Biashara ya kuanzia mtaji milion 200

Biashara ya kuanzia mtaji milion 200

habari wanajamii wenzangu ,,, nngependa kupata mawazo hasa kwa waliowajasiliamali,, mm nimekuwa mchimbaji mdogo eneo moja hapa nchini nmeanza kuchimba miaka 9 ilopita ,, kwa bahati wiki ilopita nilibahatika nikapata dhahabu ambayo imeniingizia milioni 200 na kitu,,
nilikuwa nataka kuachana na kazi ya uchimbaji maana ni ngumu sana , napenda nifanye biashara ,, na ni biashara ipi naweza anza na nayo?
Million 200 dhahabu hizo ni kilo si chini 300..

Acha masihara mkuu..
 
Endelea kufanya hiyoo biashara(commodities) ulitoipata hyo pesa,sio lazima dhahabu unaweza nunua ata copper au manganese ore in bulk na kuuza..commodities business inalipa kama ukiwa makini
 
Ukijenga nyumba ya m80 unaipangisha kwa bei gani kwa mwezi? 500,000? Fikiria mtu anawekeza kibanda cha TigoPesa mtaji haufiki 5m kwa mwezi anapata over 1m kulingana na eneo, wewe ukajenge nyumba m80 upate kodi kwa mwezi 500,000/-!
It's more safer kujenga nyumba na kuipangisha..

Tigopesa wakora wakiingia, matapeli wakikuchezea, wakala akiingia mitini unasaga meno..

By the way, unaweza kufanya vyote hivyo viwili kwa mtaji wa million 200..
 
Kwasababu unayajua madini vizuri kwanini usiwe dealer? Unanunua kwa wachimbaji wadogo halafu unawauzia wengine.
Angejua watu wanavyo pukutisha mitaji angebaki huko mana sizani kama kuna njaa sana na ukibahatisha huko unauwezo wa kufanya jambo kubwa.
 
Ukijenga nyumba ya m80 unaipangisha kwa bei gani kwa mwezi? 500,000? Fikiria mtu anawekeza kibanda cha TigoPesa mtaji haufiki 5m kwa mwezi anapata over 1m kulingana na eneo, wewe ukajenge nyumba m80 upate kodi kwa mwezi 500,000/-!
Prondo,mimi siyo mtaalamu wa mambo ya biashara lakini kwa mtaji wa milioni themanini na kuingiza laki tano kwa mwezi siyo mbaya. Ni biashara halali chache sana ambazo unaweza kupata faida ya zaidi nusu milioni kwa mwezi kwa mtaji wa milioni themanini.
 
inautapeli mwingi ndo maana naiepuka bora kuchimba kuliko kuwa dealer ni risk
Kujua tu kama wa inautapele imetosha kuifahamu tayar hakuna biashara isio na utapeli ni uwemjanja tu wa huo utapeli tenga kiasi kidogo cha pesa ndo uzungushie huna haja ya kutia yote na muhimu ufanyie maeneo hayo uliokaa kwa miaka 9
 
Prondo,mimi siyo mtaalamu wa mambo ya biashara lakini kwa mtaji wa milioni themanini na kuingiza laki tano kwa mwezi siyo mbaya. Ni biashara halali chache sana ambazo unaweza kupata faida ya zaidi nusu milioni kwa mwezi kwa mtaji wa milioni themanini.
Yaani uwekeze milioni themanini upate laki tano kwa kuwa nyumba sio biashara ni aset sawa ila ukiifanya biashara ni hasara tasilimu
 
Mfano biashara ya nguo from China, unachukua frame kariakoo kwa 6m kwa mwaka. Unaenda China unachukua mzigo wa kama 20m unakuja kuuza. Jinsi utakavyoona biashara inaenda n unavyojifunza mwisho wa siku unakuwa unaleta containers kadhaa kama Wakinga. You grow gradually....
K.koo watu wanabadilishana tu flem hali sio kama ilivyokua imebadilika sanaa hakuna wageni tena wanaokuja kununua bidhaa.

Wale waliokua wanaingiza kontena 4 kwa mwezi kipindi hichoo. basi kwa sasa akimaliza 1 ndani ya mwezi huyo anamali nzuri sana.
 
Wakati mtaani kumejaa maneno kama yako wengine mauzo yanaongeka mwezi kwa mwezi. Game ime-change only the fittest will survive. Be the best,unique....biashara ya mazoea haina nafasi sasa hivi.
 
Ukijenga nyumba ya m80 unaipangisha kwa bei gani kwa mwezi? 500,000? Fikiria mtu anawekeza kibanda cha TigoPesa mtaji haufiki 5m kwa mwezi anapata over 1m kulingana na eneo, wewe ukajenge nyumba m80 upate kodi kwa mwezi 500,000/-!
Nyumba itabaki kwa myaka mingi lakini wekezo la mda mlefu.
 
Prondo,mimi siyo mtaalamu wa mambo ya biashara lakini kwa mtaji wa milioni themanini na kuingiza laki tano kwa mwezi siyo mbaya. Ni biashara halali chache sana ambazo unaweza kupata faida ya zaidi nusu milioni kwa mwezi kwa mtaji wa milioni themanini.
Mkuu afadhali umesema wewe sio mtaalam wa biashara. Hata mimi sio mtaalam ila siwezi kuwekeza 80m nipate 500,000!
 
Huyu mleta mada anaacha kazi yake ya uchimbaji. Anataka biashara ingine ni wazi anategemea biadhara hio kula,kuvaa etc yrye na familia yake. Sasa nyumba ya kodi 500,000 atakula na kutunza familia yake? Acheni utani.
 
Mkuu afadhali umesema wewe sio mtaalam wa biashara. Hata mimi sio mtaalam ila siwezi kuwekeza 80m nipate 500,000!
Yaani kama mtu unawekeza m 80 ukapate laki tano kwa mwezi utakuwa una matatizo ya ufikiri

Ila kama unawekeza hiyo hela kama aset sawa. Au mtu ane ogopa kuharibu hela

Ila mfanya biashara hawezi kukubali kuwekeza hela hiyo kwa hiyo faida
 
Prondo,mimi siyo mtaalamu wa mambo ya biashara lakini kwa mtaji wa milioni themanini na kuingiza laki tano kwa mwezi siyo mbaya. Ni biashara halali chache sana ambazo unaweza kupata faida ya zaidi nusu milioni kwa mwezi kwa mtaji wa milioni themanini.
Ha haa jamaa huenda anapiga sana hela.
Hata ingekua laki 3 ikiwa garatii nipesa nzuri tu
 
Back
Top Bottom