Dah ndiyo maana kayumba the doctor aliona mambo yasiwe mengi akamtema mwanetu ,mara Nay akajitutumua nyimbo mbili naye akala kona ila sanaaa🙌
Nikampata msanii mmoja kijijini sana akasema ana wimbo ameshoot kwa gharama zake na watu wanampenda sqna ,sasa anataka afanye show hapo hapo kijijini ila mimi nigharamikie kila kitu na mwisho kuanzia hapo nitakuwa manager wake .
Huku na huku naona wanakijiji wanamkubali sio mchezo ,masikini mimi mtoto wa chole mizimuni naipe da hela nikaamua nijiingize kichwa kichwa ,mabango ,DJ mavazi na takataka zote ulizosema kwa makubaliano hela yangu itarudi baada ya show na hapo nitakula faida na yeye nitampa chochote kitu ila nitaendelea kummanage .
Matangazo kata nzima ,nikazama Tunduma nikawabeba wadada wacheza uchi waje wafanye mazoezj na msanii wangu ili siku hiyo watoe sebene la kufa mtu .
Wakakubali juma zima wanakula na kunywa hela yangu huku mazoezi ya kufanya dhambi jukwani yanaendelea .
Nikapanga gharama za kiingilio kulingana hiyo siku ni siku ya wakulima hivyo nikajua watu wana hela hawawezi kupiga chenga .
Dj kakubali kupiga kazi kwa nusu gharama pamoja na wanenguaji ili tukimalizq nilipe gharama zinazobaki .
Siku ya tukio niko ndani ya suti kali MR meneja nazunguka huku na kule kuhakikisha jambo halikwami ,ila dunia hii tembea kote ila hakuna watu wanafiki kama wanavijiji ,kila waliposikia matangazo na bado na kadi za mualiko nilitengeneza kwa maneno ya pokeeni show ya mtoto wenu mzione kazi za mtoto wenu mumbariki na hakika walinipa maneno mazuri nikawa nawaza haya mahela nikiyapata nitawakomoa aisee .
Siku ilipowadia ,sehemu ya kuingia watu walau Mia nne kulingana na hesabu za haraka ili nipate kurudisha gharama zangu walikuwa watu sabini na hao wanaingia wanatoka hakuna utulivu na bado walioko nje wanadai wanasubiri fungulia mbwa usiku ukifika 😀
Nikawaza DJ ananidai ,wadada wanenguaji wanadai ,team zote hizo zilikula sehemu kwa mama mmoja muuza chakula nako nadaiwa laki na nusu .
Nikakumbuka na vinywaji vya msanii na wenziye walikunywa ili kupata mzuka ,nikicheki bado ulingo hausomeki nakumbuka by saa tano usku niliwasha kamkweche kangu taratibu nikaaga naelekea nyumbani nichukue vitu fulani ikawa njia ya kukikimbia kijiji nikazima na simu nikaenda bar fulani kunywa pombe ili niweke akili sawa .
By saa kumi na moja nikarequest chumba nikalqza fuvu ili nijue kutakucha vipi ,saa mbili nipo job namuona DJ kwa mbali na wenziye wanakuja ofisini ikabidi niwambie washikaji kuwa watimulie mbali hao jamaa sitaki kuonana na mtu .
Simu nawasha kumpigia ninayemtaka ila baadaye nikaona ni ujinga ilibidi niwatafute tukae meza moja tuzungumze ili yaende sawa.
Ila siwezi kusahau yale manjegeka aisee ,unachosema brother
Hance Mtanashati sina cha kuongeza zaidi nakusecond kwa kusema ile ni biashara kichaa kabisa