Moja kati ya michezo pendwa sana kwa vijana na hata wazee na watoto kwa ujumla ni mchezo wa miguu, mpira (Football). Ligi nyingi sana zimeanza na zinatarajiwa kuanza ndani ya mwezi huu, huku tayari ligi pendwa ya EPL imeanza kutimua vumbi huku ligi ya Tanzania soon kuanza nayo.
Napenda kuanza biashara hii ya kuonyesha mpira hasa kwa ving'amuzi vya DSTV na AZAM ikiwa kuonyesha mechi za nje ya nchi na ndani hasa timu pendwa za watani wa jadi (Simba na Yanga).
Huu ndo uchambuzi wangu ambao nategemea kufanya makadirio kabla ya kuanza ujenzi na biashara kwa ujumla:
Ujenzi wa Banda kwa kutumia Mabati pamoja na umeme hasa kutokana na sehemu niliyopo ni ya kijijini (sio sana) itanigharimu Tshs 900,000
TV ya Kisasa (LED Inch 43) itanigharimu Tshs 900,000
Manunuzi ya Ving'amuzi vyote viwili (AZAM - Tshs 135,000 & DSTV - Tshs 109,000)
Jumla = Tshs 244,000
Vifurushi Vya Kujiunga Ndani husika (AZAM PLUS - Tshs 23,000 & DSTV Compact - Tshs 69,000)
Jumla = Tshs 92,000
Kabati kwa ajili ya kuwekea/kuhifadhi TV itanigharimu Tshs 85,000
Matumizi mengine ya dharura (Emergency) ndani ya ujenzi ni Tshs 200,000
Jumla Ya Mahitaji Na Gharama Kwa Ujumla Itanigharimu Kiasi Cha Tshs 2,421,000
Nakaribisha maoni na mapendekezo yenu yaweze kunisaidia mimi pamoja na wanajukwaa wengine wenye malengo kama yangu ya kuanzisha biashara hii.
Asanteni[emoji120]