Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake


Asante kwa taarifa mkuu. tutatafutana.
 

Nashukuru, ngoja nijaribu njia hii na nyinginezo halafu nitarudisha majibu njia gani ziliota kwa haraka.
 
Mashamba wanauzaje huko? I would wish to venture in this deal this year. Kwa kuwa unasema umennua, nadhan itakuwa vyema kama ukanipa info za bei ya shamba ili niwe jirani yako huko.
 
Jamani maeneo ya chalinze -- lugoba ni miti gani inastawi vizuri..........
Kiongozi katika uwekezeji wa muda mrefu kama huu unahitaji kuwa na taarifa zinazojitosheleza na za kitaalam. Nakushauri wasiliana na ofisi za wakala wa mbegu za miti tanzania TTSA Tel: +255 232 603 192/3903 utajifunza mengi sana hususan mti gani upandwe mkoa gani. Pia wanauza mbegu za aina mbalimbali pale kitu amacho kinaweza kikakupunguzia cost sana kwenye uwekezaji wao. Hawa jamaa wanambegu bora, I would advice you ufike ofcn kwao kama una nia ya kuwekeza kwenye miti.
 
Kiongozi angalia haraka yako ya kuvuna usije ukajikuta unapanda mabua badala ya miti. Kinachotudrive kupanda mti wa aina fulani ni soko, usije ukajipandia miti inayokua haraka ukasahau kuassess marketability ya hiyo species.

What i would advice you ni kwamba wewe panda miti ambayo soko lake linafahamika kama hiyo Pinus spp, Eucalyptus spp au Teaks. Suala la muda wa kuvuna lisikupe pressure mana nadhan wewe shida yako ni pesa na sio utavuna lini. Ukiona wahitaji pesa haraka, nenda bank kakope harafu hilo shamba la miti litumie kama collateral then utapata hiyo hela utafanyia mambo yako wakati miti yako inaendelea kumea shambani. Yapo mabenk mengi ambayo wanakubali mashamba ya miti kutumika kama Collateral kwenye mikopo yao.
 
Hiyo bei mbona kubwa sana? TTSA Morogoro wanauza kilo moja kwa 7500 ambayo unaweza pata miche mingi sana! Ni mkoa gani huko mvua inaposumbua? Kigoma, ruvuma nadhan ardhi ni kubwa na mvua ni nyingi sana. Nimeona miteak iliyoota maekeo hayo ina afya nzuri sana suggesting that ukipanda huko itakuwa haraka zaid ya ile inayopandwa maeneo yenye uhaba wa mvua.
 

Asante kwa ushauri wako
 
Kwa sisi ambao tuko Dar unadhani tunaweza kupanda aina gani za miti ambao ni za muda mfupi?
 
Mimi naishi Mvomero, tayari nimeanza kupanda Mitiki na Nina zaidi ya ekari kumi hadi sasa. Kwa MVOMERO sio wengi waliohamasika kupanda Miti ingawa Miti Ni Bima ya uhakika. Nachukua nafasi hii kumwomba mkuu wa Wilaya yetu Mr. A. Mttaka kuhamasisha, kuhimiza Na kusimamia upandaji wa Miti kama mojawapo ya zao muhimu ili kuokoa mazingira, lakini pia kujijenga kiuchumi.
 
Huku pwani Bagamoyo haioti?

Kuanzia B/moyo mjini kuelekea Msata, ni ukanda ambao mitiki inamea vizuri, na mlingoti nimeuona leo umepandwa kidogo upande wa kulia kama unakwenda Fukayosi, nyuma kidogo.
 
Mimi nigependa kuwahamasisha wanJF kupanda miti ya mbao hasa mbao nyeupe (pines and cypress). Miti hii inasitawi sana sehemu za nyanda za juu kusini.

Huko maeneo wanauzaje ili tuje kuwekeza?
 
Karibu sana,Hakuna kiingilio kabisa,cha umuhimu ni uaminifu wako tu, nipe mail yako kupitia pm ili tuanze mawasiliano ya moja kwa moja.
Hallo Mkuu, hata me nimevutiwa na kilimo hiki na nimeshaanza kujiandaa na ninaomba msaada wenu na hasa kuingia katika organisation yenu ili nijfunze mengi zaidi.
 
Hallo Mkuu, hata me nimevutiwa na kilimo hiki na nimeshaanza kujiandaa na ninaomba msaada wenu na hasa kuingia katika organisation yenu ili nijfunze mengi zaidi..
Tuma mail address ili nikuunganishe tuanze kazi.
 
Mkuu wewe una shamba Dar? mi nilifikiri Dar hata kiwanja tu kupata ni issue
Dar kubwa ndugu yangu. Unadhani dar inaishiaa posta tu? Kuna maeneo kama kimbiji kote huko ni Dar na unaweza kumiliki shamba kwa bei pouwa tu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…