Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tuma mail address ili nikuunganishe tuanze kazi.
Ziko Tanzania kakaZipo wapi congo au zaire
Mitiki inamea vizuri sehemu zenye joto na unyevunyevu wa kutosha kama Kilombero, Longuza,Kyela, Muhoro nk. Sehemu zingine inaota lakini haifikii viwango.
Nashukuru mkuu kwa ushauri mzuri. Je ni mikoa gani ninaweza kupata ardhi ya kununua kwa ajili ya kupanda miti ya mbao tukiachana na mikoa ya njombe na Iringa?
Mkuu KVM na Malila! Nawashukuru sana kwa moyo wenu wakupenda ku-share information ambazo zinaweza zikafuta ufukara kwa watu tuliowengi. Ni watu wachache wenye mioyo ya kutaka kujuza wengine kwenye mambo yamaana kama haya.Mikoa yote unaweza kuotesha miti ya mbao kwa sababu kila mkoa kuna aina ya mti unaomea vizuri, sasa kuna miti ya muda mfupi ( 10yrs to 15yrs), kuna miti ya muda mrefu ( 15yrs to 25) na kuna miti ambayo ukiotesha wewe, hata mtoto wako hatavuna.
Tatizo linaanzia hapo kwenye muda, mikoa yote ambayo inaangukia kundi la pili,wengi wanadhani haiwezi kuotesha miti ya mbao, kwa hiyo tunadhani ile mikoa ya kundi la kwanza ndio pekee.
Mtiki ni 25yrs, upo tayari kusubiri?
Cyprus ni 15/25yrs je utasubiri?
Pinus patula 10/15yrs
Eucalyptus 6yrs to infinite - kuanzia poles,nguzo mpaka mbao
Accrocarpus 9yrs to 12yrs.
Pinus patula inamea vizuri nyanda za juu kusini, sasa hivi hadi Bukoba/Pemba iko na inavunwa mapema. Lakini ukiniambia nipande Mvule unaomea vizuri Tabora, halafu nivune baada ya miaka 70 !!!!!!! hesabu inakataa.
Mimi nigependa kuwahamasisha wanjf kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.
Mimi nilianza kupanda miti hii kama miaka kumi iliyopita. Nimepanda miti mingi kila mwaka bila kukosa. Kwa sasa ninazo ekari nyingi za miti hii. Vile vile miaka ya karibuni nimepanda eucalyptus.
Wakati naanza kupanda miti mche mmoja nilikuwa nanunua kwa shs 50 na kuupanda kwa shs 20. Kwa vile napanda miti mingi (zaidi ya laki moja kwa mwaka) baadaye niliamua kuotesha miche mimi mwenyewe ili kupunguza gharama.
Gharama zaidi ya miche na upandaji ni barabara za moto kuzunguka msitu. Hata hivyo nilinunua ngómbe na kuwaweka kwenye shamba ili wale majani yanayozunguka msitu. Wamenisaidia sana.
Unaweza kupanda miti kidogo kidogo kila mwaka kutumia mshahara wako kama nilivyofanya mimi. Baada ya miaka kadhaa utakuwa na miti mingi na utaweza kuwa unauza miti au kupasua mbao kila mwaka.
Mlio anza zoezi la kupanda miti tunaomba uzoefu ili na sisi tujitose
Mkuu KVM na Malila! Nawashukuru sana kwa moyo wenu wakupenda ku-share information ambazo zinaweza zikafuta ufukara kwa watu tuliowengi. Ni watu wachache wenye mioyo ya kutaka kujuza wengine kwenye mambo yamaana kama haya.
Nimefuatilia thread yote toka ilipoanza Aprili 2012 (mwaka juzi sasa) mpakapost ya mwisho na niko very moved and geared!
Naomba mnishike mkono na mniongoze ili name nijifunze na nifuate njiayenu japo kwa mbali! Naomba mnijuze kuhusu malengo ya association yenu na jinsiya kujiunga.
Mungu awabariki sana.
Hiyo biashara Mufindi, Njombe na Makete inalipa sana. Kule Njombe vijijini kwa sasa mti mmoja wa kupasua mbao ukiuza jumla unakwenda kwa bei kati 10,000 mpaka 15,000 kutemegea na size yake na wateja wapo sio wakutafuta wanakufuata wenyewe, sasa ukiwa na miti 100,000 tayari milionea. mwenye nimenunua mashamba huko kwaajili ya kupanda Pines .
Karibu sana,
Hakuna kiingilio kabisa,cha umuhimu ni uaminifu wako tu, nipe mail yako kupitia pm ili tuanze mawasiliano ya moja kwa moja.