Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Wawekee wateja maziwa ya unga ya kupima na prestige ya kupima wakikuzoea utanikumbuka
Prestige ya kupima!
Sijawahi iona. Huona prestige za makopo sealed, hizi za kupima zinakuwa kwenye ujazo gani?
 
Mkuu hizi kanuni ulizoeleza hapo zinawahusu hata wenye mitaji chini ya m.4?
 
GOOD
 
Ni rahisi kwake kujua faida anayoipata kwani awali kabisa wakati anaanza biashara alihesabu kila bidhaa alizozileta kisha akajua bei aliyonunulia kila bidhaa na bei atakayouzia. Hivyo, aliweze kujua faida ya kila bidhaa moja moja. Kisha akawa anarekodi kila siku vitu anavyouza. Mfano kama kitu kanunua 250, ye anauza kwa 500. Hapo faida ni 250 so kama leo kauza hivyo vitu kwa siku 10 means ana faida ya 2500.

Kikubwa na cha msingi katika biashara yoyote no matter how small it is, kutunza kumbukumbu ya mauzo na matumizi yako ya biashara ni muhimu ili kujua kama mwenendo wa biashara yako.
 
Very true. Shida moja kubwa binadamu tunakosa uthubutu and that's the biggest problem vijana wa sasa tunalo. We don't want to take risks. Mtu badala ya kuchukua mafunzo anataka kujua progress akiamini kufanikiwa kwako basi naye akifanya ulichofanya atafanikiwa kama wewe.
 
Uzi bora kwangu kila siku maana lazima niupitie kupata nondo mpya, asante nyote mnaochangia
 
Duuuuu sasa hiyo si ni hatari...! Matumizi yanaweza kuzidi faida
 
Mkuu kama hujui jambo bora ukakaa kimya, mimi hizi ndio biashara zangu, hiyo kwa rejareja faida yake si chini ya 20% labda uwe unauza bei za chini ya zilizozoeleka, na hiyo jumla ndio ina faida ndogo sana, faida zake ni 7% mpaka 12%, hapo inategemea na aina ya biashara.

Reja inayolipa zaidi ni vipodozi na baadhi nyinginezo ambazo ni za kupatania bei hasa ukiwa eneo zuri ya vitu maduka vitu vidogo mtaani bei zake zinajulikana
 
Kama umeshaweka hivyo vitu utakua umeelewa komenti yangu mkuu, na faida zake zilivyo...
 
Duka la rejareja faida yake ni ndogo mnooo,kwa mfano waweza uza laki tatu kwa mwezi ukapata faida 15000 tuu.Kwa mm ninavyoona fanya biashara ya kitu kimoja kingi uuze kwa jumla mfano viazi toka Mbeya to dar,au maharage na nafaka nyingine.
Sio kweli mkuu, hizi biashara nmefanya mwaka wa 10 huu sijaona faida ndogo hivyo, kwenye laki hukosi 20
 
Asante Mkuu
 
Nashukuru na wewe uliliona kuna wadau wanakatisha tamaa sana wakati biashara hawazijui, hongera mkuu kwa kutokatishwa tamaa
 
Nunua daftari chora jedwali lenye tarehe, manunuzi, mauzo, faida, na matumizi utagundua kila kitu, ukiona umenunua mzigo wa laki 1 ukaandika faida yake ikawa elfu 20 au ziadi au pungufu kidogo ujue siku ukiwa na mauzo hayo faida yake inacheza hapo kwenye elfu 20...
 
Sio kweli biashara ipo hivi ulieka mtaji wala laki 5 hiii leo mtaji unasomeka laki 9 hivyo ww biashara yako inaongezeka ila huchunguzi
 
Mkuu hizi kanuni ulizoeleza hapo zinawahusu hata wenye mitaji chini ya m.4?
Na wewe fanya homework kidogo bana....si umesikia kila siku kuwa vitambulisho vya wafanyabiashara wanapewa wenye mtaji chini ya 4,000,000! sasa ukiwa nacho hicho si ndo umemaliza kila kitu au? Sina hakika ya njia wanayopitia ila nadhani haihitaji process zote hizo.
 
Nipo kwenye hii biashara (rejareja). Nimefanya kaubunifu flan ka kuongeza maziwa ya mgando ya mgando na cake tam baada ya kugundua kuna uhitaji. Nasubri laini zang za figo pesa na Mpesa. Vyote hv (maziwa, figo, m-pesa) nimefanya kwaajil ya kujiingizia pato tengefu au la pemben. Mfano maziwa kwa mwez (predictably) napata si chin ya laki na nimeanza wik 3 zilzopta Expecting to increase kwa upande wa tigo na m-pesa sijajua maana sijawahifanya na lain zang hazijatoka bado miez 2 ss hvyo mwnye uzoefu naomba kujua pato lake kwa mwezi.

Hapa pia naomba kuongezewa ubunifu mwngine wa biashara nyingine simple kama ya hyo maziwa itakayo nipa kuanzia laki (100, 000) kwenda juu.

Asanteni.

Note:
Duka lina miez 3 ss.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…