Biashara ya Mbao na Miti: Fahamu Uendeshaji, Faida na Changamoto zake

Kuna shamba kubwa kwel la miti ila miti yake ipo saiz ya kati kitu kama ina miaka sita au saba iv ni kama eka tisa iv nmeskia wanalitangaza kwa mill 100

Lipo kijiji gani? Kwa bei hiyo bora ununue kibali upasue msitu wa serikali. Miti ya miaka hiyo utapata mbao ngapi mpaka zirudishe hiyo hela jamani?
 
Mashamba hadi ya bure yapo,ila hayana sifa kwa mwenye mtaji mdogo. Bei ya chini kabisa ni Tsh 35,000/ mpaka 60,000/ kwa eka kwa maeneo ninayootesha miti mimi. Haya ya laki moja mpaka laki tatu yapo,ila mimi sikushauri kununua haya, kwa sababu hela nyingi unampa dalali. Kipo ki-blog fulani kinabamiza watu sana kwa hizi bei.

Ni lazima ofisi ya kijiji uingie, usinunulie kichochoroni kwa mjumbe, wala usitoe hela kabla hujamwona VEO, kamati ya ardhi ya kijiji na familia husika.

Eucalyptus ya Zimbabwe generation ya ngapi mkuu? Vijiji vingi vya Mufindi kusini miti hiyo inakubali, Kilolo Kusini,Njombe sehemu kubwa, Ludewa, ila Makete usiende, hakuna ardhi ya ukubwa huo. Kama utafika mpakani mwa Ruvuma na Njombe pia ni pazuri sana.

Cha msingi kikubwa ni uwepo wa mvua, manpower,miche na fire awareness ktk sehemu utakayo chagua.

Alafu kuhusu kupata hati ya hayo mashamba ukishanunua unapataje mkuu? Naomba kujuzwa.
 
alafu kuhusu kupata hati ya hayo mashamba ukishanunua unapataje mkuu? naomba kujuzwa

Hati kwa maana ya Title Deed au Hati za Mkurabita? Kama ni Title deed, habari yake ni ndefu na gharama. Kijiji lazima kiandike muhitasari kuonyesha kuwa ww ni mmiliki Ts 300,000/ to 500,000/, ksha unapeleka Wilayani, na hapa ndio kwaya inaanza wimbo.

Mkurabita, muhitasari wa kijiji unaupeleka idara ya ardhi Wilaya, wao wanaangalia kama kijiji hicho kama kimepimwa, kama kimepimwa, wanawasiliana na kamati ya ardhi ya kijj,unapangiwasiku,unakwenda naye shambani pamoja na kamati ya ardhi kuonyeshana mipaka na kupima Baada ya week 2 unapata.
 
Wandugu naomba msaada kwa mtu mwenye aidia ya biashara ya mbao kutoka iringa na kusafirisha kuuza mikoani, natanguliza shukurani.
 
Nawasalimu,

aina gani ya miti inatumika kuzalisha mirunda inavunwa bada ya muda gani. Soko likoje, bei ya mirunda ikoje kwa sasa.

(mirunda ni ile miti inayotumika wakati wa ujenzi wa linta au gorofa)
 
Nawasalimu,

aina gani ya miti inatumika kuzalisha mirunda,,,,,inavunwa bada ya muda gani,,,,,,,,soko likoje........bei ya mirunda ikoje kwa sasa.

(mirunda ni ile miti inayotumika wakati wa ujenzi wa linta au gorofa)

Eucalyptus,unaanza baada ya miaka sita hivi, ukipata Zimbabwe gereration yatatu, miaka mitano waweza vuna mirunda, factor kubwa ni sehemu ulikootesha.
 
Vipi mkuranga. Je, kunastawi? Kuna mtu yoyote mwenye experience eneo hilo? Na ni mitiki tu au kuna aina ingine pia?
 
Katika mkoa wa iringa mbao zinapatika Mafinga; Makambako na Njombe ambayo sasa ni mkoa; kila size ya mbao ipo ni wewe tu; mzigo wa kujaza gari kubwa yaani semi trailer unagharimu takriban milion 16; na mzigo wa kawaida ni milion kumi; kwasasa masoko mazuri ya mbao yanapatikana mwanza na Dodoma; Dsm yapo ila kwa unayeanza siyo mazuri sana; kwahiyo kama una mtaji ni vyema uanze kutafuta masoko kisha uanze kununua na kuuza.
 
