Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Hilo duka utauza mwenyewe au utaajiri mtu? Kama utauza mwenyewe hela utaiona, kama utaajiri mtu bac weka maxmum mwaka mmoja utakuwa huna duka.. [emoji4][emoji4][emoji4]
Sio kila siku ni jumapili ila matairi ya gari ndo hayana rangi nyingine zaidi ya nyeusi. Duka siuzi mwenyewe anauza mdogo wangu na kwa miezi miwili na sasa watatu tutaumaliza soon mambo yanaenda kama nilivyosema hapo juu. Bora kuwa positive kwa kutoa changamoto na suluhisho lake. Yes tunajua kama ukiajiri mtu hasa kwa maduka haya anaweza kukuulia mtaji, na si wote wanaweza kufanya hivyo. Mazingira unayoyaweka mwenyewe kwenye duka, na jinsi ulivyo mgroom huyo muuzaji ndo yatakuwa maamuzi wa mwendelezo wa biashara yako.
 
Acha kabisa. Mimi mara ya kwanza nilifungua Manzese. Ila washirikina walinifanya nifunge nikahamia nilipo sasa.
Mimi ushirikina ulinifanya nifunge duka,nilizungukwa na maduka ya washirikina cha moto nilikiona,Najipanga nitafute sehemu nyingine nifungue tena,Vina faida sana hivi vidude ukipata site nzuri!
 
Nilifanikiwa mkuu naendelea mdogo mdogo. Kifupi bidhaa huwa nanunulia maduka ya jumla pale Manzese Tip top na darajani na ndo nilienda kuna wauzaji waungwana sana wakanipa list zote na utaratibu wa kupanga bei.

Kuna jamaa walijitokeza humu kunisaidia ambao nilitaka niwape elfu 40,000 ila nikaona wazugaji tu. Mara tuma kwanza pesa mara njoo tuonane hii kasi sio rahisi kama unavyofikiri na wakati mimi nilitaka mtu aniandalie excel file yenye bidhaa zote na bei ya kununulia na kuuzia na wapi nikanunue alafu nampa hiyo 40,000 simple tu. Watu wagumu kweli. Baada ya kuona longo longo hizi na mimi ni mtu aisiyetaka complication na mtu wa kuyaona mambo hata magumu kuwa ni marahisi nikaachana nao nikaingia mwenyewe chimbo madukani na kwenye maduka ya akina mangi na kuulizia. Wengine walinifukuza na wengine walikataa kata kata hata kwa kuwalipa. Ila kwa vile penye nia pana njia nilifanikiwa. Na kwa vile sina hiyana na tamani watanzania wenzangu watamanio kuifanya hii biashara waifanye bila longo longo nyingi nimeweka hapa baadhi ya bidhaa ambazo nimezidowload kwenye accounting software ninayotumia dukani. So far so good nilianza na mauzo ya siku ya kwanza ya shilingi 10,200 nikala faida ya buku mbili kwa siku na kwa sasa in average mauzo ni 70,000 kwa siku with average profit ya 30% ambayo ni 21,000 kwa siku.

Nenda kafungue mkuu na niulize nikwambie ninayoyajua so far kwa hii experience ya miezi mitatu.

Karibu sana

Mkomamazu
Hii software inaitwaje na upatikanaji wake upo vipi?
 
Asante Mkuu kwa mawazo je nikiwa Na m.1.5 naweza kuanzisha duka la reja reja ondoa kodi ya flem.hiyo kwa bizaa tu.
Nadhani zamani kwa siku hizi mkuu sijui japo nadhani ni bora ukapambana upate chochote chako uanze biashara hiyo baadae kama unataka kuendelea ndo ukakope. Ila wazo tu bila uzoefu wa biashara kwa waswahili wa mabenki yetu hapa sijui kama inawezekana. Maana siku hizi watu wanachukua business plan online wanazi - customize kwenye idea zao na wengi wanakuwa na wasiwasi na feasibility ya kitu mpaka waone. Kukopa ili uanze biashara mimi sishauri sana bora upambane hata kama ikubuma unakuwa huna deni na mtu. Nimefanya hivyo maraja nyingi na zimenibumia na wala sidaiwi na mtu.
 
