Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Hilo duka utauza mwenyewe au utaajiri mtu? Kama utauza mwenyewe hela utaiona, kama utaajiri mtu bac weka maxmum mwaka mmoja utakuwa huna duka.. [emoji4][emoji4][emoji4]
Sio kila siku ni jumapili ila matairi ya gari ndo hayana rangi nyingine zaidi ya nyeusi. Duka siuzi mwenyewe anauza mdogo wangu na kwa miezi miwili na sasa watatu tutaumaliza soon mambo yanaenda kama nilivyosema hapo juu. Bora kuwa positive kwa kutoa changamoto na suluhisho lake. Yes tunajua kama ukiajiri mtu hasa kwa maduka haya anaweza kukuulia mtaji, na si wote wanaweza kufanya hivyo. Mazingira unayoyaweka mwenyewe kwenye duka, na jinsi ulivyo mgroom huyo muuzaji ndo yatakuwa maamuzi wa mwendelezo wa biashara yako.
 
Acha kabisa. Mimi mara ya kwanza nilifungua Manzese. Ila washirikina walinifanya nifunge nikahamia nilipo sasa.
Mimi ushirikina ulinifanya nifunge duka,nilizungukwa na maduka ya washirikina cha moto nilikiona,Najipanga nitafute sehemu nyingine nifungue tena,Vina faida sana hivi vidude ukipata site nzuri!
 
Hii software inaitwaje na upatikanaji wake upo vipi?
 
Asante Mkuu kwa mawazo je nikiwa Na m.1.5 naweza kuanzisha duka la reja reja ondoa kodi ya flem.hiyo kwa bizaa tu.
 
Safi, naona watu walikuwa wanaenda different na matakwa yako, but biashara inaendeleaje now.
 
km wataka watu waje PM,sasa maana ya kufungua huu uzi ni nini?
 
Safi, naona watu walikuwa wanaenda different na matakwa yako, But biashara inaendeleaje now..
So far so good mkuu....line of business zote nilizotaka nimeshaziweka kasoro ya gas tu ndo naitafakari bado na kuisoma. Ila mambo ni mazuri kuliko hata maximum target nilizoweka.
 
Asante Mkuu kwa mawazo je nikiwa Na m.1.5 naweza kuanzisha duka la reja reja ondoa kodi ya flem.hiyo kwa bizaa tu.
Inatosha sana mkuu ni nyingi sana ya kuanzia hiyo. Kikubwa ni kuwa unachukua bidhaa kidogo kidogo. Mfano kama bidhaa zinauzwa kwa carton unaweza kuchukua nusu au dasani unchukua nusu nakadharika.
 
Inatosha sana mkuu ni nyingi sana ya kuanzia hiyo. Kikubwa ni kuwa unachukua bidhaa kidogo kidogo. Mfano kama bidhaa zinauzwa kwa carton unaweza kuchukua nusu au dasani unchukua nusu nakadharika.
Mkuu utafanikiwa sana kwakuwa siyo mchoyo wa mafanikio.
 
""Kazi yangu ya dukani yaniweka matatani wanaonirudisha nyuma wengi wao ni majirani""

In ubongo wa fuleva voice!!
 
Wawekee wateja maziwa ya unga ya kupima na prestige ya kupima wakikuzoea utanikumbuka
Plse naomba niambie kwa jumla yanauzwa bei gani, halafu nikiuza kwa kupima (sijajua kama ni kwa kilo au kikombe) unauzaje ili nipate faida?
 
Plse naomba niambie kwa jumla yanauzwa bei gani, halafu nikiuza kwa kupima (sijajua kama ni kwa kilo au kikombe) unauzaje ili nipate faida?

Sijui mie nimezowea kununua maduka ya wapemba na yana wateja. Prestige ni nzuri kuliko blueband

Wanapima kwenye kilo, unanunua ile ndoo unapima ina kilo ngapi unaangalia bei uliyonunulia kisha utaangalia utauzaje upate faida
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…