Biashara ya dawa za kulevya kurejea kwa kasi? Watanzania 2 wakamatwa na Cocaine kilo 2 tumboni Uwanja wa ndege wa Mumbai

Biashara ya dawa za kulevya kurejea kwa kasi? Watanzania 2 wakamatwa na Cocaine kilo 2 tumboni Uwanja wa ndege wa Mumbai

Kwa lipi? Kwamba madawa yaliingizwa baada ya kufa? Tuache unafiki, hizi mambo hazijawahi kuisha, sema tu hawa jamaa wamechukua kilo kadhaa maana haisomeki tani moja tena bali 860kgs
Wewe ndio uache unafiki,vita dhidi ya madawa ya kulevya aliweza kuipunguza kama sio kuimaliza kwa kiasi kikubwa,mkazi yoyote wa jiji la Dar anajua ni kwa jinsi gani vijiwe vingi vya uuzwaji wa madawa ya kulevya vilipungua.
Hata mateja barabarani na vituoni mwa mabasi walipungua sana.Wacheni unafiki, biashara ya madawa ya kulevya tuseme tu kwa sasa inaanza kurudi.
 
Akili zao zinasema hivi:-
Wakati wa JPM ukikamatwa wanakwambia vita dhidi ya madawa ya kulevya ni kali. Serikali ipo makini.
Leo hii ukikamatwa, utasikia biashara imerejea.

Zote hizi ni lugha tu, lakini uhalisia ni kwamba biashara ipo siku zote.
Ingekomeshwa awamu ya 5 tusingeona watu wakikamatwa. Pia serikali ingekuwa haijali (kukumbatia wafanya biashara wa madawa) kama tunavyotaka kujiaminisha, tusingeona watu wakikamatwa pia.
Aisee...

Umeongea jambo la msingi sana!!
 
Kwa masikitiko makubwa naangalia jinsi wasafirishaji wa Madawa ya kulevya wameona kuwa huu ni muda muafaka kuanza biashara yao haramu.

Baada ya lile tukio la kukamatwa kwa kiwango kikubwa zaidi ya tano moja kule lindi ambapo ukisoma muendelezo wake kwenye magazeti utaona hati ya mashtaka imebadilishwa na kuandika kiwango kidogo cha Madawa kuliko kile cha awali.

Watanzania wengine wamekamatwa nchini India 🇮🇳 wakiwa na kilo mbili za cocaine kama chanzo kinavyoonyesha kwenye picha, hii inaenda sambamba na idadi kubwa ya watumiaji ambao wameanza kuonekana katika mitaa yetu. Swali langu ni kwa nini wanadhani sasa ni muda sahihi?

=====

yaani wewe unaamini kuna muda hiyo biashara iliisha au. njoo hapa kwa mfipa , miaka nenda miaka rudi mateja wapo na wauzaji wapo.
polisi wenyewe ni wateja
kuna siku nilitaka kupeleka taarifa polisi, mara paah na wenyewe nikaona mtu ana yunifom kabisa anachukua mzigo
ikabidi nitulizane
 
Ni muda sahihi madhambi yote kurudi.

Juzi nimesikia mpuuzi mmoja akisema "mama amesema kazi iendelee, kwahiyo wanafunzi tutawatia mimba na kesi zitaishia police.

Vibaka, najambazi mitaani wanatamba hawana wa kuwazuia.

Nidhamu ya kazi maofisini imepungua.

Yeyote aliemuona jpm mbaya amini nawaambia miaka itapita mingi sana bila kupata rais makini kama jpm.
Sisemi kwamba hakuwa na mapungufu ya kibinadamu hapana. Ila kazi amefanya alinyoosha nchi akaiweka kwenye mstari.

"Vita ya siasa na uchumi ni ngumu sana"

Jpm aliposema amejitoa kwa wananchi wanyonge kuna watu hawakumuelewa.

"Ukigusa mzinga wa nyuki lazima uumie"

Pole sana jpm.
angedumu milele ili kuzuia hayo yote
 
jpm alidhibiti unga,matundu ni kawaida maana kila sehemu kuna binaadamu wenye tabia zao.

leo utaanza kubishana na watu kwamba hata ujambazi na ujangiri hakuna alichofanya???huo unga ndio umesababisha uhasama mkubwa sana na watu.

na tobo la kwanza la mama kufeli akilegeza hapo.
Hakuna serikali ambayo haijawahi kudhibiti... tofauti ni kwamba wengine wanadhibiti kwa mbwembwe na makelele na wengine wanachukulia kama utaratibu wa kazi!

Lakini kubwa zaidi, ni pale watu wanapojaribu kutuaminisha kwamba hili suala linarudi upya as if lilitoweka! Au ndo kama alivyogusia Lucky Star hapo juu, kwamba zama za JPM wakikamatwa wauza unga mtasema "vita dhidi ya wauza unga ni kali, serikali ipo makini" lakini wakimatwa leo, "biashara imerejea kwa kasi"

Na kama nilivyosema kwenye post yangu, ninaheshimu sana ukamataji kwenye viwanja vya ndege, au ile iliyofanyika kule Kilwa... yaani jamaa wanaotewa kabla hawajaingiza mzigo!

