Habari wanajukwaa
........................................................................................................
Update: MABADILIKO JUU YA KUPATA LESENI YA BIASHARA YA MIKOPO
Kwa mujbu wa notisi ya Benki Kuu ya Tanzania kuna mwongozo umetolewa w namna gami kampumi au mtu binafsi anaweza kufanya biashara hii ya kutoa mikopo
1. Suala la Mtaji
2. Jina la kampuni kuwa na neno linalotambulisha shughuli ya kampuni
3. Shughuli zilizoainishwa ktk MEMARTS kuwa za mwelekeo wa masuala ya fedha tu
4. Wamiliki wa kampn kuwa na elimu tambuzi juu ya biashara hata kama wameajiri wasimamizi
5. Taratibu za kupata kibali na leseni
6. Makundi yalivyogawanywa ie Tier 1,2,3 na 4 nk
..,.....................................................................................................
Vile vile tumeandaa semina juu ya notisi hiyo ya BOT kwa wadau wanaohitaji karibuni sana
........................................................................................................
Watu wengi wamekuwa wanauliza juu ya suala hili wengine ikiwa hapa jukwaani na wengine kwa kuja PM. Naona vema kuweka wazi suala hili katika jukwaa letu maarufu la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali.
Mwongozo huu unaweka bayana juu ya kusajili kampuni ya kutoa Mikopo binafsi na upatikanaji wa leseni yake (Application conditions for Microcredit business license)
Utangulizi
Microcredit company ni kampuni inayojihusisha na kutoa MIKOPO TU kwa mtaji binafsi iliyonayo na hairuhusiwi kuweka pesa za mtu hii itambulike hivyo.
Ukitaka masuala ya kuweka na kutoa pesa huko ni Microfinance.
Leseni ya biashara hii inatolewa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, ofisi za BRELA Ghorofa ya 5, jengo la ushirika, brbr ya Lumumba, Mnazi mmoja, Dar es Salaam.
Mambo muhimu yanayotakiwa ni
1. Usajili - BRELA
Hapa ni kusajili kampuni au partners inategemea mmejipanga vipi na hufanyika BRELA. Mtaji lazima uwe mkubwa, jitahidi uwe japo 50mil+ japo nashauri uwe mkubwa (mfano x00mil) zaidi kwani biashara hii inaweza kukua hadi ukahitaji kuanza huduma za kutoa na kuweka pesa (microfinance)
Hakikisha MEMARTS au Partnership deed yenu isiwe yenye mlengo (Objects) wa biashara yoyote isiyosimamiwa na Benki Kuu
2. TIN-TRA
Sajili TIN ya kampuni TRA, pata TAX CLEARANCE CERTIFICATE ambayo utaandika inaenda Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
3. Sera ya ukopeshaji (lending policy and procedure Manual)
Uwe na hii sera ya ukopeshaji ambayo itatoa mwongozo wa riba, taratibu, kanuni nk
4. CV za wanahisa
Wanahisa/wakurugenzi/wahasibu wawe na CV na vyeti kuonyesha uzoefu wao ktk tasnia ya fedha
5. Taarifa za kifedha
Walau taarifa za fedha (bank statements) zao wanahisa au kampuni walau kwa miezi mitatu
6. Uthibitisho wa uraia
Kopi za vitambulisho vya Taifa vilivyothibitishwa
7. Mkataba wa Pango
Uwe umethibitishwa kisheria na vilivile umelipiwa kodi ya stempu TRA
8. Nyaraka zote zibanwe kama kitabu
Wazoefu na wajuzi zaidi wanaweza kuongezea zaidi. Karibuni kwa mjadala
Kwa huduma hizi unaweza kumtumia Consultant alie jirani yako au ukatucheki kwa email:
consultafrolinktz@gmail.com na mobile/whatsapp: 0659211222/0777777766/0755411455