Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

Biashara ya Duka la Rejareja: Ushauri, Mchanganuo, Changamoto na Namna ya Kutunza Kumbukumbu

uzi nzur sana mods upelekeen jukwaa la. biashara
tupate ideas zaid
 
Habari wana jamvi, nahitaji kufungua biashara ya duka la rejareja mahitaji ya nyumbani. Naomba mwongozo maduka ya jumla yako wapi jijinibdar es salaam mimi ni mgeni.

Maduka ya vitu kama sabuni, baby diapes,betri. Achana na vitu vya kupima kama nafaka, hivyo nimekuja navyo toka Tanga nimehamisha duka.

karibuni kuchangia wajameni.

sijapata jibu wajameni..... msaada kama mnafahamu hizo chimbo
 
Habari za jion wadau nataman sana kujua faida za maduka ya vyakula vya majumbani madogo maarufu kama maduka ya mangi faida yake ipo haswa kwenye bidhaa gani maana naamin faida ipo hata kama ni kwa kiasi flan maana wenzetu hawa wachagga ndo unakuta analitigemea hilo na maisha yanaenda wakati mwingine mpka kujenga nyumba maeneo ya mjin pasipo kusahau mwisho wa mwaka kwao kama kawaida.

Tujuzane mambo ya kuzingatia katika kuyaanzisha ikiwemo location, mtaji pamoja na faida.
 
Habari wadau;
Leo nizungumzie kidogo kuhusu boashara ya reja reja ya maduka ya bidhaa za matumizi ya nyumbani kama mchele,unga sabuni,nakadhalika.

Unapotaka kufungua aina hii ya duka ni lazima kwanza utambue eneo unalotaka kufungua je ni eneo la watu wenye kipato au watu wa hali ya chini,je ni eneo lenye mzunguko wa watu ni eneo ambalo halina mzunguko wa watu.

Kwa sababu za kiuchumi huku kwetu Super market culture bado haijakuwa vizuri kwa hiyo basi maduka haya yanauza sana.Unapotaka kufungua biashara hii haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia.
  1. Kodi ya fremu ya duka la reja reja yapaswa kuanzia shilingi 30,000 kwa mwezi hadi shilingi 150,000 kwa mwezi iwapo imazidi hapo ni lazima uwe na hakika kuwa eneo lina mzunguko wa uhakika.
  2. Leseni ya duka la rejareja ni kati ya shilingi 50,000 hadi 200,000
  3. Kodi kwa duka la rejareja inayolipwa TRA inaanzia shilingi 300,000 kwa mwaka kutegemea na makadirio ya mapato yako
  4. Kuna vitu vya aina mbili katika duka la rejareja,kwanza ni vitu vya kupima ambavyo ni muhimu zaidi kama vile unga,mchele,mafuta taa,maharagwe n.k.hivi unaweza kuviwekea mtaji wakuanzi shilingi 450,000 hadi shilingi 900,000 kutegemea kiasi na uwezo na pili ni vitu ambavyo si vya kupima mwenye kama vile sabuni,mafuta ya kupikia,sabuni za unga,sabuni za kuoga,lotions na mafuta ya kupaka,dawa za mswaki,viberiti,stili waya,mishumaa,soda,maji na vifaa vidogo vidogo.Hivi unaweza kuviwekea mtaji wa kati ya shilingi 600,000 na 1,500,000
  5. Kama una uwezo ongeza huduma za Mpesa,na uuzaji wa LUKU
  6. Unaweza kuhitaji kuwa na FRIJI,MIZANI,MASHINE YA KUUZA LUKU ambavyo unaweza kuvitengea mtaji wa angalau TZS 1,500,000
Jambo la muhimu katika duka la rejareja ni kuhakikisha kuwa unaweka kumbukumbu za manunuzi na mauzo ya kila siku na kama unaweza kufunga stock basi funga stock kila baada ya miezi mitatu au unaweza kufunga stock kwa kuchagua upande wa duka yaani,vitu vya kupima peke yake na vitu vya mashelfu peke yake.Vile vile hakikisha unaweka mtu muaminifu unamfuatailia hasa kwenye mauzo na iwapo unasimamia mwenyewe usipende kutoa pesa za dukani kwa matumizi ya nje bila kujua katika mauzo hayo faida yako ni kiasi gani.

Kwa kawaida vitu vingi vya dukani profit margin yake ni ndogo sana hivyo kwa ajili ya makadiria weka margin ya 0.5 % mpaka 5% na hapo utajua iwapo mauzo yako yanakupa faida kiasi gani.

Tuendelee na mjadala
 
Habari zenu wakuu

Kwa wakazi wa songea mjini, nina wazo la kutaka kuanzisha duka la rejareja vitu vya matumizi ya nyumbani .
Tatizo Mimi sio mwenyeji sana songea hii, nilikuwa naomba kama kuna mwenyeji aniambie location nzuri nayoweza kufanyia biashara hii na frame pia ziwe zinapatikana.

Lakini pia kama una idea nzuri tofauti na hili unaweza nishauri.
Asanteni wakuu.

Mtaji wangu ni mil 1.5
 
Kijana Mimi binafsi huko sipa faham vizur ila Ni mwenyeji wa k'njaro na Dar hata mikoa mingne pia tofaut na huko.

WAZO LANGU KWAKO

Mahali kama hapa Dar, una weza anzisha hata saluni mbili kwa hela yako Hiyo. Una Fanya hvi,, unafungua ofisi ya kawaida sana maana saiv vyuma vime kaza kwahyo watu wengi hawapendi Kwenye saluni za gharama sana.

Tafuta vijana uwaweke pale kila siku wana kulipa wewe eg 9000@ saluni moja,, ambapo una kuta Ni 18000 kwa siku,, hebu piga Mara wki then Mara mwezi,, hhehehehheh,, hata Bachelors' holder haku fuati hata kidogo,,

Faida ya hii biashara.
1. Una kua free kufanya mambo mengne
2. Hakuna kinacho oza hapo kama biashara ya nyanya
3. Na zingine nyingiii.

NB: Nina experience 100% so kama una swal au kama Kuna mwingne ambae pia ana mtaji wake na Yupo interested kufanya hyo biashara ana ruhusiwa kuuliza chochote.

0763885349
 
Back
Top Bottom