Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

Mkuu mimi niko dar. Ni kweli kuwa kwa sasa kuwa watu wengi wanakula dona. Lakini kumbuka kuwa kama unatengeneza dona lazima uwe na oda kabisa na uwe makini na mahindi unayo nunua, mengine wanaweka dawa ku-prerve. Kwa hiyo wakati wa kutengeneza dona ni lazima uyaoshe Ni vigumu Kwa uzoefu wangu kutunza unga wa dona kwa muda mrefu.

Unavunda haraka kwa sababu mahindi wanakauka kwa kutumia joto la jua hivyo ku-control moisture content ni vigumu unless una unakausha hayo mahindi kwa njia ya kisasa zaidi. Pia swala la mizani uwe makini. Wakala wa vipimo huwa wana mizana ambayo weme-certify/recommend unaweza ukawaon wakakushauri. Kupunguza usumbufu na imani kwa wateja mimi nilinunua mzani mkubwa wa digital wenye capacity ya 100kg for about 1M. Pia kumbuka kutengeneza nembo yako.
 
Hahaha yaan changamoto kubwa mkuu naiona kwenye kupata mahindi mazuri. Nikinunua digital sihitaji kuwaona wazee wa vipimo au ni lazima pia? We una brand gani maana nilipita juzi pale makutano ya Morogoro road na samora nikaiona ila sina uzoefu na mizan sikujua ipi inafaa na ipi haifai.
 
Lazima watu wa vipimo wa-certify. Unajua wateja wengine wakifika nyumbani wanapima tena. Niliwahi pata tatizo hilo wakati natumia mizani ya rula-analogue. Inaweza kuharibu biashara yako kabisa hasa kwa wateja wadogowadogo wanaenda kuuza kwenye retail shops. Digital haiongopi. Yes nilinunua mashine along Morogoro road/Samora.
 
Safi sana Lutifya.

Hawa wanapatikana wapi mi niko temeke? Na je nikinunua lazima niwapelekee au watakuja kiwandani? Na je hii biashara inanilazima kusajiri TFDA na TBS?
 
Safi sana Lutifya.

Hawa wanapatikana wapi mi niko temeke? Na je nikinunua lazima niwapelekee au watakuja kiwandani? Na je hii biashara inanilazima kusajiri TFDA na TBS?
Biashara yeyote inayohusisha kupaki au kusafirisha chakula cha binadamu, TFDA ni lazma wahusike.
TBS sina uhakika.
 
 
Watu wameshaamka kusema ukweli tofauti na unavyofikiri. Wale elfu kumi wanatafuta mtaji na wao waweze kujiendeshea miradi yao kama huyu. wapate wapi capital unadhani?

Nikweli kwenye Kilimo kuna fulsa nyingi lkn Kwenye kilimo km huna mtaji nikujilisha Upepo juzi nilikuwa 88 Moro,na Dodoma,Nilikuta waTHAILAND wanawataka wakulima watakaoweza kulima Mahindi yale zamani yaliitwa YANGA kwaajili yakutengenezea Chakula cha mifugo, wanasema wanamahitaji makubwa ya hiyo kitu lkn km uko peke yako angalau uanzie Eka 30 vinginevyo muwe km kikundi so unaweza kuona Bila mtaji ni Shidaaaaa.
 
Wako wapi vipi unayomawasilino nao kiongozi.
 

Kaka mawasiliano unayo please
 
Biashara ya kuproces ni nzuri sana, na kinacho takiwa hapa ni kuanza na eneo uliko, anza kisaply mtaa ulipo na ukisha kamilisha mtaa wako hamia mtaa wa pili, haina maana kupeleka mbali wakati mtaani kwako hiyo product haipo.

Na pumba zile unaweza uza na zingine ukaanzisha project ya kuku au kitinoto, by product utatumia kulishia kuku wako.
 
Watakuwa si wanaenda kula? Haya mahindi ndo yenye virutubisho vingi sana kuliko haya meupe na ukiweza kuwa na unga wake wa Dona ukawa unatumia inakuwa vizuri sana. Hata kwenye kutengeneza unga wa uji inashauliwa kutumia haya mahindi.
 
Ila kutokana na ushindani ni lazima uwe na ubunifu, ni lazima uje kivingine kabisa.
 

Habari mwamaJF; dolevaby. Naomba kama ulifanikiwa kupata maelezo ya kutosha ya hao jamaa (hasahasa mawasiliano) unijuze niwatafute. Tafadhali sana.
 
Watakuwa si wanaenda kula? Haya mahindi ndo yenye virutubisho vingi sana kuliko haya meupe na ukiweza kuwa na unga wake wa Dona ukawa unatumia inakuwa vizuri sana. Hata kwenye kutengeneza unga wa uji inashauliwa kutumia haya mahindi.

Yaah! Wanasema huu UNGA watu waliudharau sababu ulikuja kipindi cha Njaa lkn kwa maelezo niliyopewa wanasema unavirutubisho vya kutosha kuliko mahindi Meupe.
 
kaka mawasiliano unayo please

Chek na huyu ndg anaitwa Christopher 0717 000 772 na Ndg Rafael 0718 467 878 KAMPUNI yao inaitwa CP Offisi yao kwa hapa DAR iko MLIMANI CITY kwa anaetaka Maelezo zaidi wanasema kwa mtu mmoja mpaka sasa walieingia nae Mkataba ni MKUU wa WILAYA ya MVOMELO yy analima Eka 60 waliobaki wote ni vikundi tena ni MKOA mmoja tu TANGA watu bado hawajachangamkia hiyo Fulsa
 
Khs wale waTHAILAND wanasema unaweza kuchukua Mbegu kwao baada ya kuvuna unarudisha kitakachobaki unawauzia na kwa Bei ya sasa wananunua Tsh 530 kwa KG namna ya kupanda 50x25 kila shimo.una mbegu moja moja na 75x50 unaweka mbegu mbili wastan Gunia 20 kwa Eka hayo ni miongoni mwa niliyoshuhudia huko 88 Samahani kwa muanzisha Uzi manake km tumehama kwenye Lengo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…