Nashukuru sana. Ila mimi hii biashara ya rejareja nimefanya utafiki kidogo hapa mtaani itanifaa sana maana hakuna duka la rejareja karibu lilopo liko mbali kidogo na service yake sio nzuri na linafungwa mara kwa mara na kuwalazima jamaa kutembea umbali mrefu kufuata huduma. Ni biashara ambayo nina passion nayo mda mrefu na sitauza vitu hivi tu ila nitaweka na gesi, huduma za kutuma na kupeka pesa na vocha za kurusha. Kwa sasa zinapatikana mbali kidogo kama gesi lazima upande boda boda kuifuata. Nadhani ni vizuri nikashauri kuwa nielekezwe na kushauriwa na wanaoifanya hii biashara na ushauri ujikite kwenye hii biashara maana nimeomba kusaidiwa list ya vitu kwenye hii biashara na sijaomba wazo la biashara. Hatua ya wazo la biashara nimeshatoka huko.
Safi, naona watu walikuwa wanaenda different na matakwa yako, but biashara inaendeleaje now.
 
Wadau naomba kama kuna mtu anafanya biashara ya duka la rejareja kwenye makazi ya watu anisaidie list ya bidhaa dukani nikahemee. Nataka kufungua duka la rejareja mtaani kwangu nimeshaandaa fremu na mambo mingine kilichobaki ni kuchukua mzigo. Unisaidie bidhaa zinazotoka sana dukani. Najua maeneo yanatofautiana ila kwa makazi yetu watu wa wastani na kawaida nadhani mahitaji yetu yanafanana. Duka nalifungua maeneo ya kibamba. Nimetenga milioni 5 ya mzigo na nitashukuru kama utanisaidie na bei za jumla za kuchukua mzigo ili nijue nichukue kiasi gani na mahali unapochukulia pia. Natambua taarifa ni mali, hivyo nimetenga elfu 40 kwa atakaenisaidia hili. Ni PM. I will pay you seriously. Nahitaji anaefanya biashara hii tafadhali.
NB supplier wa unga na mchele nishampata
km wataka watu waje PM,sasa maana ya kufungua huu uzi ni nini?
 
Safi, naona watu walikuwa wanaenda different na matakwa yako, But biashara inaendeleaje now..
So far so good mkuu....line of business zote nilizotaka nimeshaziweka kasoro ya gas tu ndo naitafakari bado na kuisoma. Ila mambo ni mazuri kuliko hata maximum target nilizoweka.
 
Asante Mkuu kwa mawazo je nikiwa Na m.1.5 naweza kuanzisha duka la reja reja ondoa kodi ya flem.hiyo kwa bizaa tu.
Inatosha sana mkuu ni nyingi sana ya kuanzia hiyo. Kikubwa ni kuwa unachukua bidhaa kidogo kidogo. Mfano kama bidhaa zinauzwa kwa carton unaweza kuchukua nusu au dasani unchukua nusu nakadharika.
 
Inatosha sana mkuu ni nyingi sana ya kuanzia hiyo. Kikubwa ni kuwa unachukua bidhaa kidogo kidogo. Mfano kama bidhaa zinauzwa kwa carton unaweza kuchukua nusu au dasani unchukua nusu nakadharika.
Mkuu utafanikiwa sana kwakuwa siyo mchoyo wa mafanikio.
 
Wawekee wateja maziwa ya unga ya kupima na prestige ya kupima wakikuzoea utanikumbuka
Plse naomba niambie kwa jumla yanauzwa bei gani, halafu nikiuza kwa kupima (sijajua kama ni kwa kilo au kikombe) unauzaje ili nipate faida?
 
Plse naomba niambie kwa jumla yanauzwa bei gani, halafu nikiuza kwa kupima (sijajua kama ni kwa kilo au kikombe) unauzaje ili nipate faida?

Sijui mie nimezowea kununua maduka ya wapemba na yana wateja. Prestige ni nzuri kuliko blueband

Wanapima kwenye kilo, unanunua ile ndoo unapima ina kilo ngapi unaangalia bei uliyonunulia kisha utaangalia utauzaje upate faida
 
Back
Top Bottom