Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu biashara hii inalipa sana cha msingi sehemu iwe na mkusanyiko wa watu, nunua dstv dish na decoder yake na unakuwa unalipia kila mwezi kama tsh.80000/-
Pia tafuta wanachama wa kudumu wanakuwa wanalipa tsh.10000/- kwa mwezi, wakiwa 50 sawa na tsh.500000/- achilia mbali wale wa rejareja watatoa 500/- au 1000/- kila mechi.
hii 80000 haitoshi kama kweli unataka kufanya biashara. Unahitaji tsh 130000 hivi kwa mwezi ili kupata premium bouquet. Aidha decoder 1 huenda ickutoshe, unaweza kutafuta ya pili ambayo ikiunganishwa na ya kwanza itakufanya upate chnl 2 kwa wakati m1. Itakugharimu tsh 150000.
Wadau nashukuru kwa maon yenu nakaribisha mwenye maoni pamoja na ushauri kuhusu aina ya projector na ubora wake ninayoweza kutumia kwa shughul hii
Kwa kweli hapa sina utaalamu. Lakini mambo ya free to air. yaani neno free, neno promotion neno lipia upate bure ni maneno sitakagi wala kuyasikia kwa sababu ni uzushi wa kijinga. Na wala usiwasikilize wajinga wa startimes au ting au wajinga wowote eti wataonyesha mpira wa majuu. Ni upuuzi mtupu. Jipige weka dstv simamia biashara yako hii waweza toka.
Kuna kitu nasikia sijui Arab sat sijui nini nasikia hii kitu ni nzuri na cheap pia. Ila gharama za mwanzo za kufungiwa ni za juu sana.
Unalipa kama laki tisa, wanakufungia upuuzi woooote halafu baada ya hapo kila mwaka, narudia tena kila mwaka unakua unalipa kama dolla 40 na unalipiA KWENYE MTANDAO hiyo pesa.
Ila hii kitu nimesikia tu, kuna ndugu yangu anajishughulisha na dili hizi A-town, ila kokote anafunga. Mimi hii huduma siiitumii
Mimi ntumia tu dstv kwa matumizi yangu binafsi
yhanx
Wapo nadhani hata ukiingia kupatana au hata humu kuna baadhi ya matangazo yao shida inadumu kwa muda gani?mimi ninatumia star times. Hao wanaoweka channel za mpira wako wapi waniwekee?