Tafuta fremu fungua duka....nenda TRA kaombe TIN number (siku moja tu unapata), watakupa tax clearance nenda halmashauri kaomba leseni ya biashara ndani ya siku saba unapata na gharama ni 70,000 tu. Then waulize hapo halmashauri bibi afya yuko wapi ili wakupe certificate ya afya maana wanasumbua baadae kama huna cheti cha afya. Kwangu walikuja wanataka kunipiga faini eti kwanini nauza unga na maharage sina cheti cha afya... uduanzi kabisa. Ila niliwafuata wakanipa. Then pale dukani nunua dust bin la uchafu la kuweka maganda ya pipi, chupa za maji nini nakadharika ili wasije jamaa kukupiga faini maana siku hizi pesa baba inatafutwa kama nini. Then fungua duka kula vichwa hapo....mambo ya kisheria yameishai hapo. Kitambulisho mimi sikuchukua maana mtaji wangu ni zaidi ya milioni 4 kwa mwaka na wala sitaki umasikini na kusumbuana na watu....
Ajabu juzi walikuja watu wa halmashauri ya ubungo wakawa wamejaza form eti wanasema nauza duka bila kulipa service levy. Na wakawa wamesaini kwenye karatasi eti nimekubali nilipe faini 380,0000/-. Nikawaambia kuwa kwa nini mimi nilikuja kuomba leseni pale Halmashauri hamkuniambia kuhusu mambo ya service levy? na iweje wewe usaini siani yako kwa kuandika jina langu alafu useme mimi nimekubali. Nikawaambia kuwa utaratibu ni nyie kunipa elimu alafu niende kama natakiwa kulipa service levy nilipe sio kuja na kunitisha na makaratasi mengi alafu unataka pesa on the spot 380,000/-. Tulizinguana wakaondoka hawajarudi mpaka leo na wala sijui kama natakiwa kulipa service levy au la!!! Ila acheni bana wafanyabiashara wanateswa na hawa watu wanajiita manispaa duhhhh....ila nakomaa nao tu ninapoelewa tunaenda sawa nisipoelewa mtiti kweli kweli mpaka nielewe....huwa sitoi pesa hivi hivi