Nyendeke
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 1,552
- 2,849
Kiongozi huo Mzigo nauza wote kwa jumla, ila kama utahitaji kuanzia kilo 100 pia tunafanya biashara!unauza kuanzia kiasi gani?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kiongozi huo Mzigo nauza wote kwa jumla, ila kama utahitaji kuanzia kilo 100 pia tunafanya biashara!unauza kuanzia kiasi gani?
Biashara ya mchele ukitaka inaweza fanyika kwa watu wa aina 5.
1. Unakuwa na mashamba yako au yakukodi. Ukalima.ukakoboa.ukaingiza sokoni mwenyewe. Hao ni wachache na wana maeneo makubwa.
2. Wananunua mpunga kwa jumla na wana mashine za kukoboa. Wanahifadhi bei zikipanda wanakoboa na kuingiza mchele sokoni.
3. Wananunua mpunga mashambani na kuhifadhi kwenye magodown/mashine huko maeneo kama ubaruku nk. Bei zikiimarika wanakoboa na kuingiza sokoni ama kwa kuleta wao au kuuzia huko mashine.
4. Wanaenda nunua mchele huko mashine unaokobolewa na kusafirisha kuleta sokoni kama wafanyabiashara wa jumla.
5. Unanunua huku mjini kwa wafanyabiashara wa jumla nawe unauza kwa wenzio. Jumla au rejareja.
We unaulizia na.ngapi upate undani wake na umelenga mbeya? Morogoro? Mchele wa mwanza na shinyanga una soko rwanda na burundi dar haulipi.
Kadri ya jinsi nilivyoelewa maswali yako juu:
Ili kujua mpunga kama ni mzuri huwa tunachukua sample na kuumenya na kisha kutathmini ubora wake-mzuri hutoa punje zilizonyooka na nyeupe wakati mbaya hutoa mpunje zilizovunjikavunjika, ama nyekundu badala ya nyeupe.
Pia ubora wa punje/mchele huweza tegemeana na mashine uliyokobolea na technician anaeseti mashine-kuna mashine zenye wataalam wa kuseti mashine kulingana na mpunga unaokobolewa kwa wakati husika na mchele wote utokao kwenye mashine hizo ni "super" au ulionyooka tu.
-Ubora wa mchele hutathmini faida utakayopiga wakati wa kuuza mchele huo.
Kwa mtaji mkubwa wa kuweza kununua tani hata 2 za mchele ni vyema ukauza mchele pale bei ya mchele inapokuwa juu zaidi sokoni wakati mashineni ukiuzwa kwa bei ya chini. Kwa mfano kama mashineni unauzwa kwa Tsh.800 kwa kilo na kuuzwa kwa Tsh. 1400 sokoni na wewe ukanunua tani 2 kwa Tsh. 1,600,000/- na kuuza kwa Tsh. 2,800,000/- wakati gharama ya usafiri ni kama 90,000/- kama utakuwa umetoa mzigo Shinyanga kuja Dar kwa mfano, hapo unakuwa umetengeneza faida ya 700,000/- kwa safari moja.
-Faida itaongezeka kutegemeana na safari unazofanya kwa wiki yaani safari moja, mbili au tatu; na hii inaonesha atakaepiga faida zaidi ni yule anaenunua mchele na kusafirisha moja kwa moja kuliko anaechukua mpunga na kupanga mstari mashineni ili akoboe ambapo anaweza koboa tani chache tu siku.
