Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Biashara ya chips: Faida na Changamoto zake

Wazo lako ni zuri lakini kwa mtaji ulionao una uwezo wa kuanzisha biashara nzuri na yenye kulipa zaidi ya hiyo...Mimi ni mshauri wa biashara toka CPM business consultant...Kama upo serious na ulichokiandika nicheki kwa 0655040772,Nikufumbue macho.
Mkuu Baraka Rabson .....
sidhani kama ni busara kumwita PM mtu aliyeomba ushauri Public, kama unatoa msaada toa hapa ili watu wengine waweze kunufaika pia. Kumbuka huyu ni mwakilishi tu, wapo weengi wanafuatialia huu Uzi na wana Cash , tatizo ni wazo la biashara,....Kama hutajali elezea hapa.
 
Last edited by a moderator:
Ni kweli kwamba ni vizuri kuweka public ili na wengine wajifunze..lakini mtoa mada yeye ameomba ashauriwe juu ya hizo biashara alizozitaja.Mimi lengo langu ni kumfumbua macho aone na fursa nyingine na mimi nadhani kuliko niandike mpaka nichoke mtu anaweza akanicheki kwa hiyo namba tukashauriana..na ni kwa mtu yeyote si aliyetoa mada tu.0655040772
 
Ila sio wote wapo Tanzania mkuu, au unapatikana whatsapp?
 
Biashara ya chipsi inalipa sana ukipata location nzuri
 
Wazo lako ni zuri lakini kwa mtaji ulionao una uwezo wa kuanzisha biashara nzuri na yenye kulipa zaidi ya hiyo...Mimi ni mshauri wa biashara toka CPM business consultant...Kama upo serious na ulichokiandika nicheki kwa 0655040772,Nikufumbue macho.

Peleka njaa zako huko, na minamba ako, ye kaomba ushaur hapa kwa faida yake yy na wengne pia, mambo ya kuanza muita kwenye ofis ako c ndo kumuibia huko? Nyie mnakula pesa za watu hata wazo la maana hammpi, kma wajiamini shusha nondo hapa watu wapime
 
simwite mtu mwizi wakati hajawahi kukuibia.
Biashara ya simu na vifaa vya simu.

Hii ni moja ya biashara ambayo ni nzuri kufanya ukiwa na mtaji wa mil7.MFANO.. Milioni 3.5 unaweza itumia kwa ajili ya manunuzi ya simu na vifaa vya simu. kwa maisha ya kitanzania simu za mchina ndo zina soko sana kutokana na vipato vyetu kuwa vidogo kwa hiyo simu nzuri kwa ajili ya biashara ni simu za mchina.Mil 3.5 nyingine iliyobaki naweza tumia kwa ajili ya pango pamoja na kuboresha fremu na kununua makabati ya vioo ya kuwekea simu.Kwa kawaida biashara ili ikue kwa haraka ni vizuri uanze kuuza wewe kama wewe kabla ya kuajiri mtu wa kukuuzia kwani anakuwa hana uchungu na biashara na wala hajui huo mtaji umeupata wapi yeye anaangalia maslahi yake.FAIDA.SIMU KWA BEI YA JUMLA UNAWEZA KUTA INAUZWA SHILINGI 45ELFU...WEWE KWA BEI YA REJAREJA UNATAKIWA UUZE 55ELFU MPAKA 65ELFU SASA FIKIRI UKIUZA HATA MFANO CMU TANO KWA SIKU UTAKUWA NA KATI YA ELFU 50 MPAKA 70 JE HAPO NI HASARA????

ANGALIZO; BIASHARA HII INATAKIWA IWE SEHEMU YENYE MKUSANYIKO WA WATU WENGI..AU ENEO LENYE SOKO.

