Wazo la 1: Biashara ya duka.
Tafuta miji 20 michanga inayochipukia yenye uhitaji zaidi na mahitaji ya jumla ya nyumbani kama, sabuni, mafuta, n.k fungua maduka20 yenye thamani ya Tshs million 8 kila duka. Tafuta mtalaamu wa masuala ya pesa akutengenezee mfumo wa jumla wa mauzo. Yaani bidhaa zote zinakuwa kwenye system kila inapotoka bidhaa huku inajirekodi na kuongeza kiasi cha pesa. Possibly kwa mtaji wa million 8 mauzo ya siku hayatakuwa chini ya laki 1 kwa siku. So utaingiza million 2 kwa siku na kwa mwezi mmoja itakuwa 2,000,000 x 30= 60,000,000/= hapa rudisha million 50 kununua biadhaa na kulipa wafanyakazi. Baki na 10m faida ukienda kwa mwaka mmoja utakuwa umeshajua biadhara ikoje na changamoto zake kisha kama inalipa ongeza maduka mengin 10. Ukija kufikisha maduka 100 hapa bongo pamoja na hasara za kuibiwa n.k Mengi na MO watakuwa ni rafiki zako.
Wazo no 2.
Ifukie chini million 100 kwenye kilimo cha mpunga Morogoro au nyanda za juu kusini. Ukija kuvuna hii nakuhakikishia zitakuwa 200million. Maelezo zaidi kafanye survey mwenyewe.
Wazo no 3.
Iweke Forex trade na lot size ya 0.5 position mbili tu kwa mwka utapata million zingine 200. Taarifa zaidi muone memmber anaitwa
ONTARIO
Wazo namba 4.
Usiogope biashara za risk ndo zenye pesa na hakuna biashara isiyo na risk.
Nunua viwanja kwenye maeneo yanayochipukia kisha uza baada ya mwaka mmoja though faida yake si kubwa sana lakini ni biashara ambayo haina risk.
Wazo na 5.
Nikopeshe mimi million 20 tu dhamana ipo baada ya mwaka nikurudishie million ..........(sema wewe)
Kama vipi nitafute mawazo ya biashara ninayo mengi