Kuna wakati pia kununua mpunga na kuuhifadhi kwa ajili ya kukoboa na kuuza baadae kunalipa sana, kwa mfano ikiwa leo gunia linauzwa kwa Tsh. 55,000/- na ukanunua na kulihifadhi hadi mwezi wa 12 (2016) au kwanza mwakani (2017) ambapo bei inaweza kuwa 85,000/- hadi 100,000/- kuna uwezokano wa kupiga faida isiyopungua 25,000/- kwa gunia kama utauza mpunga kama mpunga; ukikoboa na kuuza mchele unapiga zaidi ya hiyo (25,000/-)
Kwa ujumla ni vyema kipiga zote (mchele na mpunga) kulingana na kile kinachotoa faida zaidi kwa msimu husika, eneo unalofanyia biashara kama vyote vinapatikana kama mpunga haupatikana usione tabu kwenda maeneo ama mkoa wanakolima na nununua kisha hifadhi au koboa-ukiwa mfanyabiashara lazima uzungukie maeneo ya interest yako na utajua mikoa mingi na hata vijiji vingi nchini na umbali kutoka mkoa mmoja kwenda mwingine hususani ukishakuwa na usafiri wako.
Njoo Sumbawanga wadau tupo na mm siyo dalali utapata mzigo
Mkuu napenda kujua yafuatayo:Mkuu ni vyema kweli kujifunza hata mimi hapa najifunza kutoka kwa walionitangulia na kunishawishi niingie huku kwa kweli kuna watu wako juu kiasi kwamba wao mchele wao ni wa kimataifa simu wanazopokea ili wapeleke mzigo ni kutoka Rwanda, Kenya na wanapeleka kweli ila nasi ndo tunawapatia mzigo na tunapata faida ya kutosha.
Kizuri zaidi ni kupiga zote mchele mpunga vyote nunua kama una nafasi na una sehem nzur ya kuhifadhi kwani kuna wakati mpunga unakuwa chini sana kati ya 35 000/- na 55,000/- tu katika mikoa ya Katavi na shinyanga respectively lakini baada ya muda fulani unauza kwa 85000/- hadi 100,000/ - na ukikoboa inakuw zaidi ya hapo.
Hapa mwenzako ni kuzunguka tu mikoani kama mtalii wa ndani ila watu wanakusanya punga na hata shambani naingia.
Hakuna kitu kitamu kama hii game mkuu vigari vya M20 kwako itkuwa kawaida tu hadi natamani serikali iache amsha amsha inayofanya kwa vijana kuhimiza wajiajiri-waachwe waendelee kusubiri ajira za kuagizwa maana wao waziona hizi kazi ni kizamani. Kusema kweli namuona mbunge mmoja yuko kwenye kilimo na anapiga gunia 5, 000 na anapeleka sijui nje na ana trecta zake kwa kweli hata wananchi wakimpiga chini ubunge hana njaa kabisa.
Nitaku-PM mkuu naona umeuliuza confidential question! Hahahaaaaaah, nimefurahi sana mkuu kwa swali lako!Asante kwa majibu ya kina..Barikiwa sana
Mimi nataka kununua lakini naona mpunga ni risk sana sababu nahitaji mchele ulionyooka grade 1..na vile siendi kununua mwenyewe natuma mtu basi ni bora mchele kuliko mpunga.
Pia naomba ushauri,mchele grade 1 wenye kupendwa na watu unaonukia na wenye ladha ni wa mkoa up? Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Morogoro? Wapi nitapata mzuri zaidi
Nitajibu baadae mkuu usiwazeMkuu napenda kujua yafuatayo:
1: Msimu wa mavuno ni upi?
2: Kama nataka kuchukulia mchele kati ya Shinyanga au Mwanza halafu nisafirishe Burundi au Rwanda,itanigharimu kiasi gani kwa kuanzia na tani mbili?
3: Kuhusu vibali vya kutoa mchele hapa na kupeleka kwenye nchi nilizotaja hapo juu vikoje?
4: Kwa wastani gunia inafika kiasi gani kwa kipindi cha mavuno na soko lake kwenye nchi hizo likoje?
Naonba yeyote mwenye ufahamu wa hayo anisaidie kunijibu.
Naweza wasiliana na wewe mkuu maana na mimi nataka nijikite huko sasa.Okay, kama utakuwa poa biashara iko poa sana tena sana hususan kama utakuwa na uwezo wa kufuata au agiza mzigo mkubwa toka Shinyanga, Mbeya au Morogoro au Dodoma. Pia kama uko vizuri zaidi unaweza chukulia hapa mjini (Dar) na kuuza popote unapoona inafaa hata nje ya nchi kama kibali kinaruhusu.