Biashara ya baa.
Biashara hii ni nzuri japo inahitaji mtaji kiasi pia faida ya vinywaji ni ndogo hivyo inahitaji udhibiti wa fedha wa hali ya juu ili usifilisike. Ili ishamiri biashara hii inahitaji ubunifu na usimamizi wa karibu. Matatizo ya biashara hii ni wizi wa makaunta na mameneja wa baa ambapo kama wewe mmiliki hufiki mara kwa mara kupiga hesabu ya mauzo na bidhaa wanaweza kuwa wananunua vinywaji wanaviuza wanachukua faida kisha wanarudisha bidhaa pale pale, ili kukudanganya watakwambia hawakuuza kabisa au wameuza kidogo. Tatizo jingine ni wizi wa kaunta au wahudumu ambao husingizia wamepata shoti wakati fedha wamechukua. Pia panaweza kutokea wizi wa fedha za mauzo kama unakaa muda mrefu bila kufika kwenye baa yako na kupiga hesabu baa kuchukua fedha za mauzo kuna baa ambazo makaunta au mameneja wa baa walitoroka na fedha na mauzo baada ya fedha hizo kuwa nyingi na tajiri kutofika kuzichukua. Kuna wizi wa wahudumu kuwapunnja chenji wateja wakati wamelewa, wahudumu kutorudisha chenji kwa wateja, kuwaibia wateja wakiwa wameelwa na kusinzia, fedha na vitu vyao vya thamani kwa kuwapekua mifukoni, hivyo kuharibu heshima ya baa yako kuwafanya wateja kuikimbia baa yako. Kugeuzwa baa yako kuwa danguro kutokana na wahudumu kufanya umalaya na kuwafanya wateja wenye heshima kuikimbia baa yako, Uchafu kwenye baa hasa upande wa kaunta, jikoni, kwenye vyombo na chooni. Hali hiyo inaweza kukimbiza wateja au baa yako kufungwa na Bwana afya. Kukosekana kwa vivutio katika baa yako mfano kukosekana jiko la kutengeneza mchemsho Chips, nyama choma, burudani ya muziki, michezo kama vile pool table, kamari na drafts ambayo hupendwa sana na wateja kunaweza kuwakimbiza wateja. Kushindwa kuajiri wahudumu wanaoweza kuvutia na kutoa huduma nzuri kwa wateja, pia kunaweza kukimbiza wateja.
Ili kukabiliana na matatizo haya unapaswa kusimamia vizuri biashara yako, Jitahidi ufike kila siku kwenye baa yako upige hesabu na kuchukua fedha za mauzo. Unaweza kuweka sanduku la maoni ili kupata taarifa kuhusu huduma ya baa yako. Changanyika na wateja wakati mwingine bila ya kujitambulisha kwamba wewe ni mmiliki wa baa hiyo ili upate taarifa ya biashara yako.Ajiri wafanyakazi waaminifu,wenye kutoa huduma nzuri na wanaoweza kuvuta wateja. Usivumilie tabia ya wizi,chukua hatua za kinidhamu ukigundua wizi. Weka vivutio katika baa yako kama vile jiko kwa ajili ya nyama choma mchemsho na chipsi, weka michezo kama vile drafts Pool table na kamari. Jenga ukumbi ili kualika vikundi vya muziki ngoma taarab na maigizo kuvutia wateja vikundi hivi vinaweza kuongeza mauzo ya vinywaji na viingilio kwenye ukumbi wako. Ukumbi wako unaweza kuukodisha kwa watu wanaotaka kufanaya sherehe za harusi, Ubatizo na vinginevyo jiepushe na tabia ya kukopa fedha au vinywaji bila kulipa kwani kwa kufanya hivyo unaweza kufilisi baa yako.
 
PUB tafuta wadada wenye mata.ako makubwa uwaweke hapo utauza mpaka useme POOO. Si unaona ROMBO VIEW pale panavyochangamka. na ukihitaji mmojawapo fasta unaacha pesa unatambaa na mzigo fasta
 
Ni kweli kwamba ni vizuri kuweka public ili na wengine wajifunze..lakini mtoa mada yeye ameomba ashauriwe juu ya hizo biashara alizozitaja.Mimi lengo langu ni kumfumbua macho aone na fursa nyingine na mimi nadhani kuliko niandike mpaka nichoke mtu anaweza akanicheki kwa hiyo namba tukashauriana..na ni kwa mtu yeyote si aliyetoa mada tu.0655040772
acha utapel kwan yeye ajui kuna hiz kampun c angekuj moja kwa moja
 
kwel kiongoz hay ndiy mawazo ya wasomi tache kujifany atuwez fany kaz za chin
 
tz wasomi tena degree holderz tupo wengi mtaani na hakuna kaz ila ukibweteka tu kusubiria ajira badala ya kuparangana itakula kwako ts about time tuondokane na mentality ya kuajiriwa cjui kampuni gan suala hapa ni kuprove kama kwel umeelimika kichwan na kubuni biashara yako plus elimu uliyoipata miaka yote hiyo unaamka asubuh kwenda kuifata hyo elimu.
 
BIASHARA YA CHIPS IPO HIVI
Biashara hii inafanywa kwa makubaliana ya kumpangishia kijana mahala pakufanyia kazi,mahitajio yote muhimu km viazi,kalai,sahani,jiko,mafuta na pesa,tomato na vingine ikiwezekana na pesa kidogo ya dharura..sasa kinachotakiwa kwenye mkataba wenu ni kwamba yeye aendeshe hiyo biashara anavyojua yeye ameuza hajauza lazima akupe kiasi fulani ambacho ww utakiona kitafaa kukulipa kwa mtaji uliouanzisha,malipo mtalipana kwa jinsi eneoo la biashara litakavyokuwa aidha kwa siku au kwa wiki is it up to nyinyi..HAKUNA HAJA YA KUMFATILIA WEWE FANYA SHUGHULI ZAKO,ikifika muda wa kukupa fedha yako fasta usichelewe nenda kaichukue...km itakuwa anakupa pungufu ya ile mliokubaliana mvumilie kwa kipindi fulani tu nasi mda mwingi,lingine hakikisha unapata muda wa kuhakiki mtaji km unaendelea vizuri.

