Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Biashara ya Kuonesha Mpira wa Miguu (Kibanda-umiza): Fahamu Kiasi cha Mtaji, Vifaa na Mbinu za Uendeshaji

Kwenye TV naona umepiga hesabu Expensive Sana.

Inchi 43 inapatkana kwa laki 550,000 bei ya JUMLA.

Ukiwa na 1million na laki moja unapata TV mbili.

Kwenye bajeti yako ya awali ya 900,000 .

Ongezea laki mbili upate TV mbili kwa bei ya Jumla.
Tv inchi 43 kwa laki 5 ni kampuni ipi?
 
Ni kwel mkuu lakin hapa nilipo mm weng ni boda boda na wazee ndio weng czan kam nitawapat kweny movie
Jomba jamaa kakupa nondo kali yaani wale walio wahi dak kadhaa unawaonjesha vitu hivyo kidogo kabla au baada ya mechi watanasa tu. Fungua kichwa. Utajua Menu ipi watu wanataka kula.
 
Vinginevyo ajiandae kuoga mvua ya matusi.
hapa kwenye mvua ya matusi ajiandae na asiwe mkali hata kama akitukaniwa mama yake mzazi, utasikia ma***ya wa kike wewe, mara ****** ni hatari sana
 
Kitambulisho muhimu nalifahamu hilo, thanks kwa kunikumbusha pia.

Kuhusu TV ndugu ntaanza na moja mbeleni ntaongeza nyingine kadiri ya mapato yatakavyo kuwa.

Asante Tena.

Hiyo pesa ukiongeza laki moja unapata za mtunba genuine Zanzibar kwa ukubwa huo.
 
Nilitaka kumwambia hili pia.

Labda cha kuongezea, aonyeshe na mieleka hata kwa kiingilio kidogo, kijijini atakuwa anapiga sana hela, kila jumanne na jumatano watu watakuwa wanajazana kwenye mieleka.
Kama ni Mpira unahitaj 169,000 kila mwezi ulipie Dstv(Premium )..not 69,000
 
Kwenye TV naona umepiga hesabu Expensive Sana.

Inchi 43 inapatkana kwa laki 550,000 bei ya JUMLA.

Ukiwa na 1million na laki moja unapata TV mbili.

Kwenye bajeti yako ya awali ya 900,000 .

Ongezea laki mbili upate TV mbili kwa bei ya Jumla.
Kweli kabisa mkuu mimi nilienda zenji nkachukua tv mbili 43" kwa laki nne nne. Nkaleta bongo hapa plus all transportation cost 970k .
 
Moja kati ya michezo pendwa sana kwa vijana na hata wazee na watoto kwa ujumla ni mchezo wa miguu, mpira (Football). Ligi nyingi sana zimeanza na zinatarajiwa kuanza ndani ya mwezi huu, huku tayari ligi pendwa ya EPL imeanza kutimua vumbi huku ligi ya Tanzania soon kuanza nayo.

Napenda kuanza biashara hii ya kuonyesha mpira hasa kwa ving'amuzi vya DSTV na AZAM ikiwa kuonyesha mechi za nje ya nchi na ndani hasa timu pendwa za watani wa jadi (Simba na Yanga).

Huu ndo uchambuzi wangu ambao nategemea kufanya makadirio kabla ya kuanza ujenzi na biashara kwa ujumla:

Ujenzi wa Banda kwa kutumia Mabati pamoja na umeme hasa kutokana na sehemu niliyopo ni ya kijijini (sio sana) itanigharimu Tshs 900,000

TV ya Kisasa (LED Inch 43) itanigharimu Tshs 900,000

Manunuzi ya Ving'amuzi vyote viwili (AZAM - Tshs 135,000 & DSTV - Tshs 109,000)
Jumla = Tshs 244,000

Vifurushi Vya Kujiunga Ndani husika (AZAM PLUS - Tshs 23,000 & DSTV Compact - Tshs 69,000)
Jumla = Tshs 92,000

Kabati kwa ajili ya kuwekea/kuhifadhi TV itanigharimu Tshs 85,000

Matumizi mengine ya dharura (Emergency) ndani ya ujenzi ni Tshs 200,000

Jumla Ya Mahitaji Na Gharama Kwa Ujumla Itanigharimu Kiasi Cha Tshs 2,421,000

Nakaribisha maoni na mapendekezo yenu yaweze kunisaidia mimi pamoja na wanajukwaa wengine wenye malengo kama yangu ya kuanzisha biashara hii.

Asanteni[emoji120]
Kama sehemu ulipo kuna ving'amzi vya Canal+ ni bora utumie hicho kwa ligi zote za nje kuliko kutumia dstv coz canal+ kwa
mwezi Tsh.40, 000/- na unaonesha ligi zote kubwa duniani.
 
Kweli kabisa mkuu mimi nilienda zenji nkachukua tv mbili 43" kwa laki nne nne. Nkaleta bongo hapa plus all transportation cost 970k .
Asante sana kaka kwa ushauri, japo nipo Arusha kwa sasa naona kama gharama ya TV na usafirishaji kwa ujumla itakuwa kubwa zaidi.
 
Asante sana kaka kwa ushauri, japo nipo Arusha kwa sasa naona kama gharama ya TV na usafirishaji kwa ujumla itakuwa kubwa zaidi.
Arusha unataka fungua sehemu gani,niko kwenye hii game takupa ushauri.
 
Nataka nifungue biashara ya kuonesha mpira live ligi na makombe ya Ulaya.

Nimekua nikifikira kununua dekoda 2 za dstv na vifurushi vyao ila nikawaza hui gharama naweza kuikwepa kwa kutumia laptop, website za mechi live na internet ya smile 4g niwe nazirusha mechi live kwenye flat screen mbili na hii itakuwa sio gharama.

Je, kuna changamoto zipi nazoweza kuzipata nikitumia internet kuoneshea mechi.
 
Sio reliable, Mashabiki wenye hasira Kali wanaweza kuvunja TV ikianza kunata nata hasa timu ikiwa imefungwa. Na unaweza unaangalia mpira mwenyewe ikaonesha fresh tu Ila watu wakijazana kwenye Banda signal nazo zikaanza kuleta tabu na speed kudrop.

Kuna jamaa wa canal watu wanatumia Bei zao Ni affordable.

Pia DStv Wana DStv now unaweza ukajaribu kwa decoder moja na service ya DStv now uangalie Kama online inaweza kuwa nzuri.
 
Back
Top Bottom