Biashara ya duka stress tupu

Biashara ya duka stress tupu

TEAM 666

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2017
Posts
4,399
Reaction score
8,594
Habar wana JF

Hii biashara ya duka dah ni biashara nzuri but imejaa hofu kibao kwanza wenyewe kwa wenyewe mnarogana

Chengine jamii inatuchukulia sisi wenye maduka tuna Uhuru wa kipesa lakini si kweli uhalisia tuna mashaka sana.

Hii biashara ya duka haina future nzuri miaka nenda miaka rudi unakaa tu dukani mambo kibao mtaani yanakupita unabaki kusimuliwa tu

Kiukweli bora ufanye poultry
Naomba niweke kumbukumbu sawa nafanya biashara ya duka mwaka wa 3 sasa na inaenda vizuri ila na inanipa faida nzuri tu

Ila haina free time yaani no bataz muda wote upo shop

But my future naanza kukita mizizi kwenye poultry cuz ndio itanipa free time
 
Akili zako maziwa mgando, achana na biashara ya duka sasa kawe mpiga debe ili usiwe unakaa sehemu moja.
.
Kurogwa ni unajiroga mwenyewe na hautofanikiwa kamwee. Biashara inaendeshwa na ubunifu na utayari, ingekuwa hayo unayoyaamini ni ya kweli maduka mengi ya kariakoo yasingekuwepo WEWE UMELAANIWA AKILI MPAKA MWILI
 
Ukiona mtu anaendesha biashara ya duka rejareja(nadhani vyakula Kama mtoa mada amekusudia hivyo) kwa muda wa miaka 3 na linaendelea vizuri mpe heshima yake.

Hii biashara watu wanaweza sema ni rahisi ila ni biashara ngumu Sana inayohitaji akili maana ukicheza kidogo tu unafunga.

Wengi imewashinda kwasababu hajui njisi ya kuiendesha, kwenye mauzo atataka ale hapo hapo atachota sukari, hapo hapo atachukua sabuni ,chumvi, unga n.k kwa matumizi ya nyumbani ila haesabu , yeye anahesabu alizouza tu na tatizo linaanzia hapo.
 
Akili zako maziwa mgando, achana na biashara ya duka sasa kawe mpiga debe ili usiwe unakaa sehemu moja.
.
Kurogwa ni unajiroga mwenyewe na hautofanikiwa kamwee. Biashara inaendeshwa na ubunifu na utayari, ingekuwa hayo unayoyaamini ni ya kweli maduka mengi ya kariakoo yasingekuwepo WEWE UMELAANIWA AKILI MPAKA MWILI
Lazima utakuwa muuza duka we
 
Habar wana Jf


hii biashara ya duka dah ni biashara nzuri but imejaa hofu kibao kwanza wenyewe kwa wenyewe mnarogana


Chengine jamii inatuchukulia sisi wenye maduka tuna Uhuru wa kipesa lakini si kweli uhalisia tuna mashaka sana.


Hii biashara ya duka haina future nzur miaka nenda miaka rudi unakaa tu dukani mambo kibao mtaani yanakupita unabaki kusimuliwa tu



Kiukweli bora ufanye poultry
Mimi niko ktk biashara hizi za maduka leo mwaka wa 10, ila nilichogundua duka lazima ukubali kupitwa na mengi yanayojili maana ukisema uajili hawa vijana au watu wa dunia ya sasa hata kama ni ndugu yako atakuibia tu mtaishia kulaumiana bora kukomaa ww na mkeo tu kama umeoa.. Ukitoka au ukichoka funga tu ujue moja kuliko kumuachia mtu litaisha.. Ila ukishaona umepiga hatua hata ukimuweka mtu akakuibia huta yumba unawez ajili.
 
Sikubaliani na Mtoa mada;

Binafsi nna biashara ya duka, na huwa nakaa dukani.

Biashara ya duka itakuboa pindi kutakapokua na mzunguko mdogo,

afu wateja hawaji na huna chochote ndani ya duka lako kurefresh mind. MF: kucheck TV,kuchat n.k

Ila kama mzunguko upo, na wateja wanapishana kila Mara mlangoni.

Unakua kama unadownload tu pesa dukani.

WALLAH UTAIPENDA SANA BIASHARA YA DUKA MAISHA YAKO YOTE.
 
Back
Top Bottom