MJADALA UMEFUNGWA LETE MADA INGINE.:bump:

daaaaaaaaa....... wew ni mchafu kwa mamipango, yaani maushauri umetisha xan kiongozi hilo ni bonge la mkakat yaan hapo anajiibia mwenyew coz wewe pesa yako iko pale pale
 
Kaka mtoa Mada ndoo moja kubwa ya viazi inatoa sahani ziliso pungua 21 inategema na upimaji ikipingua sana 19 kuwa na daftari ya manunuzi na mauzo chochote kinachonunuliwa kiandikwe na chochote kinachouzwa kiandikwe Hilo ni daftari ambalo itabidi uwe unalipitia kila jioni, na kwasababu biashara Yako ni mpya Mara chache inabidi uwepo eneo husika hata kwa masaa 3 ili uweze kuwafahamu wateja wako na pia wewe mwenyewe kujifunza jinsi ya kuendesha hiyo biashara ni muhimu sana, mfanyakazi wako msome tabia yake, jaribu kumfahamu vizuri ukishaifahamu tabia yake itakuwa rahisi kwako kuishi nae.Na kitu kingine CHA muhimu ukifanya biashara usiwe na mawazo ya kuibiwa kuwa na mawazo chanya hivyo vitu vipo lakini usimfanye mfanyakazi wako akaona Kama humuamini Jenga urafiki lakini linapokuja suala la kazi Kama vitu havijaenda sawa mbadilikie sio kwa kumuogopa ila uwe mkali hasa! Biashara ya chakula itakulipa vizuri weka mipango Yako sawa.

Kwa mkaka ambae ulisema huwezi kuacha kazi kisa biashara ya chips ninayo maneno machache kwako usidharau biashara kubwa 3 ya kwanza ni ya choo,ya pili ni ya chakula na ya tatu ni ya dawa.

Nakutakia Siku njema
 
Yaani nichomwe na mafuta
niungue na moto nigombane na wateja mpaka jioni...alafu nikukabidhi elfu 80 yote alafu pengine mimi unanilipa elfu 5 tu...!!!
Never...lazima nikuibie aiseeee...
 
Kwasasa nipo mwanza wakuu nimefungua na banda la kuuza kitimoto... Vijana biashara yalipa.. Kwa siku unapiga faida sometimes mpaka 50000 as profit. Sometimes petty business payz... Haya maisha kweli ni ku explore opportunities, mtaji ni laki 3 tu ndo nilianza nao.. Nkanunua fridge then na other materials... Tafuta maeneo ya bar au maeneo yenye watu weng inalipa sana..
 
nami pia nataka fanya biashara ya chipsi. nipo kijitonyama natafuta eneo litajakonilipa vzuri kwenye hii biashara. nmezukunguka sana eneo la makumbusho lakini. cjapata sehemu
Wadau wa dar hata mikoani plz kama kunamaeneo mnadhani naweza anzisha hhi biashara ikakua. tafadhari nsaidieni ushauri
 
Kwasasa nipo mwanza wakuu nimefungua na banda la kuuza kitimoto... Vijana biashara yalipa.. Kwa siku unapiga faida sometimes mpaka 50000 as profit. Sometimes petty business payz... Haya maisha kweli ni ku explore opportunities, mtaji ni laki 3 tu ndo nilianza nao.. Nkanunua fridge then na other materials... Tafuta maeneo ya bar au maeneo yenye watu weng inalipa sana..

Siku Mteja akifa na maambukizo ya mafua ya nguruwe Utakaa Butimba mpaka wakusahau.
Badalisha biashara fasta mkuu.

Nguruwe mnyama Hatari sana.
 
Kwasasa nipo mwanza wakuu nimefungua na banda la kuuza kitimoto... Vijana biashara yalipa.. Kwa siku unapiga faida sometimes mpaka 50000 as profit. Sometimes petty business payz... Haya maisha kweli ni ku explore opportunities, mtaji ni laki 3 tu ndo nilianza nao.. Nkanunua fridge then na other materials... Tafuta maeneo ya bar au maeneo yenye watu weng inalipa sana..
Hongera sana
 
Naomba aliyewahi kuifanya aniambie changamoto zake kulingana na eneo alilowahi kufanyia. Nishanunua vifaa na nishampata dogo mmoja, sehemu kuna mchanganyiko wa watu na hela ya kulipia kibaraza sio kubwa maan ninaeka na kafriji!

Sasa nataka kujua ni mambo gani ya kuzingatia, lakini pia nilitaka niweke sehemu kubwa kidogo ila sijapata sehemu ambayo ni classic on the long run nitengeneze brand yangu ya chips, msaada!

Sasa tatizo jingine, nataka kujua changamoto za hii mambo. Japo hii ni biashara yangu ya pili ya msosi ila sio nyanja hii. Please msaada kwa aliyewahi ifanya!
 
Back
Top Bottom