Biashara ya Kuuza Mkaa: Uzoefu, Vibali vya kuchoma, Changamoto na Ushauri

vp kwa mkoa mwanza gharama za kuchoma mkaa zinakuwaje?
msaada tafadhali
 
Wadau,

Nataka kuanzisha biashara ya mkaa hapa Dar, jumla na rejareja.

Naombwa kujuzwa sehemu naweza upata mkaa kwa jumla kwa bei nafuu hapa Dar

Au msaada wa mawazo kwa aliyejaribu.
 
Kama upo serious mm nipo rufiji naweza kukuletea kiasi utakacho ila uwe na store nipm tufanye biashara.
 
Nipm nikuunganishe na mfanyabiashara huyu. Anachukulia pori la Kiserengwe huko kupita bagamoyo. Gunia moja linanuliwa elfu 18+ usafiri kwenye magari yenye kibari cha kusafirisha mkaa ni elfu18.jumla mpaka gunia linafika Dar ni elf 36.mkaa wa kule ni mgumu na mzito.
 
Wana jukwaa poleni na pilika. Naamini huku Kuna wazoefu WA biashara ya mkaa.
Niko Lindi, lengo nijue changamoto zake, soko lake kwa Dar es. Salaam.
karibuni
 
Changamoto kubwa ni hawa maafisa misitu na askari barabarani ili kuweza kuufikisha mzigo wako ni lazima uwe na kibali cha kusafirisha au kukata mkaa .kingine ambacho ni cha msingi sana uwe na bulungutu la kutosha si unajua tena jamaa wa barabarani.
 
Changamoto kubwa ni hawa maafisa misitu na askari barabarani ili kuweza kuufikisha mzigo wako ni lazima uwe na kibali cha kusafirisha au kukata mkaa .kingine ambacho ni cha msingi sana uwe na bulungutu la kutosha si unajua tena jamaa wa barabarani.

Na kweli. Kuhusu kibali hakina shida Sana. Kuhusu soko ndo inanipa mtihani. Sina mtaji, ILA nataka niende benki nikakope mil. 5. Kwa mchanganuo niliopewa mil. 4,700,000 inatosh kuanzia. Hapo had usafiri. Je niko sahihi au
 
Hebu kabla ya kuingia bank,rudia utafiti wako kama utakuta kuna mtu alitoka kimaisha kwa kufanya biashara ya mkaa.Ukimpata rudi utuambie hapa jukwaani.Bora ufuge kuliko biashara ya mkaa
 
biashara ya mkaa ni nzuri hasa kama ukiifanya full( kuchoma na kusafira) kikubwa ni mtaji. mtaji ulioutaja ni mkubwa na unatosha na kubaki.gunia kubwa shanga mbili kununua na kusafirisha itakugarimu elfu 40 mpaka 45.(mali asili na polisi 20,gari elfu 10,mkaa elfu 12).

kikubwa uwe na store au wateja wa store wa kuwaachia unapofika dar wakupe cash yako.
 
na ni biashara inayolipa sana elfu 40 * 80= mil 3.2 kama utachoma mwenyewegarama zitapungua maana gunia bei yake itafika hata elfu 7 kwa maana ya garama za uchomaji. hela hiyo maana yake unafikisha gunia 80 dar. na mkaa wa kusini kwanzia rufiji somanga,lindi ni kwanzia elfu 55 kwa gunia la shanga mbili dar na unakubalika sana maana unakuwa wa ukweli maana kuna miti ya uhakika sana ya mkaa maeneo hayo.
 
Mkuu nashukuru Sana. Uliwahi kuifanya hii ili unipe uzoefu zaidi?
 
Hebu kabla ya kuingia bank,rudia utafiti wako kama utakuta kuna mtu alitoka kimaisha kwa kufanya biashara ya mkaa.Ukimpata rudi utuambie hapa jukwaani.Bora ufuge kuliko biashara ya mkaa

asante mkuu. Nimefatilia kwa huyu mwenyeji wangu ambaye ananifumdisha hii biashara. Ye ameifanya miaka 10, na naona maendleo yake mazuri. Mtaji wake uko njema amehamia kwenye mbao
 
Nina plan ya kufanya biashara ya mkaa kuutoa iringa to dar bt naomba guyz mnishauri risk za hii biashara hususani mm ni mchangs kwe biashara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…