Ukikamilisha aliyokushauri
Shakel
empire unatakiwa kujisajili eneo utakalokuwa unauzia mbao mfano kama utauzia Dodoma nenda ofisi ya Tanzania Forest Service Agency ((TFS) Dodoma) watakusajili kwa Tsh 256,000/= pamoja na form ya maombi Tsh 5000/= (Renewable 01 July yearly). Baada ya hapo hakikisha mbao unazonunua zimevunwa halali i.e. unaweza kupata mbao kwa njia tatu:
1. Kuvuna katika msitu wa serikali (Hapa lazima uwe umeruhusiwa kuvuna (utakuwa na lesseni ya uvunaji))
2. Kununua kwa wananchi wenye mashamba ya miti (Uwe na vibali/barua ya mtendaji)
3. Kununua kwa wafanyabiashara maeneo tofauti (Uwe na nyaraka za kununulia i.e delivery note, Invoice na uthibitisho wa source ya mbao mfano leseni ya uvunaji)
Ukiwa navyo hivi vitu nenda ofisi ya TFS iliyo jirani na uliponunulia mzigo wataukagua halafu utapewa kibali cha kusafirishia (TP) mbao zako ambayo inalipiwa kwa gari ya tani 7 ni Tsh 6500/= na zaidi ya tani 7 ni Tsh 13,000/=. Pia utatakiwa kulipia ushuru wa halmashauri ambao hutofautiana halmashauri moja hadi nyingine either kwa pieces or ujazo (CBM).
Mkuu
DIBEGU nakutakia kila la kheri katika hii FURSA na wana JF wengine wanaweza kujazia ili ufanye kazi kwa ufanisi.