Kuna sources nyingi sana kwenye internet ila nafikiri tunaongelea vitu viwili tofauti. Mimi naongelea bei ya mti shambani siongelei bei ya mbao ulaya iliyokuwa processed tayari. Data zipo wizara ya maliasili na utalii na ni juu sana ila ni kwa miti iliyopandwa miaka hamsini iliyopita na serikali. Zinaonyesha bei za juu ila ni za kwenye makaratasi tu (za kisiasa for strategic planning). Nafikiri cha muhimu ni kuanzia na baseline data. Kama una mitiki kwenye uwanja wako Dar, halafu serikali ikakufidia kupanua barabara au kuendeleza hilo eneo, utalipwa kiasi gani? Hiyo ndio bei nzuri ya kutumia kwenye kufanya analysis kwa sababu hata wataalamu wengi ukiwauliza bei wanakwambia hakuna soko la ndani ni la nje tu. Kama utapata mtu ameuza mitiki hapa Tanzania shambani naomba utujulishe miti ilikuwa na umri gani na iliuzwa kiasi gani kwa ujazo au kwa mti.
Tumeanza na trial ya miti 600 kwenye ekari moja tuone kama itakwenda vizuri mwaka ujao tutaingia kwa gia kubwa. Mbegu tunanunua SUA, shs 1,000 kwa mche. Ila mvua zinatusumbua.
Nawasilisha.