Habari zenu wadau... Leo nataka niwaletee biashara ya kuanza na mtaji mdogo... Biashara ambayo kama wewe Ni mwanafunzi wa chuo au mama wa nyumbani au hata mfanyakazi unaetaka kujipatia kipato Cha ziada itakufaa Sana.. biashara hii usipokua na aibu itakutoa vizuri tuu...
Hii biashara unaweza kuanza na mtaji wa 55,000... Ni biashara ya dagaa...
Kwenye hii ela utapata dagaa ndoo kubwa ambao wanafika kilo kumi...
KWENYE JINSI YA KUWA PACK SASA..
Unaweza ukafunga
gram 100 ukauza TSH 1,000
gram 50 ukuaza TSH 500.....
Sasa kwenye kila kilo moja utapata utapata packet 10 za elfu Moja au packets 20 za 500... Kwenye kila kilo moja utapata faida ya tsh 4500 ambapo kwenye kilo kumi utapata faida ya tsh 45,000 Kama kila week ukiweza kuuza Hadi kilo kumi natano hadi ishirini utajikuta mwisho wa mwezi umesave hela nzuri sanaaa...
Natamani maswali na maoni yote niyajibie humu humu ili hata ambao watakua sio wateja wapate kitu Cha kujifunza..