Biashara ya Bodaboda

Kwa arusha wanapenda sana sinoray,skygo,boxer au kinglion ila ni chaguo la kijana unayempa anataka ipi



Kikubwa hapo n mkataba wa mwanasheria au wakili

Na muhusika lazima umjue anapoishi pia lazima awe na wadhamini
 
Mimi kwenye Mkataba wangu Kuna

1. Sehemu ya Wadhamini Wa mmiliki,
2. Sehemu ya Wadhamini Wa mkabidhiwa Pikipiki,
3. Sehemu ya kuweka picha (passport size/ scanned picture) ya mmiliki & mkabidhiwa na Saini,
4. Sehemu ya Mjumbe/ Mwenyekiti kusaini,
5. Sehemu ya Mwanasheria/ Wakili kusaini.
 
Hata hiyo ya mkataba service kubwa ni juu ya boss
 
Wadhamini wa mmiliki maana yake nini ? Pikipiki yako, wanakudhamini nini ???

Mwenyekiti wa kijiji anasaini nini ? Kwamba anamjua dereva, na wewe nani anakujua ???

Mdhamini wa dereva kazi yake nini, atakulipa pikipiki dereva akipotea nayo ???

Mkataba una vigezo vya kisheria. Kuongeza mistari ya vidoti ya watu kusaini haiongezi nguvu ya mkataba.
 
Nina mwaka sasa na miezi kadhaa nafanya hii Biashara na Mkataba wangu ndio hvyo ulivyo sijawai kupata shida yoyote Ile.

Mkataba ni makubaliano tu ya kimaandishi baina ya pande mbili yaani ni kuwepo na mashuhuda tu.

Sijawai kukutana na changamoto yoyote ya Mkataba maana vijana wanapiga kazi mpka pale Mikataba Yao inapoisha.

Mkataba ni ushuhuda tu lakini kiuhalsia nikishakuwa na KADI na RISITI ya Pikipiki basii Sina haja ya maandishi au Mkataba. Wadhamini ni kuongeza nguvu tu ya kijana kujituma basii

Maana TRA inasoma majina yangu ya kwenye TIN NUMBER pamoja na kwenye KADI inasoma majina yangu.
 
Muone Lema kwa ushauri zaidi
 
Sijawai kufanya Biashara ya kuchoma mahindi, hivi ni kweli wanapata hii Faida per day?

15,000/= per day Kwa anayechoma mahindi Kwa muda Gani anapata hii Hela maana wengi wanafanya mida ya Jioni Saa 12!
Hi biashara Haina muendelezo, maana Kuna kipindi mahindi hakuna. Je utachoma mikate🤔🤔
 
Hizi ni hesabu za nadharia hazina utofauti na kilimo cha matikiti cha mtandaoni.
Hujapiga hesabu kuna spea kuharibika,kupata ajali,kukamatwa na polisi,kuibiwa pikipiki.
Lakini ni bora umeweka wazi kwamba una ajira yako nyingine hiyo bodaboda ni ya ziada tu.
Ila kwa mtu anayeishi kwa kutegemea afanye biashara ya bodaboda ni biashara kichaa.
Sio biashara endelevu na anayenufaika ni dereva tu kwa sababu baada ya mwaka anakuwa mmiliki wa hiyo pikipiki.
 
Okay, ni hesabu za nadharia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…