Biashara ya boda boda

Biashara ya boda boda

uza maandazi au eggchop mtaani kwenu itakulipa kuliko boda boda,,,,, utanunua mpya baada ya siku mbili vijana watakuambia wameibiwa boda boda
 
Jiandae , Mosi, Hesabu kutokutimia Pili, Matunzo mabovu Mara kwa Mara iende gereji kwa gharama za mishahara wako, Tatu,Kutokumpata dereva Mwenye leseni itakupelekea wewe kulazwa keko kwa Siku 14 wewe na dereva wako Kisha mahakamani pale anapopata ajali.Pia bima haitakulipa kwa kuwa uliajuri dereva asiye na leseni.MIMI NILiNUNUAGA MIL1.8 NILIIUZA KWA MIL1 BAADA YA KUNITIA HASARA. LAKINI USIFE MIYO JARIBU BAHATI YAKO
 
tafuta mradi mwingine miaka hii biashara ya bodaboda uendeshe mwenyewe .. zaidi ya yote hakuna pikipiki mpya ya kibiashara inayopatikana kwa bei hiyo
 
Nenda kwa jamaa wa GSM wana pikipiki nzuri na wanatoa warranty ya miezi kama mitatu hivi. Kingine utaratibu mzuri ni kumpa dereva ambaye mnakubaliana anakuwa anakupa hesabu fulani kila wiki baada ya miezi 8 kama unazitunza utakuwa umeshapata hela ya kununua nyingine then baada ya mwaka unamuachia pikipiki inakuwa ya kwake
 
biashara hiyo ya bodaboda ni paisua kichwa ila nakushauri ifanye na tafuta dreeva mwaminifu ila ni bora utafute biashara ingine mkuu maana mmhm
 
yan km unataka kupoteza ela yako ingiza uko....ataluletea wik ya kwanza vzr akijitahd nayapili ila kutokea apo utajuta..mara kaumwa...mtt kapelekwa hosp....binafsi almanusura nijiingize boda boda mmoja ndo kaniokoa kaniambia bro ela yako bora ukanunue ata mahindi km huna kaz nayo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wadau habari zenu.

Ninataka kuanza biashara ya bodaboda ila kwa mkataba. mwenye ujuzi naomba msaada wa maelezo inavyokuwa tafadhali. nahitaji kujua dereva anapaswa alete kiasi gani cha fedha kwa wiki, na mkataba huwa wa muda gani? na service anafanya yeye kwa pesa zake au nafanya mimi mmiliki? Naomba kueleweshwa tafadhal. natanguliza Shukrani.
 
hiyo hela yako ya kununua boda boda bora unipe mimi niizungushe tu non risk.. nikurudishie kwa mfumo ambao boda boda ya mkataba inampa mmiliki..

tofauti yake ni kwamba mimi nakupa faida nusu ya boda wa mkataba angekupa... sabab hutakuwa na risk yoyote tofauti na boda boda inaweza ikagongwa au kuibiwa before mkataba kuisha...ukala hasara..

mimi naitumia kwenye tshirt business tu... naongeza tu mtaji na naagiza zangu plain tu somewhere

Tshirt Garage Mabibo Hostel (@tshirt_garage_mabibo_hostel) • Instagram photos and videos

na loundry shop yangu naongeza hela nanunua mashine heavy duty
 
Wadau habari zenu.

Ninataka kuanza biashara ya bodaboda ila kwa mkataba. mwenye ujuzi naomba msaada wa maelezo inavyokuwa tafadhali. nahitaji kujua dereva anapaswa alete kiasi gani cha fedha kwa wiki, na mkataba huwa wa muda gani? na service anafanya yeye kwa pesa zake au nafanya mimi mmiliki? Naomba kueleweshwa tafadhal. natanguliza Shukrani.
Nimekutumia ujumbe PM
 
