Kuliko kufanya hii biashara kama una Daladala Kaipige service Ipaki uwe unaikodisha tu kwa shughuli za Jamiii ila sio kusafirisha Abiria tena kwa awamu hiii,waliofaidika na hii biashara ni huko nyuma kuanzia kikwete kurudi nyuma.
Kama una hela za kununua daladala Nakushauri usinunue bora ununue TIPA au CANTER ukaja ipaki huku sokoni nauhakika utapiga Hela mpk hutotaman biashara zingine.
Biashara ya usafirishaji Abiria sio sio dala dala Tu ila mpaka ma BUS ya mikoani ni BIASHARA pasua Kichwa,ukitaka kuuamini hili RUUDI NYUMA miaka mi 5 tafuta MAJINA ya MABUS famous ulokua ukiyajua yako wapi?? wengine wamebadilisha biashara wengine wameyabadilisha MAJINA kwanini sasa yote haya??
Biashara Hii tena ya daladala sijaribu hata kidogo..Ni hela unazoweza pata j3,j4,j5 halafu ALHAMIS trafc wakaichukua yote au Ukaenda kuiacha Garage..sasa shida zote hizo zanini?
Anaetaka hii biashara aifanye ila kwa ushauri wangu biashara pekee inayolipa ktk magari ni ya Usafirishaji MIZIGO wenye malori,fuso,canter,tipa,kirikuu Hao ndo wanapata hela maana mishindo yao ni ya maana na mahali popote wanaenda.
Tofauti na daladala kama umepangiwa RUTI ya USA RIVER to TOWN ndo hyo hyo...kama umepangiwa KISONGO to TOWN ndo hyo hyo kama ni NGARAMTONI to TOWN do hyo hyo huwezi badili RUTI sasa biashara gani hiyo GARI LANGU NINUNUE KWA HELA ZANGU HALAFU UNIPANGIE NJIA YA KUPITA???? Hamna faida utaipata milele barabara moja haiwezi kuwa na wateja kila siku TUSITIANE MOYO. hiii biashara ni UPOTEZAJI WA HELA.