Biashara hii iko poa huwezi jutia japokuwa mwaka huu kidogo kodi zinasumbua kwa mfano Shinyanga vijijini kodi imekuwa kubwa sana (imepanda toka 500 hadi 2000) ndani ya wiki hii halimashauri ilipochukua jukumu la kukusanya kodi yenyewe badala ya mudhabuni kitu ambacho kitapandisha bei ya mchele maradufu na kama itapanda zaidi itapunguza faida kwa mfanyabiashara ya mchele hususani yule mwenye kununua na kuuza mchele badala ya mpunga toka kwa mzalishaji.
Wala usijali mkuu tunawasiliana tu, napatikana muda wote.Naweza wasiliana na wewe mkuu maana na mimi nataka nijikite huko sasa.
MI nipo Dom Nina guns Mia 250 karibunj
Elewa topic !Kama unataka biashara ya mchele, una uwezo wa kuchukua tani ngapi kwa wakati mmoja?
Mkuu napenda kujua yafuatayo:
1: Msimu wa mavuno ni upi?
2: Kama nataka kuchukulia mchele kati ya Shinyanga au Mwanza halafu nisafirishe Burundi au Rwanda,itanigharimu kiasi gani kwa kuanzia na tani mbili?
3: Kuhusu vibali vya kutoa mchele hapa na kupeleka kwenye nchi nilizotaja hapo juu vikoje?
4: Kwa wastani gunia inafika kiasi gani kwa kipindi cha mavuno na soko lake kwenye nchi hizo likoje?
Naonba yeyote mwenye ufahamu wa hayo anisaidie kunijibu.
Hi mdau pls ukikamilisha utafiti naomba unishirikishe nipo interested sana na hii business asanteNiko katika utafiti mkuu
Okay, kama utakuwa poa biashara iko poa sana tena sana hususan kama utakuwa na uwezo wa kufuata au agiza mzigo mkubwa toka Shinyanga, Mbeya au Morogoro au Dodoma. Pia kama uko vizuri zaidi unaweza chukulia hapa mjini (Dar) na kuuza popote unapoona inafaa hata nje ya nchi kama kibali kinaruhusu.
Biashara hii iko poa huwezi jutia japokuwa mwaka huu kidogo kodi zinasumbua kwa mfano Shinyanga vijijini kodi imekuwa kubwa sana (imepanda toka 500 hadi 2000) ndani ya wiki hii halimashauri ilipochukua jukumu la kukusanya kodi yenyewe badala ya mudhabuni kitu ambacho kitapandisha bei ya mchele maradufu na kama itapanda zaidi itapunguza faida kwa mfanyabiashara ya mchele hususani yule mwenye kununua na kuuza mchele badala ya mpunga toka kwa mzalishaji.
sorry ratiba zilikuwa zimebana hata simu sikuweza shika toka nilipokuambia nitakucheki baadae-kesho nitakucheki maana nitakuwa sina kazi sana0656960240 naomba japo unitumie tu massage nitakupigia.
Hata siku 1 usidanganyike na mafanikio ya akina dada, wanambinu na mitaji mingi ambayo wewe huwezi, ukivutiwa na hao umepotea mkuu.Nina dada yangu alifeli form 2 mara mbili akaamua kuacha shule akawa anashinda maporini kununulia watu mipunga anapata faida kidogo sasa may nilienda likizo home yaani huyo dadaangu anahela za kumtosha na kashajenga nyumba mm msomi na degree yangu na cpa ila hela alizonazo huyo dadaangu smtyms naona kuajiliwa sio kabisa.
Nitafte boss nitakusaidia Mimi miradi yangu mjiniWadau nataka kujua kuhusu biashara ya mchele. Masoko yako vp .. Na upatikanaji wake. Na mtaji wake. Mwenye ujuzi anisaidie