Maelezo yako nayakubali kwa100% mm nlifanya ila nliacha wakati zinauzwa1.8 milNina mwaka mmoja sasa katika hii Biashara.
Mimi Huwa nawapa vijana Pikipiki mpya FEKON Kwa MKATABA Wa miezi 11 au 12. Mahesabu ni 100,000/= Kila baada ya siku 10 yaani Kwa Siku ni hesabu ya 10,000/=.
Vijana wengine sio waaminifu na kweli hamna mtu mkamilifu Kwa asilimia 100% changamoto zipo anaweza kupata dharula, ajali, kuumwa au matatizo binafsi tu. Ambayo Kwa hizo siku 10 anaweza kukuletea 60K au 70K au 80K etc ila Hamna shida Huwa naandika kama deni ambalo baadae Mkataba ukiishi naongea nae Tena mezanii.
Ni Biashara nzuri Kwa maana FEKON Moja inauzwa 2.3M Kwa Faida wewe Utapata sio chini ya 1M Kwa miezi 11 au 1.3M Kwa miezi 12. Ambayo ni sawa na faida ya 100,000/= Kwa Kila mwezi Kwa Pikipiki Moja.
Mwaka Huu nataka nijaribu Kwa kununua Pikipiki USED na nianze kuwapa vijana Pikipiki USED za 1.2M -1.5 Millions Kwa Mikataba ya miezi 7 mpka miezi 8. Ili nitengeneze Faida nyingi Kwa muda mchache na Kwa kutumia Hela ndogo badala ya kununua Pikipiki mpya ya 2.3M.
Changamoto zipo lakini usikate Tamaa, Kila Biashara inachangamoto zake.
Vijana wapo mtaani kwako ni swala la kupeana Mkataba mbele ya mashahidi wa pande zote mbili na Kwa kusainiwa na Mwenyekiti au Mjumbe Wa Kijiji/ mtaa husika.
Nafkiria kurudi ulingoni mwakani,vijana bado wananipigia kuhitaji pk pik