Hakuna serikali ambayo haijawahi kudhibiti... tofauti ni kwamba wengine wanadhibiti kwa mbwembwe na makelele na wengine wanachukulia kama utaratibu wa kazi!
Lakini kubwa zaidi, ni pale watu wanapojaribu kutuaminisha kwamba hili suala linarudi upya as if lilitoweka! Au ndo kama alivyogusia
Lucky Star hapo juu, kwamba zama za JPM wakikamatwa wauza unga mtasema "vita dhidi ya wauza unga ni kali, serikali ipo makini" lakini wakimatwa leo, "biashara imerejea kwa kasi"
Na kama nilivyosema kwenye post yangu, ninaheshimu sana ukamataji kwenye viwanja vya ndege, au ile iliyofanyika kule Kilwa... yaani jamaa wanaotewa kabla hawajaingiza mzigo!
Kinyume chake, nimekuonesha hapo wauza unga waliokamatwa wakati wa JPM, na karibu wote hao, mizigo ilikamatwa majumbani!
Kwa maana nyingine, walipita sehemu zote bila kukamatwa!!! Sasa ulishawahi kujiuliza mtu anapokamatwa na gram kadhaa ndani, mzigo hasa unakuwa wapi?