Biashara ya Kununua na Kuuza Mazao (nafaka): Jifunze Mbinu za Kuanzisha na Kusimamia


Mimi nilifikiria wa shinyanga lakini mchele nije kuuza reja rejana jumla. Na kwa nini wa shinyanga au Mwanza hauna soko Dar. Unatofautiana vipi na mwingine?

Natanguliza shukrani.
 

Asante kwa majibu ya kina. Barikiwa sana

Mimi nataka kununua lakini naona mpunga ni risk sana sababu nahitaji mchele ulionyooka grade 1na vile siendi kununua mwenyewe natuma mtu basi ni bora mchele kuliko mpunga.

Pia naomba ushauri,mchele grade 1 wenye kupendwa na watu unaonukia na wenye ladha ni wa mkoa upo Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Morogoro? Wapi nitapata mzuri zaidi?
 
Mkuu napenda kujua yafuatayo:

1: Msimu wa mavuno ni upi?
2: Kama nataka kuchukulia mchele kati ya Shinyanga au Mwanza halafu nisafirishe Burundi au Rwanda,itanigharimu kiasi gani kwa kuanzia na tani mbili?
3: Kuhusu vibali vya kutoa mchele hapa na kupeleka kwenye nchi nilizotaja hapo juu vikoje?
4: Kwa wastani gunia inafika kiasi gani kwa kipindi cha mavuno na soko lake kwenye nchi hizo likoje?

Naonba yeyote mwenye ufahamu wa hayo anisaidie kunijibu.
 
Hapo mpka ufanye kwanza research kwa watu wanao Fanya biashara za mikoan but mm huwa nauzia hapahapa na inanilipa, japo kuwa mda mwingi nafanya shughuli za kiserikali.
 
Nitaku-PM mkuu naona umeuliuza confidential question! Hahahaaaaaah, nimefurahi sana mkuu kwa swali lako!
 
Nitajibu baadae mkuu usiwaze
 
Naweza wasiliana na wewe mkuu maana na mimi nataka nijikite huko sasa.
 

1. Msimu wa mavuno ni kipindi ambacho wakulima wanavuna mpunga toka shambani na kupeleka majumbani mwao au kwenye maghala yao. Ni kipindi ambacho mpunga ni mwingi sana pia bei yake mara nyingi huwa ya chini sana- Demand and Supply principles zinaapply.

Misimu hii hutofautiana miongoni mwa mikoa inayozalisha mpunga kwa wingi kwa mfano leo hii mpunga umeshaisha mashambani huko Shinyanga wakati Morogoro wakulima bado wanatoa mashambani.

2. Tani mbili ni chache sana kupeleka Rwanda ama Burundi, itakupa hasara tu kwa sababu gari za kwenda huko toka Shinyanga ni sawa na hamna kwani zinazoenda huko ni zile semi kubwa ambazo kuibebesha tani mbili tu hadi Kigali hakuna mwenye gari atakaekubali kuacha kubeba saruji, nondo ama makontena ya shehena ya kemikali toka bandarini ukilinganisha na kuvizia gari hizo wakati zikirudi toka Kigali na kuzipatia tani moja kwa 45,000/- kwenda Dar kwani zinakuwa tupu dreva anabeba chochote hata kama ni mkaa au kuku ili tu dreva apate kidogo.
Hivyo kwa tani chini ya 100 ni vizuri kupigia Dar, Arusha na inalipa tu tena sana.

3. Kiufupi vibali vinasumbua isipokuwa kwa wale wateule kwani hakuchelewi kutolewa zuio la kuuza nafaka nje ya nchi japo wateule huendelea. Sijui labda safari hii mambo yatakuwa laini au magumu zaidi katika kuuza nje ya nchi muda utaingea kufukia mwezi wa 9/10.

4. Bei hutegemeana na mkoa husika kwa mfano Shinyanga (45,000 hadi 55,000/-) wakati wa mavino na vile 35,000/- hadi 40,000/- Mpanda, n.k.

Kwa upande wa Rwanda na Kenya wakati wote bei inakuwa juu ukilinganisha na hapa Tz kwa mfano kama Dar unanunua kwa Tsh. 22,000/- Kigali inakuwa Tsh. 3,000/- kwa kilo kutegemea na muda (miezi).
 
Habari,

Kwa anayetaka tufanye biashara ya mchele, nipo kahama na nina connection na watu wa malori yanayoenda dar, if ur interested lets join hands.
 

Nipo Dar natamani sana kufanya hii Biashara naomba ila sijui lolote mtaji ninao naomba unisaidie mkuu asante nina uwezo wa kuanza na tani 5 mpaka 10 itategemea na bei ya manunuzi.
 
Hata siku 1 usidanganyike na mafanikio ya akina dada, wanambinu na mitaji mingi ambayo wewe huwezi, ukivutiwa na hao umepotea mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…