Biashara ya kujiuza, Dada poa, Kaka poa na Ma-sugar Mamy: Nini kifanyike kupambana nayo?

Biashara ya kujiuza, Dada poa, Kaka poa na Ma-sugar Mamy: Nini kifanyike kupambana nayo?

Nikiwa ni kijana mdogo nasoma kijijini kwetu nilikuwa nikisikia habari kwamba mjini kuna wanawake wanajiuza, sikuweza kuelewa kulingana na mazingira niliyokuwa nikiishi, nilitamani siku moja niwaone nipate uhakika na kwa mara ya kwanza nimefika mjini ilikuwa jiji la mwanza nilimuomba mwenyeji wangu anipeleke wanapopatikana kiujumla nilipata jambo la kujifunza ambalo mpaka sasa napata kitu cha kukuandikia wewe mdau wa Jamii forum.

Biashara hii imeshamiri sana kwa siku za hivi karibuni, Je umewai kujiuliza kwa nini, serikali inapiga marufuku sana Je watu wanaofanua hawaogopi serikali, nikagundua pia serikali yenyewe kuna watu ambao ni wadau wa biashara hizi kwani wananunua hawa dada poa au pia wao wanajiuza.

Sababu kubwa za hii biashara ni ugumu wa maisha unaowakumba wanawake na mabinti wengi wa kitanzania ingwa kuna watu wanaifanya hii biashara kama burudani kwa sababu hakuna jipya yaliwai kufanyika tangu kipindi cha sodoma na gomora kwa wale wenzangu na mimi wasomi wa biblia.

Asilimia kubwa ya wanaofanya hii biashara ni wanawake wenye mtoto mmoja au zaidi na hawana mme, hii inatoa tafsiri kwamba ugumu wa maisha ndo chanzo nilifanya utafiti katika jiji la Dodoma ambapo nilikutana na wanawake wanaofanya hii biashara zaidi ya 20 na wote walikuwa na mtoto na walisema wanafanya hivi ili mtoto wake aishi maisha mazuri. Kitu nilichopenda kutoka kwao ni kwamba hawakai na watoto wao kama ni mzawa wa Dar es salaam utakuta bishara ya kujiuza anaifanyia dodoma pesa anayopata anatuma kwa familia yake.

Katika asilimia izo kuna wanachuo pamoja na wahitimu wa vyuo mbali mbali, kwa mkoa wa Dodoma kuna vyuo vingi ambavyo vinatoa idadi kubwa ya hawa watu wanaojiuza hii ni kwa sababu ya ugumu wa maisha uliopo vyuoni pesa anayopata mtoto wa kike haiendani na uhitaji wake.

NINI KIFANYIKE?
Je, serikali inaweza kupambana kuondoa hii biashara ili kutunza taswira ya nchi jibu ni hapana.
Ni kweli kwamba dini na siasa vinategemeana lakini si kitu kimoja, nafikiri kisiasa hii biashara sio mbaya lakini kidini ni mbaya kwa sababu ni kinyume na maadili.

Hivi kwa nini serikali isiache hii biashara ifanyike kwa uhuru na viongozi wa dini husika wafanye kwa nafasi yao, kwa sababu uhalisia ni kwamba mtaani hali ni mbaya, kikubwa ni yatengenezwe mazingira sahii na sera nzuri ili bishara hii ifanyike salama ikiwa ni pamoja na kuzuia maambukizi ya magonjwa ya ngono kwa kasi zaidi.

Madhara ya hii biashara ni mengi kiafya na kimaadili lakini sera nzuri inaweza kuwa suluisho pamoja na viongozi wa dini kusimama katika zamu yao, inaweza kuondolewa bila ata kutumia nguvu ya dora.

Karibuni kwa mjadala kwa maswali na maoni pia
Hii biashara ilikuwepo hata kabla hajaja masihi yaani zile enzi za Babylon,Roman , ottoman empire zilikuwepo.
Hakuna jipya duniani wewe haulewi
 
Chanzo cha hio biashara ni sisi wanaume wenyewe siku wateja wakikosekana watoa huduma nao watafunga makampuni yao
 
Hivi kwanini mnapenda kuwaonea akinamama. Hii biashara kuna upande unataka pesa na kuna upande unataka utamu na upo tayari kutoa pesa ili utamu upatikane.

Wateja wengi ni wanaume tuliooa. Hii ni huwa ni kama suspension ya gari, ndani hupati kitu na hapo hapo abdallah anataka kuachia. Punyeto inagoma maana abdallah anataka kuachia ndani ya mwili wa mtu si katika mikono.

Suluhisho la hii kitu ni ngumu maana wahanga wa kunyumba wasipopata hao machangu utawafunga miaka 30 wote. Kwa upande wangu hao machangu wanafanya kazi ya kutukuka maana wanadumisha ndoa nyingi hasa za hao wasio na kipato cha kuwatunza akina Unique Flower wanaotoa mapovu kwa vile hakuna wanaowatongoza PM
Bwana ni kweli kina mama majumbani ndio chanzo cha madada poa kupata wateja kama serikali ikiwafungia basi ifungie na akina amalishe maana mama akizingua unaenda kwa mama lishe unashona Fasta vivyo hivyo kwa dada poa wa ndani akizingua unazunguka mtaa Fasta mbona trafiki anakukamata ukitembea bila gurudumu la akiba?
 
Hiyo biashara ni kongwe zaidi, hata huyo Maria Magdalena ambaye Bible inasema alikuwa wa kwanza kumuona Yesu baada ya kufufuka alikuwa Changudoa kabla ya kukutana na Yesu. Na conspiracy theorists wanasema Yesu alikuwa anamtafuna na walifunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja
Hahahahahaha
 
Hivi kwanini mnapenda kuwaonea akinamama. Hii biashara kuna upande unataka pesa na kuna upande unataka utamu na upo tayari kutoa pesa ili utamu upatikane.