Kinyume chake, nimekuonesha hapo wauza unga waliokamatwa wakati wa JPM, na karibu wote hao, mizigo ilikamatwa majumbani!

Kwa maana nyingine, walipita sehemu zote bila kukamatwa!!! Sasa ulishawahi kujiuliza mtu anapokamatwa na gram kadhaa ndani, mzigo hasa unakuwa wapi?
 
Mchungaji kalala hapo lazima ng'ombe na mbuzi wajiachie kwenyemashamba tutaludi kulekule vijana kuhalibika na kupoteza nguvu kazi ya taifa.

Sent from my TECNO B1f using JamiiForums mobile app
 
"Nasema mtanikumbuka! sio kwa mabaya bali kwa mema."

Maneno haya alipata kuyatamka mwendazake.Bado kidogo Twiga wataanza kupakiwa ndege na viroba vya dhahabu vitaanza kupakiwa kwa ndege!
Mwendazake alikuwa fisadi kuu, jitu lenye roho mbaya na chuki, Mungu kasikia kilio cha watanzania kamnyakua akaongoze kundi la watu wa jehenam kuitia waovu wenzao
 
Kwa lipi? Kwamba madawa yaliingizwa baada ya kufa? Tuache unafiki, hizi mambo hazijawahi kuisha, sema tu hawa jamaa wamechukua kilo kadhaa maana haisomeki tani moja tena bali 860kgs
Jifunze kupongeza panapo Jambo zuri.

Huoni hata mateja mtaani wamepungua na wengine wanameza dawa Muhimbili, Mwananyamara n.k?
 
Mtandao wa biashara ya madawa ya kulevya haukuwahi kupungua hapa Tanzania kiuhalisia, umeendelea kuwepo lakini kwa style tofauti. Habari na matukio yake zinaweza kuwekwa wazi sasa kwa sababu utawala kwa kiasi uko huru kuyasimulia au zinaweza kufichwa kwa woga wa kumchafua mtawala (hili lilikuwa kwa Magufuli).
Unalazimisha Jambo ambalo huna uhakika nalo.

Jifunze kutunza akili uitumie kwa mambo mengine
 
Wewe ndio uache unafiki,vita dhidi ya madawa ya kulevya aliweza kuipunguza kama sio kuimaliza kwa kiasi kikubwa,mkazi yoyote wa jiji la Dar anajua ni kwa jinsi gani vijiwe vingi vya uuzwaji wa madawa ya kulevya vilipungua.
Hata mateja barabarani na vituoni mwa mabasi walipungua sana.Wacheni unafiki, biashara ya madawa ya kulevya tuseme tu kwa sasa inaanza kurudi.
Hujui unachokisema wala hustahili kujibiwa na mimi
 
Umewaza Kama Mimi ambaye naona haya yalikuwa Kama hidden story lkn ni wala tatizo halikutatuliwa ht kwa robo kiwango...unga ni unga tu na hela yake ni ya maungaunga
Sasa hao kenge wachanga hapo juu wananijibu ujinga eti niache unafiki nipongeze
 
Hakuna serikali ambayo haijawahi kudhibiti... tofauti ni kwamba wengine wanadhibiti kwa mbwembwe na makelele na wengine wanachukulia kama utaratibu wa kazi!

Lakini kubwa zaidi, ni pale watu wanapojaribu kutuaminisha kwamba hili suala linarudi upya as if lilitoweka! Au ndo kama alivyogusia Lucky Star hapo juu, kwamba zama za JPM wakikamatwa wauza unga mtasema "vita dhidi ya wauza unga ni kali, serikali ipo makini" lakini wakimatwa leo, "biashara imerejea kwa kasi"

Na kama nilivyosema kwenye post yangu, ninaheshimu sana ukamataji kwenye viwanja vya ndege, au ile iliyofanyika kule Kilwa... yaani jamaa wanaotewa kabla hawajaingiza mzigo!

Kinyume chake, nimekuonesha hapo wauza unga waliokamatwa wakati wa JPM, na karibu wote hao, mizigo ilikamatwa majumbani!

Kwa maana nyingine, walipita sehemu zote bila kukamatwa!!! Sasa ulishawahi kujiuliza mtu anapokamatwa na gram kadhaa ndani, mzigo hasa unakuwa wapi?
hamna tatizo muda ni mwalimu mzuri.

nimekupa mfano wa ujangiri na ujambazi,kwa makusudi unauruka ili dhana yako isiingie doa.

kazi za mtu huwa zinaongea,kuziita makelele na maonyesho ni maamuzi ya mtizamaji.
 
Back
Top Bottom