Nilifanikiwa mkuu naendelea mdogo mdogo. Kifupi bidhaa huwa nanunulia maduka ya jumla pale Manzese Tip top na darajani na ndo nilienda kuna wauzaji waungwana sana wakanipa list zote na utaratibu wa kupanga bei.
Kuna jamaa walijitokeza humu kunisaidia ambao nilitaka niwape elfu 40,000 ila nikaona wazugaji tu. Mara tuma kwanza pesa mara njoo tuonane hii kasi sio rahisi kama unavyofikiri na wakati mimi nilitaka mtu aniandalie excel file yenye bidhaa zote na bei ya kununulia na kuuzia na wapi nikanunue alafu nampa hiyo 40,000 simple tu. Watu wagumu kweli. Baada ya kuona longo longo hizi na mimi ni mtu aisiyetaka complication na mtu wa kuyaona mambo hata magumu kuwa ni marahisi nikaachana nao nikaingia mwenyewe chimbo madukani na kwenye maduka ya akina mangi na kuulizia. Wengine walinifukuza na wengine walikataa kata kata hata kwa kuwalipa. Ila kwa vile penye nia pana njia nilifanikiwa. Na kwa vile sina hiyana na tamani watanzania wenzangu watamanio kuifanya hii biashara waifanye bila longo longo nyingi nimeweka hapa baadhi ya bidhaa ambazo nimezidowload kwenye accounting software ninayotumia dukani. So far so good nilianza na mauzo ya siku ya kwanza ya shilingi 10,200 nikala faida ya buku mbili kwa siku na kwa sasa in average mauzo ni 70,000 kwa siku with average profit ya 30% ambayo ni 21,000 kwa siku.
Nenda kafungue mkuu na niulize nikwambie ninayoyajua so far kwa hii experience ya miezi mitatu.
Karibu sana
Mkomamazu