Amazon Woman
JF-Expert Member
- Aug 24, 2016
- 796
- 1,187
[emoji23][emoji23][emoji23]dhababu haina utofauti na kamali.Hii biashara inakubidi uwe
1: mwizi wa macho kbs.(kuchezea mzani)
2.roho mbaya (utapeli kwa wateja wako)esp kwenue calculations..
I have been there...niliamua kuiacha!
Na serikali ya Magu mnagawana faida mnoo!..
Shida kuu iko kwenye soko...hawa wenye majiko wanachzea sana bei...yaan matajiri wanaambizana leo tutanunua kwa bei hii...! Wanaweza panga kununia kwa 85000/...lakini soko la dunia linasoma figure nyingine!
Ukitaka kumake labda uwe na jiko...ila kununua dhahabu na kwenda kuuza faida ni ndogo...( kule jikoni kama huna uzoefu watakuibia had utabasamu hata kama umepewa habari mbovu)
Unaweza nunua kwa 80000 jikoni ukakuta 77000!..na pia ubora wa dhahabu(purity)... Unauziwa mzigo kwa 80000@gramu lakini jikoni purity ikisoma 78%, 77% jua imekula kwako!
So unajikuta mtaji unakatika polepole!
Kifupi toka serikali hii iingie imeharibu...! Kodi zimekua juu mnooo!...labda ukutane na jiko wasilojua kucalculate unaweza ondoka na super profit!
Ushauri ...nenda kwanza migodini kasome kwamza mchezo kwa hao wanunuaji dhahabu( kota).., then utaamua mwenyewe!na usiwe mbahili kuwezesha watu ... Usipompa hela mteja wako jioni anaenda uza kwingine unakosa mzigo ..ukipata ufate faida atleast kwa siku ukusanye gramu kuanzia 25 hivi bila kodi kodi zao za wizi unaondoka hata na 100k&120k!daily...!
Kodi hapo unaweza acha zaidi ya 40!ila kama wenye majiko waelewa mnapoozeana! (Sasa hapa na wenyewe wanaogopa wanajua wewe mpelelezi..mie had leo wanajua ni mpelelezi..very dangerous))...tena kama ndo una sura sio ya kimgodi utakwepwa had ujute ..watajua ww mpelelezi...watakukata kodi kama ilivyo ada
Kuna makota wanapeleka kwa wahindi ..ananunua kwa shiling 80000 anaenda uza 87(mfano)lakini hawakupi deal hata siku moja...!..kifupi uwe mwizi mwizi ( Kuonea wateja...kuwaibia hela kbs )mjanja mjanja utatoka!ukiwa humble hiyo 5m itaisha august tu
HELA YA DHAHABU TAMU SANA!
Sema watu wanapigwa mno esp wageni. Kuna mtu alinunua mzigo ndani copper nje wakafanya coating ya gold, a very thin layer ukisugua two times unaona copper hiyoooo