Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,968
- 36,044
Miongoni mwa biashara pasua kichwa ni hii biashara ya kumsimamia msanii haswa msanii wa muziki .
Awali ya yote, wengi hawajui kuna utofauti kati ya sponsor na manager.
Manager kiuhalisia inabidi yeye ndiye awe analipwa na msanii ili amsimamie kazi zake lakini kibongo bongo ni tofauti. Kibongo bongo ukishakuwa meneja automatically umeshakuwa baba/mama wa msanii , msanii kaishiwa umeme , meneja unapigiwa simu, msanii hajala meneja unapigiwa simu.
Baba/mama wa msanii anaumwa ,meneja unapigiwa simu nk.
Haya yote nina ushahidi nayo maana nimeshafanya hii biashara ya kusimamia wasanii.
Tuachane na hilo,
Katika tasnia ya muziki na burudani, watu wengi huona mafanikio ya msanii jukwaani, nyimbo zinazotamba, mashabiki wengi na maisha ya kifahari. Lakini nyuma ya mafanikio hayo kuna kazi kubwa sana inayofanywa na watu waliopo nyuma ya pazia, hasa meneja wa msanii (artist manager).
Kusimamia msanii si kazi rahisi kama watu wengi wanavyofikiria. Ni kazi inayohitaji muda, fedha, uvumilivu, akili ya biashara na uwezo mkubwa wa kushughulikia changamoto nyingi kwa wakati mmoja.
Meneja wa msanii (artist manager) huwa na majukumu kama:
Kupanga kazi na ratiba za msanii,
Kutafuta matamasha (shows)
Kujadili mikataba ya kazi
Kusimamia fedha za kazi za msanii
Kusimamia mahusiano na media
Kupanga mikakati ya kukuza brand ya msanii
Kwa kifupi, meneja ndiye nguzo ya maendeleo ya msanii.
B. Gharama Kubwa za Kusimamia Msanii
Watu wengi hudhani meneja hupata faida haraka, lakini ukweli ni kwamba mara nyingi meneja hutumia fedha nyingi sana kabla ya kuona faida yoyote na mara nyingi huambulia hasara au usaliti.
Baadhi ya gharama hizo ni:
1. Gharama za Kurekodi Muziki
Msanii ili atoke lazima atoe nyimbo nzuri , ni wasanii wachache sana wanarekodi kwa gharama zao , wengi wanawategemea mameneja wao .
2. Gharama za Video za Muziki
Ili msanii aweze kukuza brand yake /apanue soko lake la muziki lazima awekeze gharama ya kutosha kwenye kushoot video ili wimbo uende mbali zaidi.
Video nzuri itahitaji
Kamera za kisasa
Location
Wachezaji
Editing
Hizi zote ni gharama.
3. Gharama za Promotion
Bila promotion wimbo hauwezi kufika kwa watu.
Promotion ya wimbo mmoja gharama yake unanunua IST kabisa 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Promotion inaweza kuhusisha:
Media tours (TV na Radio stations)
Social media ads
Kulipa watu wafanye challenge ya wimbo .
4. Gharama za Usafiri
Msanii anahitaji kusafiri kwenda:
Shows
Interviews
Recording
Media tours
Hii inahusisha:
Nauli
Malazi
Chakula
5. Gharama za Muonekano wa Msanii
Image ya msanii ni muhimu sana katika soko la muziki.
Hii inahitaji:
Nguo nzuri
Styling
Makeup
Photoshoot
Kumbuka msanii harudii nguo haswa kwenye show, lazima bajeti ya nguo iwekwe angalau laki 5 ya mavazi .
Changamoto zingine za kumsimamia msanii ni hizi.
1. Nidhamu
Baadhi ya wasanii wana nidhamu mbovu kama vile
Kutokufuata ratiba
Ulevi
Kutoheshimu mikataba
Kukosa nidhamu
Meneja hulazimika kushughulika na tabia hizi kila siku.
2. Migogoro ya Fedha
Yani ukija kwenye mambo ya pesa ndio kabisa pasua kichwa
.
Mara nyingi msanii tamaa zinamuingia wengine wanamjaza kwamba meneja wako anakunyonya .
3. Ushindani Mkubwa wa Soko
Tasnia ya muziki ina ushindani mkubwa sana.
Kila siku kuna:
Wasanii wapya
Nyimbo mpya
Trends mpya
Meneja anahitaji kuwa na mikakati ya kuhakikisha msanii wake anaendelea kuwa relevant.
4. Kutokuwa na uhakika wa Mapato
Si kila wimbo unakuwa hit.
Meneja anaweza kutumia pesa nyingi lakini:
Wimbo usipate views
Usipate shows
Usipate mapato
Hii ni hatari kubwa ya biashara.
5. Usaliti
Wakati mwingine wasanii:
Huachana na meneja wao baada ya kupata umaarufu
Huchukuliwa na management nyingine
Hii ni changamoto kubwa sana kwa mameneja.
4. Muda na Kujitoa kwa Meneja
Kusimamia msanii si kazi ya saa 8 kama kazi nyingine.
Meneja anahitaji kuwa tayari:
Kupokea simu usiku
Kushughulikia matatizo ya ghafla
Kusafiri mara kwa mara
Kufanya kazi bila kupumzika
Ni kazi inayohitaji kujitoa sana.
.
.
.
.
.
Ili angalau biashara ya muziki imlipe meneja basi msanii kwa show alipwe angalau milioni 20 ,ambapo meneja hapo inabidi achukue milioni 17 msanii milioni tatu.
Lakini ujinga wa msanii kwenye mapato napo anataka mgawane pasu kwa pasu.
Sehemu pekee msanii atagawana pasu kwa pasu na meneja ni pale msanii anapata ubalozi wa kampuni fulani.
Hata kwenye digital platforms msanii inabidi apate 40% pekee nyingine zinazobaki zinaenda kwenye uongozi wake.