Natumia approach yako ila kwenye kuwaza hizo tshirts ulikosea mimi hata nisingejaribu hata kuziwaza. Hata uwe malaika, huwezi zalisha nguo Tanzania ukawa na competitive price dhidi ya anayeagiza China. Kuna factors nyingi za kiuchumi na kisiasa hukuanza kuziwaza.
Pia faida ya kuanza kuwa mchuuzi ni kuijua market vizuri. Ila sio uwe muuza nguo mfano, alafu hujui lolote kuhusu biashara nyingine.
Uwe unatafiti na kujitahidi kujua kila aina ya biashara na ujue trend na utabiri yajayo. Mfano unajua Magufuli kawa Rais na anapenda sera ya viwanda, na ana uchungu na taifa. Jua ukicheza kwenye vipaumbele vyake sijui sukari na uzalishaji nyama unakuwa safe. Akija Samia unajua ni sherehe na kufuja mali wewe wekeza kwenye hospitality na udalali wa kitaifa au kusafirisha rasilimali, kwa Samia ni rahisi kugawa rasilimali kuliko kuleta kitu kama "Make in Tanzania Initiative".
Then unajizatiti kwenye awamu hiyo ikulee kiasi ukija upepo mwingine haukuondoi kibiashara, unatafuta mazingira pendelevu kwanza ili ukae sawa.