Aisee Shida Vijana Vijana Wakija Vichwa Chini,mikono Nyuma Mkishakabidhiana Maumivu Sijui Kama Mfumo Umebadilika Nlinunua Boda Moja 2015 mpya tukaenda kwa mwanasheria yeye akiwa na mdhamini wake ,service juu yake kila siku anatakiwa alete 10,000 (hapa Nlimuambia Awe Anarusha Kwa Fahari Huduma Crdb)Ikiisha Mwaka Inakuwa Yake,akizidisha Siku 5 Yaani Deni Hajaleta Tunaterminate Contract,nachukua Boda Bila Kumrudishia,ila Nlifanyia Kazi Mwezi 1 tu nikaiuza na nliyemuuzia nae akaiuza ndani ya mwezi maana pasua kichwa hiyo biashara.
kijana alikuwa haleti pesa,nkampa simu tuwasiliane simu hapatikani,kwake hayupo mke na mtoto mchanga wakawa wanalia njaa kwangu kwa kujua hela zote mume analeta kwangu,nkimsaka anajificha,nkawa mbabe nikaweka dau kijiweni atakayefanikisha nimkamate nampa 15,000 siku hiyo nlimpata akakabidhi funguo zote ila ilishaanza kuchoka no service nikauza na nliyemuuzia baada ya mda akaniambia ameuza pasua kichwa
ila kuna mdada kaifanikisha hii biashara anazo boda kama 15 hivi
 
Nina Jamaa Yangu Aliibiwa Tena Kwa Uzembe Wa Dereva Analewa Anaenda Nayo Bar,ila Alilipwa Pesa Yake Japo Kwa Awamu
Mimi Nimejifunza Biashara Ndogo Ndogo Za Mtaji Midogo No Stress Wala Nguvu Wala Akili Na Zinanipa Hizo 10,000 Au 20,000 Kwa Siku Ila Hiyo Hapana Aisee
 
Wadau habari zenu.

Ninataka kuanza biashara ya bodaboda ila kwa mkataba. mwenye ujuzi naomba msaada wa maelezo inavyokuwa tafadhali. nahitaji kujua dereva anapaswa alete kiasi gani cha fedha kwa wiki, na mkataba huwa wa muda gani? na service anafanya yeye kwa pesa zake au nafanya mimi mmiliki? Naomba kueleweshwa tafadhal. natanguliza Shukrani.
50 - 50 Mkuu.

Lolote linaweza kutokea.
hata hao wadhamini hao hawana uhakika.
Kwenye 4 moja faida, moja nyang'aanya, moja ibiwa, moja nalipwa ndo ndo ndo ndo
ila sikomi.

Tafuta mwaminifu na mzoefu, ukimpata aliyewahi kuibiwa ni bora zaidi.
 
Hii biashara bwana bora uendeshe mwenyewe yaani ww ndio uwe dereva,vijana wanashida sana + mihemko basi tafrani tupu,labda umpate mwaminifu kwelikweli...mm ndani ya mwaka mmoja niliiuza tena kwa hasara sana,maana kijana wa kwanza kumkabidhi aiseee baada ya wiki mbili tu chombo kiko hoooi yaani mpaka roho iliniuma maana sikununua kwa mtu,.hapo bado hela huletewi kwa wakati nikaona isiwe tabu mwenyewe nikanyoosha mikono juu..
 
Yaani hawa vijana wa bodaboda kama wana akili moja, wanakuja mikono ukishampa vitimbi vinaanza.
 
Hii biashara bwana bora uendeshe mwenyewe yaani ww ndio uwe dereva,vijana wanashida sana + mihemko basi tafrani tupu,labda umpate mwaminifu kwelikweli...mm ndani ya mwaka mmoja niliiuza tena kwa hasara sana,maana kijana wa kwanza kumkabidhi aiseee baada ya wiki mbili tu chombo kiko hoooi yaani mpaka roho iliniuma maana sikununua kwa mtu,.hapo bado hela huletewi kwa wakati nikaona isiwe tabu mwenyewe nikanyoosha mikono juu..
Dah pole kwa kuishia njiani,kuna mbinu ulikosa za kuimanage .
 
Boda boda za mkataba hutegemea na mmiliki anataka kutoa kwa kipindi gani,kuna miezi 9,10,11,12 kulingana na aina ya chombo.
Binafsi ninajihusisha na hii biashara,Nilishaweka pikipiki 9,za mikataba,kwa wakati huu nimezipunguza ili nihamie kweny bajaji
 
Back
Top Bottom