Habari mwamaJF; dolevaby. Naomba kama ulifanikiwa kupata maelezo ya kutosha ya hao jamaa (hasahasa mawasiliano) unijuze niwatafute. Tafadhali sana.
Yaah...wanasema huu UNGA watu waliudharau sababu ulikuja kipindi cha Njaa lkn kwa maelezo niliyopewa wanasema unavirutubisho vya kutosha kuliko mahindi Meupe...
Mawasiliano nimeweka hapo post ya Nyuma chek nao km uko DAR nenda pale MLIMANI CITY Ofis yao inaitwa CP 0717 000 772 na 0718 467 878 Kila la heri MKUU
Hii kitu nilikuwa naiwaza ila bado sijafanyia maamuzi ya kufanya packing,japo nimenunua mpunga gunia 100 hivi za debe 9@1.Je unafaham biashara hii vema.Rice packaging nayo inawezekana haina tofauti na sembe hata kidogo cha muhimu ni kupata mpunga mzuri na kuukoboa vizuri ili usiwe na chenga nyingi (machine factor) kama ujuavyo bei ya mchele ni maelewano na hupangwa kutokana na kunukia, aina na muonekano wake baada ya kukoboa.
Mchele utapata faida zaidi iwapo utaweka machine ya kukoboa mahali ambapo ni karibu na mpunga unapolimwa c'se kusafirisha mpunga kutoka mbeya/ifakara/shinyanga to dar kuja kuukoboa ni hasara.. c'se unapokoboa gunia moja la mpunga unapata mchele kidogo sana, pumba huwa ni nyingi kuliko mchele na pumba za mpunga si chakula pendwa kwa wanyama sana utaishia kuutupa au kuugawa kwa wafugaji wa kuku (pumba zake ni malazi ya kuu)
Hujambo,kuna mrejesho wowote ambao unaweza kutueleza, mafanikio,changamoto ulizokutana nazo na unazoendelea kupambana nazo.Hellow wa jf na wazo la kuanzisha biashara ya kusaga unga wa sembe na ku pack kwa ajil ya kuuza, jaman naomben mawazo yenu .
kuna kampuni ya ipo mbagala kazi yao ni kutengeneza mifuko ya kila aina naweza kuelekeza 0685 31 2326
asante mkuu nipo na dar na nimetafuta location maeneo ya kimara kwa ajil ya kufunga mashine but sijapata kampun ya uhakika ya kunitengenezea mifuko kwa ajil ya ku pack.
hii kitu nilikuwa naiwaza ila bado sijafanyia maamuzi ya kufanya packing,japo nimenunua mpunga gunia 100 hivi za debe 9@1.je unafaham biashara hii vema
Duu! mpunga hausagwi mamaa,tunakoboa..hapo umeshafell tayari..mambo vipi lakiniWaonaje hizo debe 100 za mpunga ukazisaga kisha tuungane kufanya hiyo biashara?
watafute Hill Packaging .... huyu jamaa mmiliki anaitwa Hillary ni mjasiriamali mzuri sana .... anakiwanda cha kutengeneza viroba kipo mapinga Bagamoyo mwanzo kabisa karibu na bunju
Duu! mpunga hausagwi mamaa,tunakoboa..hapo umeshafell tayari..mambo vipi lakini
Wadau. Nimeisha anza mchakato wa hiyo kitu kwa maana ya jengo ambayo mi nimeiita phase one sasa ndo najipanga kuezeka.
Phase two ni kununua machines ambazo ni full set kusaga na kukoboa pamoja na mizani mikubwa na midogo na packaging materials bila kusahau mahindi ambayo mdo mtaji.
Phase three ni kuanza kazi.
Naomba muongozo au ushauri kwa ambaye either anafanya au anauzoefu na hii biashara japo kwa reaserch ndogo niliyofanya inalipa na nimeamua kuanza at a medium level scale walau nipate market share kias fulan lakin naona changamoto ni nyingi mf kupata mahindi fake, unga au mahindi kuharibika ama kuoza, n.k nk.
Hizo picha ndo mjengo wa kiwanda na bahati nzuri nina eneo kubwa hapa kwangu so nimeona bora nijenge hapa kupunguza gharama na iwe rahisi kusimamia.
Ntashukuru kwa ushauri[/QUOT
Mkuu tunaomba mrejesho tafadhali