Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Biashara ya madini ni kichaa. Kaka yangu kapoteza milioni 120 mwezi huu nimemkuta ameshaanza kudata

Biashara ya madini kama unataka kuifanya inabidi uanze kidogo na ukae na wanunuzi wenye uzoefu ujifunze kidogo kidogo.

Huyo itakuwa alikuwa na mtaji ila madini hayajui.

Hata wazoefu huwa mtaji unatikisika mara kwa mara.

Nimekaa huko napajua sana, hakuna aina ya madini, eneo sifahamu.
 
Kwa kawaida kwenye uchimbaji haswa dhahabu iyo million 120 alitakiwa awe nyuma ya mtu mwenye njia za iyo kazi, kwa ujumla huo si mtaji wa kuchimba ni bora ukae mjini na duka lako la mangi! Na mbaya zaidi ukiona anakwambia kapoteza 120m kwa hakika ni nusu ya hizo pesa ndiyo imeingia kazini zingine kapigwa.
Uchimbaji unahitaji mtaji, techonologia, nguvu kazi, uzoefu, connection na mwisho ambayo ndo muhimu ni uvumilivu/ ustahimilivu.
 
Ananunua udongo anaenda kuozesha.

Hiyo ndo biashara kichaa kuliko zote. Wewe au mtu yeyote yule asijefanya biashara ya kununua rudio 101% unazika hela.

Mtu hawezi chimba ajue rudio lake linasoma akuuzie wewe. Ni either anajua halisomi au akupige bei usitengeneze faida.

Kuna ujanja mwingi sana kwenye marudio ya kununua utanunua mavumbi tu. Hakuna mtu timamu ananunua rudio au kuuza rudio lake wakati anajua linasoma. Usijaribu.
 
Kwa kawaida kwenye uchimbaji haswa dhahabu iyo million 120 alitakiwa awe nyuma ya mtu mwenye njia za iyo kazi, kwa ujumla huo si mtaji wa kuchimba ni bora ukae mjini na duka lako la mangi! Na mbaya zaidi ukiona anakwambia kapoteza 120m kwa hakika ni nusu ya hizo pesa ndiyo imeingia kazini zingine kapigwa.
Uchimbaji unahitaji mtaji, techonologia, nguvu kazi, uzoefu, connection na mwisho ambayo ndo muhimu ni uvumilivu/ ustahimilivu.

Word.
 
Bro wako sio mvumilivu kwenye haya maisha. Nilishawahi poteza 270m, ni kweli iliniuma sana. Nilitulia kiume nikaendelea na maisha.

Nilishasahau na kutengeneza zaidi ya hiyo
Huenda hiyo hela kakopa, bora iwe yako na sio mkopo. Mali zako zote zitapigwa mnada na ghafla unakuwa masikini.
 
Bahati nasibu
Technologies na research...wabongo au weusi tunakwenda na mihemko ...hatuna fungu la kufanya research kwenye Mambo ya uwekezaji ...hio amount NI ndogo sana kwenye tafiti ya madini...Luana maeneo wachina walishakata leseni ya madini nzega vitalu Kama 8 ..walimaliza zaidi ya miaka mitatu wanafanya tafiti kujua wapi waanzie...kwa mtaji kiasi gani yaani ukiangalia gharama walizo tumia Hadi kuja kuanza kuchimba Kama wachimbaji wadogo na techinologia ya uchenjuaji kubwa...unaona kabisa wabongo bado na tunafanya betingi kwenye uchimbaji wa dhahabu...wachache sana wanaofaidika baada ya wachimbaji wadogo kumaliza nguvu na rasilimali zao kuchimba na kuchenjua kizamazakale na kuacha Mali nyingi kwenye madongo senga...hio hela kwa wachimbaji walioserius NI kuungana wenye mtaji Kama. Huo nankununua tekinolojia na kufanya uwekezaji wenye tija..Google mitambo na ya kuchenjua dhahabu ya kisasa inayosaga mawe hata yakiwa yamelowa na kukamata dhahabu Bei yake ujue huyo kapoteza tu just a peanut kwenye uwanja wa dhahabu...hio hela inatosha tunkununua fuso dumps truck ya kubebea wawekezaji mawe au madongo ya wachimbaji wadogo...ukipewa hisa kwa wachimbaji wadogo na unamtaji Kama huo NI rahisi kupata hasara chap mfano hisa ya kuvuta maji na kununua mafuta na kulipa wafanyakazi wengine mwisho wa siku mje mgawane senga(dongo la dhahabu) utaona NI bahati na sibu hutoboi miezi 6 hela ishakata
 
