Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

Biashara ya Dagaa: Mjadala wa Uendeshaji, Masoko, Faida, Hasara na Changamoto zake

wanakaa mda gani hadi kuharibika?
Kawaida dagaa waliokaangwa/kukaushwa kwa mafuta huweza kukaa muda mrefu sana bila kuharibika huzidi hata dagaa waliokaushwa kwa jua kawaida kwa ubora ila tunasema "best before"

Huchukua mpaka miezi mitatu bila matatizo ilimradi uzingatie usafi na ukavu wa mahali pa kuhifadhia.


Karibu sana.
 
Kwa mimi nisietumia chumvi mkuu hao hawanifai au mnauza na wasio na chumvi?
 
Kwanini dagaa wa kukaanga ni bora zaidi kibiashara ukilinganisha na dagaa wengine au Samaki.

Kwanza ni bei rahisi
Wanalika hata bila viungo vingine
Hawahitaji maandalizi ukitaka kuwaunga
Ni watamu sanaa (wenye chumvi)
Hawaaribiki kirahisi.
Ni kati ya bidhaa ngeni hasa maeneo yasiyo na ziwa. (wengi wanapenda vyakula vigeni)
Mfanyabiashara utaweza kuwapima katika vipimo tofauti kuendana na soko Lako.

Habari zenu wadau

Pata dagaa safi wakubwa waliokaangwa katika hali ya usafi kabisa.

Dagaa hawa wametiwa chumvi na tunaanza kupima kuanzia debe 5 na kuendelea.

Dagaa wanapatikana Mwanza na utatumiwa mahali popote Tanzania kwa usafiri wa uhakika.

Bei kwa wengi tunauza Tsh 35,000 kwa debe moja na kama utafunga kwenye small containers unaweza mpaka kujipatia 100,000 Tsh

Mawasiliano ni 0622193871 masaa 24/7 press order kubwa mapema ili kupata mzigo kwa wakati.

Nyote mnakaribishwa jumla na rejareja pesa nje-nje.

Mimi nahitaji mkuu
nipo dsm kwa sasa
 
Mkuu, Mimi nipo Dar (Kongowe Temeke) na ninahitaji debe 1 kila week (kwa kuanzia,itategemea biashara itakavyoenda) itakuwa ni beo gani?!
 
Kwa mimi nisetumia chumvi mkuu hao hawanifai au mnauza na wasio na chumvi?
Mkuu tunauza wa kibiashara kwa wingi pia kuwatia dagaa chumvi inasaidia wasiharibike kwa urahisi pamoja na kwamba wanaongeza ladha japo hatuweki chunvi nyingi.

Nakushauri uwatafute dagaa safi wa Bukoba wa kawaida walioanikwa kwenye nyasi juani.
 
Wanakuwaga na michanga hao
Hawana mchanga hawa wa kukaanga sababu wanaanikwa juu ya nyavu kwenye kama vizimba na wakishakauka maji wanawekwa kwenye mafuta hivyo hawaguzi chini wanakaangwa kama samaki wa kawaida.

Karibu sana.
 
Mkuu debe ya dagaa wa kawaida wanaenda kati ya 11,000 mpaka 14,000 kuendana na upatikanaji.
Debe lina Kilo ngapi (NET)?
Na Debe lina gharimu kiasi gani Mpaka lifike Dar es Salaam?
 
Mkuu lugha yako mbona ni technical sana. Unamaanisha nini kuanza giza.
Mkuu wakati wa giza ndio dagaaa huvuliwa kipindi mwezi ni mchanga ili wakiweka taa dagaa wananaswa kwa wingi tofauti na wakati mwezi ni mkubwa au mbalamwezi kunakua na mwanga angani hata wakiweka taa dagaa hawaji kwa wingi sababu ya ukali wa mbalamwezi.
 
Nikupongeze mtangaza fursa,binafsi nitakupigia nipo Arusha tufanye biashara
Mkuu nakukaribisha sana Arusha nafikiri soko ni kubwa sana.
Fanya tuwasiliane mapema sababu huko ndipo nitaleta mzigo siku si nyingi.
 
Debe lina Kilo ngapi (NET)?
Na Debe lina gharimu kiasi gani Mpaka lifike Dar es Salaam?
4 mpaka 4.5 kg
12,000 mpaka 14,000 kuendana na hali ya siku ziwani.
Sasa ukishanunua hilo debe kuna gharama za ushuru, usafiri, upakiaji, n.k
Utapata gharama kamili ukishajua unaweka debe ngapi kwenye kila gunia na ni gunia ngapi.

Karibu sana.
 
Back
Top Bottom