Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Asante mkuu kwa mawazo yako hakika yamenipa mwanga zaidi wa kuongeza mapato, hasa kuanza kuuza vinywaji na mahala pa VIP.

Thanks[emoji120]
 
Mkuu sijaona jambo muhimu kuliko yote. Unachaji kiasi gani, unategemea kupata watu kiasi gani na watu wana uwezo wa kutoa kiasi gani as well as competition karibu yako kuna wangapi wanafanya unayofanya wanachaji ngapi na huduma yao ipo vipi.

Unless otherwise faida ya kwenye makaratasi itabaki kwenye makaratasi while practically iwe kilio.
 
Fata ushauri huu.nipo kwenye game msimu wa tatu huu ila hakuna faida kubwa labda icheze simba Vs yanga kila weekend
huko vijijini EPL hakuna wadau wengi wanachagua game zao ..hicho kingilio cha 500 utakuwa unacheza tu
 
Nyongeza, angalia wenzio wana vitu gani then wewe boresha uwe zaidi yao.

Jitahidi mafuta yawemo muda wote kwenye jenereta kama itatokea umeme kukatika unawasha haraka .

kabla ya mechi hakika jenereta linakuwa nje tayari ili umeme ukikatika unawasha chap kwa haraka.

usiweke viti vya plastic utakula hasara kubwa sana.

Mkuu usisahu kitambulisho cha mjasilimali kama uwekezaji wako hauzidi 4M.

NB: kwa Tv moja huwezi kufanikiwa, chukulia kwa mfano
15:00 Nyumbu vs Arsenal
15:00 Chelsea vs Spurs
utaweka ipi na utaacha ipi?
 
Kitambulisho muhimu nalifahamu hilo, thanks kwa kunikumbusha pia.

Kuhusu TV ndugu ntaanza na moja mbeleni ntaongeza nyingine kadiri ya mapato yatakavyo kuwa.

Asante Tena.
 
DSTV ni 99,000 mkuu. Mimi staff ingawa nipo ZANZIBAR. Kisha wewe upo wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…