Biashara ya Bodaboda

Biashara ya Bodaboda

Wakuu a-saamu aleykum...
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nina mpango wa kuwekeza kwenye biashara ya bodaboda. Nipeni ushauri, aina gani ya pikipiki ni nzuri, ntapataje dereva na kwa siku ataniletea kiasi gani..

Mtaji mil 6.5
Maeneo Arusha Mjini

Nitangulize shukrani[emoji120]
Kwa arusha wanapenda sana sinoray,skygo,boxer au kinglion ila ni chaguo la kijana unayempa anataka ipi

Kikubwa hapo n mkataba wa mwanasheria au wakili

Na muhusika lazima umjue anapoishi pia lazima awe na wadhamini
 
Mjumbe wa kwao Yombo Relini kasema dereva boda anamjua lakini mimi hanitambui.

Akashauri tufuate taratibu za kawaida za mikataba, ambazo zinaweza kuwa na mashahidi wa pande mbili lakini sio wajumbe wa mitaani na Wenyeviti wa vijiji au viongozi wengine wa serikali.

Serikali haihusiki na kusaini mikataba binafsi ya raia, kadai mjumbe.
Mimi kwenye Mkataba wangu Kuna

1. Sehemu ya Wadhamini Wa mmiliki,
2. Sehemu ya Wadhamini Wa mkabidhiwa Pikipiki,
3. Sehemu ya kuweka picha (passport size/ scanned picture) ya mmiliki & mkabidhiwa na Saini,
4. Sehemu ya Mjumbe/ Mwenyekiti kusaini,
5. Sehemu ya Mwanasheria/ Wakili kusaini.
 
Jiandae Kwa Hela za service za Kila mara, maana bodaboda anajua hiyo Pikipiki sio ya kwake na hawezi kuitunza Kwa umakini.

Atahakikisha anabeba chchote kile hata kama ni tofali, chuma etc Ili tu akuletee hesabu yako na Hapo Pikipiki haimalizi mwaka imechakaa na umetumia Marejesho kurekebisha Pikipiki yako.
Hata hiyo ya mkataba service kubwa ni juu ya boss
 
Mimi kwenye Mkataba wangu Kuna

1. Sehemu ya Wadhamini Wa mmiliki,
2. Sehemu ya Wadhamini Wa mkabidhiwa Pikipiki,
3. Sehemu ya kuweka picha (passport size/ scanned picture) ya mmiliki & mkabidhiwa na Saini,
4. Sehemu ya Mjumbe/ Mwenyekiti kusaini,
5. Sehemu ya Mwanasheria/ Wakili kusaini.
Wadhamini wa mmiliki maana yake nini ? Pikipiki yako, wanakudhamini nini ???

Mwenyekiti wa kijiji anasaini nini ? Kwamba anamjua dereva, na wewe nani anakujua ???

Mdhamini wa dereva kazi yake nini, atakulipa pikipiki dereva akipotea nayo ???

Mkataba una vigezo vya kisheria. Kuongeza mistari ya vidoti ya watu kusaini haiongezi nguvu ya mkataba.
 
Nina mwaka sasa na miezi kadhaa nafanya hii Biashara na Mkataba wangu ndio hvyo ulivyo sijawai kupata shida yoyote Ile.

Mkataba ni makubaliano tu ya kimaandishi baina ya pande mbili yaani ni kuwepo na mashuhuda tu.

Sijawai kukutana na changamoto yoyote ya Mkataba maana vijana wanapiga kazi mpka pale Mikataba Yao inapoisha.

Mkataba ni ushuhuda tu lakini kiuhalsia nikishakuwa na KADI na RISITI ya Pikipiki basii Sina haja ya maandishi au Mkataba. Wadhamini ni kuongeza nguvu tu ya kijana kujituma basii

Maana TRA inasoma majina yangu ya kwenye TIN NUMBER pamoja na kwenye KADI inasoma majina yangu.
 
Wakuu a-saamu aleykum...
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Nina mpango wa kuwekeza kwenye biashara ya bodaboda. Nipeni ushauri, aina gani ya pikipiki ni nzuri, ntapataje dereva na kwa siku ataniletea kiasi gani..

Mtaji mil 6.5
Maeneo Arusha Mjini

Nitangulize shukrani🙏
Muone Lema kwa ushauri zaidi
 
Sijawai kufanya Biashara ya kuchoma mahindi, hivi ni kweli wanapata hii Faida per day?

15,000/= per day Kwa anayechoma mahindi Kwa muda Gani anapata hii Hela maana wengi wanafanya mida ya Jioni Saa 12!
Hi biashara Haina muendelezo, maana Kuna kipindi mahindi hakuna. Je utachoma mikate🤔🤔
 
Bro Nina Kazi yangu Kila mwezi napata Mshahara.

Hii Biashara ni kuongeza mzunguko wangu Wa Hela, Biashara zipo nyingi ningeamua kuacha kazi na kwenda kufanya hizo Biashara nyingine mtaani kama kufungua duka au kuuza bidhaa tofauti.

Ila nilihitaji Biashara ambayo inaweza kujisimamia yenyewe kipindi Mimi nikiendelea na mishe zangu za Kazini.

Mimi Kwa mwaka mmoja tu pekee nimefunga Pikipiki zaidi ya 15.

Kwa Pikipiki zangu 15 tu, Kwa Siku napata 150,000/=, Kwa wiki napata 1,050,000/=, kwa mwezi Kwa hizi Pikipiki 15 napata REJESHO La zaidi ya 4,500,000/=. Kwa mahesabu ya haraka Kwa Siku napata Faida ya zaidi ya 45,000/=🟧.

Kipindi napata hizi Hela zote Mimi nipo Ofisini naendelea na mishe zangu na mshahara mwingine nausubiria mwisho Wa Mwezi.
Hizi ni hesabu za nadharia hazina utofauti na kilimo cha matikiti cha mtandaoni.
Hujapiga hesabu kuna spea kuharibika,kupata ajali,kukamatwa na polisi,kuibiwa pikipiki.
Lakini ni bora umeweka wazi kwamba una ajira yako nyingine hiyo bodaboda ni ya ziada tu.
Ila kwa mtu anayeishi kwa kutegemea afanye biashara ya bodaboda ni biashara kichaa.
Sio biashara endelevu na anayenufaika ni dereva tu kwa sababu baada ya mwaka anakuwa mmiliki wa hiyo pikipiki.
 
Okay, ni hesabu za nadharia.
 
Back
Top Bottom