioufanya Boss Anapelekewa Sh 7000 per day... Na ushauri wa Boda Boda Gani Ni Nzuri Nikaambiwa Ni SanLG na KingLion zipo Vizuri

Sasa Je Kwa Biashara Hii Nyie Mwaionaje inachangamoto Gani Na Matatizo gani Mwakutana nayo ..

Asanteni
 
Uko mkoa gani?

Kwa ujumla biashara hii ina changamoto sana hasa vijana ni pasua kichwa!!
 
Back
Top Bottom