Wateja wengi ni wanaume tuliooa. Hii ni huwa ni kama suspension ya gari, ndani hupati kitu na hapo hapo abdallah anataka kuachia. Punyeto inagoma maana abdallah anataka kuachia ndani ya mwili wa mtu si katika mikono.

Suluhisho la hii kitu ni ngumu maana wahanga wa kunyumba wasipopata hao machangu utawafunga miaka 30 wote. Kwa upande wangu hao machangu wanafanya kazi ya kutukuka maana wanadumisha ndoa nyingi hasa za hao wasio na kipato cha kuwatunza akina Unique Flower wanaotoa mapovu kwa vile hakuna wanaowatongoza PM

Pia wanasaidia mno madomo zege. Ni msaada mkubwa sana. Wasiache!
 
Mi mwenyewe nishasikia hizi story, hata ile picha ta last supper kwamba yesu alikua na wanafunzi wake eti pale mmoja alikuwepo dem wake ๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚
Tutachomwa moto kwakweli!!!!
Sasa mmoja alikua demu wake kivipi wakati wanafunzi wa yesu wote walikua wanaume
 
Hiyo biashara ni kongwe zaidi, hata huyo Maria Magdalena ambaye Bible inasema alikuwa wa kwanza kumuona Yesu baada ya kufufuka alikuwa Changudoa kabla ya kukutana na Yesu. Na conspiracy theorists wanasema Yesu alikuwa anamtafuna na walifunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja
Una uhakika na hizo conspiracy theory zako?
 
Hiyo biashara ni kongwe zaidi, hata huyo Maria Magdalena ambaye Bible inasema alikuwa wa kwanza kumuona Yesu baada ya kufufuka alikuwa Changudoa kabla ya kukutana na Yesu. Na conspiracy theorists wanasema Yesu alikuwa anamtafuna na walifunga ndoa na kuzaa mtoto mmoja
acha upuuzi aisee, hakuna hicho kitu kwenye historia..
 
frankly speaking hii biashara imeshamiri sana siku hizi...na jambo la kushangaza inafanyika wazi wazi bila kificho...

nadhani ni vyema serikali ikahalalisha ili ifanyike kwa namna inayofaa kuliko inavyofanyika sasa hivi...

wadau wa dini ni jukumu lao kuwajengea misingi bora waamini wao na kuzidisha elimu na kukazia maadili....

serikali haina dini...ila watawala wanadini...kila mtu atumie akili yake
 
ni kweli kabisa kwamba asilimia kubwa ya wanaojiuza hawafanyi kwa kupenda ila wanabanwa na ugumu kwelikweli wa maisha. wengi wao walitoka vijijini kuhadiwa kwamba mjini watapata kazi, kumbe walipofika kazi ndo hiyo na hakuna nauli ya kurudi kijijini achilia mbali pesa kwa ajili ya chakula na malazi, wengine walipofika mjini walipewa kazi za ndani, wakaanza kufanya kwa uaminifu kabisa, maskini baba mwenyenyumba kakawakia tamaa kakabaka, au kukatongoza katoto ka watu, mama mwenye nyumba kashtukia mahusiano hayo haramu pengine hata kwa kuambiwa na kabinti kenyewe, kisirani kimemjaa kakafukuza kama mbwa kwa kisingizio cha kulinda ndoa yake , hata kama ndoa ,yenyewe ni ya mkeka, ili mradi tu kwamba yeye ndo ameshika kwenye mpini. Kabinti ka watu kanafukuzwa, hakapewi hata nauli , kakianza kurandaranda mitaani pa kwenda huenda kakakutana na wasamaria wema kwa ngozi ya kondoo tu ,kumbe ndani ni wafilist, hawa kama .ni wadada watakashirikisha kazi hiyo na ni ngumu kwake kukwepa.

Hata hivo hatutaki kuhalalisha biashara hiyo kwa sababu za ustawi wa jamii. Hiyo ni kazi yenye addiction sawa na madawa ya kulevya.
Kwani unawaonaje hawa wadada kauli zao! Hawana ustaarabu hata kidogo, vinywa vyao vinazungumza machafu muda wote ni hatari sana kwa jamii inayo interact nao ikizingatiwa kwamba makazi yao ni yaleyale wanayoishi raia wengine.
Kadhalika ile asilimia ndogo ya wasiofanya biashara hii kwa shida tutawafungulia uwanja wa kuzidi kuwavuruga na kuwachafua mabinti zetu ambao wako exposed na mazingira hayo.

BINAFSI ninachoona chafaa kufanyika ni, tuwatake wazazi waliopo vijijini kutowaruhusu watoto wao kuja mjini pasipo kuwa na uhakika na aina ya kazi wanazokuja kufanya, mfano wazazi wengi wamedanganywa na binti zao aina ya kazi halali wanazofanya na wamezibariki, kumbe uongo mtupu, PIA SERIKALI iangalie namna ya kuwezesha maisha ya mabinti pamoja na vijana ili wasiingie kwenye changamoto za shida zinazokithiri kiasi cha kujihalalishia kazi haramu.
KATIBA MPYA, ndiyo pekee itakayoikurupusha serikali iweze kutimiza wajibu wake ipasavyo.
 
Duuuuh! Kweli Elimu haina mwisho, tupe shule walau kidogo juu ya hayo mahusiano baina ya Yesu na Maria Magdalena
Kuna hadi Injili ya Maria Magdalena sema hakina "Bashiru" waliichomoa kwenye bible, hata kanisa aliachiwa huyu mama na sio Petro...damn it!
 
Back
Top Bottom