Biashara zote zina faida na hasara, ila ya madini yataka usikurupuke anza biashara nyuma ya mtu ukiisoma na kuzijua njia zake zote hasa wale wapiga chabo ili ununue mchanga, kwenye duara kama huna vifaa madhubuti vya kupima mali ilipo utajikuta unaua mke na watoto ukipeleka viungo kwa waganga ili upate mkanda wa madini la sivyo ndo ivo pesa itaisha ukichimba moram
Kweli mkuu watu wanadanganywa wanamaliza ndugu kwa FAIDA sijui za Nani wakati wazungu na wachina wanawekeza tafiti na techinologia...kila dongo Lina dhahabu Ila utofauti ninkuwa utatumia gharama kiasi gani kuchakata dongo kubwa kiasi gani kupata kilo moja hapo hapo wabongo wengi hupotea na kupoteza hela...unaweza kutumia million 200 kununua na kuchakata Tani 70za udongo ambazo UTAPATA dhahabu gram 250...Hadi kilo moja ukienda sokoni unaweza kuikataa hio hela au kuikimbia kabon plant maana hata ukiiuza huwezi kulipa gharama ambazo ushakopa kwa watenda kazi
 
Mbona hao wazungu na wachina nao wanafanya ulozi Migodini?
 
Madini ni technology tu mkuu, wenye mitambo yao mizuri hawabahatishi ni vipimo tu vinawaelekeza
Tatizo la investor wengi bado wanafanya kazi kienyeji, wakat wkutoka nje wanakuja na mashine zao, wanapima ki science, matokeo yanaonekana.
 
Aisee naandika huu Uzi nikiwa nimekuja kumtembelea kaka yangu hospital hapa Mbeya, aisee hii biashara sio ya kuingilia kichwa kichwa.

Huwezi amini nipo hospitali maana broo kama akili zishaanza kuwehuka, vitu anavyoongea havieleweki aisee, haamini kama kafukia milioni 120.

Nawashauri ndugu zangu wana jamiiforums hii sio biashara ya kufanya, ni kama inauchawi fulani hivi!
Kaka lako ni popoma! Usitolee mfano majitu yaliyofeli! Mimi kaka yangu kwa mwaka jana aliweka milioni 150 juzi kati ametusua bilioni 1.5
 
Aisee naandika huu Uzi nikiwa nimekuja kumtembelea kaka yangu hospital hapa Mbeya, aisee hii biashara sio ya kuingilia kichwa kichwa.

Huwezi amini nipo hospitali maana broo kama akili zishaanza kuwehuka, vitu anavyoongea havieleweki aisee, haamini kama kafukia milioni 120.

Nawashauri ndugu zangu wana jamiiforums hii sio biashara ya kufanya, ni kama inauchawi fulani hivi!
Kitendo cha kusema upo hospitali kumuona bro wako nskushauri huyo asirudi tena mgodini

Kama ungemkuta kwa mganga ningekuambia muache

Hawa mabilionea wa madini unaowaona wanawajua waganga wote nchi nzima, hiyo kazi ni ya ndumba haswa
 
Yaani maneno anayoongea nashindwa kumuelewa yaani kama kadata hivi kumbe uchizi ni rahisi sana kuupata
Poleni wandugu,
Biashara ya uchimbaji wa madini Ina changamoto zaidi na nyingi.
Kuna Mambo unatakiwa kuyafuata na kuyazingatia kabla haujaendelea na hiyo kazi.
 
Back
Top Bottom