Ukikamilisha aliyokushauri Shakel empire unatakiwa kujisajili eneo utakalokuwa unauzia mbao mfano kama utauzia Dodoma nenda ofisi ya Tanzania Forest Service Agency ((TFS) Dodoma) watakusajili kwa Tsh 256,000/= pamoja na form ya maombi Tsh 5000/= (Renewable 01 July yearly). Baada ya hapo hakikisha mbao unazonunua zimevunwa halali i.e. unaweza kupata mbao kwa njia tatu:

1. Kuvuna katika msitu wa serikali (Hapa lazima uwe umeruhusiwa kuvuna (utakuwa na lesseni ya uvunaji))
2. Kununua kwa wananchi wenye mashamba ya miti (Uwe na vibali/barua ya mtendaji)
3. Kununua kwa wafanyabiashara maeneo tofauti (Uwe na nyaraka za kununulia i.e delivery note, Invoice na uthibitisho wa source ya mbao mfano leseni ya uvunaji)

Ukiwa navyo hivi vitu nenda ofisi ya TFS iliyo jirani na uliponunulia mzigo wataukagua halafu utapewa kibali cha kusafirishia (TP) mbao zako ambayo inalipiwa kwa gari ya tani 7 ni Tsh 6500/= na zaidi ya tani 7 ni Tsh 13,000/=. Pia utatakiwa kulipia ushuru wa halmashauri ambao hutofautiana halmashauri moja hadi nyingine either kwa pieces or ujazo (CBM).
Mkuu DIBEGU nakutakia kila la kheri katika hii FURSA na wana JF wengine wanaweza kujazia ili ufanye kazi kwa ufanisi.
 
Last edited by a moderator:

Vp mkuu kuhusu kusafirisha nje? Kuna company inahitaji mbao toka Tanzania, iko India. Hebu nipo taratibu ikiwezekana tumpe kazi huyu mtoa mada.
 
Vp mkuu kuhusu kusafirisha nje? kuna company inahitaji mbao toka Tanzania, iko India. Hebu nipo taratibu ikiwezekana tumpe kazi huyu mtoa mada.
Mkuu dikembe, Sina ufahamu mkubwa katika exportation ila kwa kuanzia inatakiwa utume maombi (TFS Head quarter) ya kibali cha kusafirisha mazao ya misitu nje ya nchi, maombi haya yataambatana na vitu hivi:

  1. Maelezo ya wapi utapata mazao (Mbao)
  2. Copy ya Usajili wa mbao wa eneo (mpakani) unalosafirishia mf. Dar, Holoholo, Holili, Namanga n.k
Ukikubaliwa;

  1. Utapewa kibali cha kukuruhusu kusafirisha (Aproval for Export of Forest Product)
  2. Utakata usajili wa kusafirisha nje mbao (Export of Forest Product) ambao ni Tsh 512,000/= (renewable yarly)
  3. Kabla hujasafirisha mbao lazima zikaguliwe (Gradind and Inspection) ambao unalipiwa kulingana na consignment lakini ya chini kabisa ni Tsh 128,000/= (Hili hufanyika huko mpakani).
Nakaribisha wataalam zaidi.
 
Nimekuelewa mkuu, nashukuru.
 
Habari za mchana wana Jf,

Naomba kujulishwa, kati ya kuweka vibarua kupasua mbao then niuze mbao na kuuza msitu wenye miti ya mbao ipi ina faida? Miti ni mipaina (pine).
 
LIGEDENGE 1

ya kuweka vibaruwa ili wapasue ww utaenda kuziuza mbao ktk mikoa yenye mahitaji makubwa ya mbao, hiyo itakupa faida kubwa zaidi!
 
Last edited by a moderator:
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako,vp kwa huo mzigo mkubwa wa semi trailer kwa utalaamu wako ukisafirisha kuuza dodoma utakuwa na faida nzuri? Na vp kuhusu garama za usafiri hadi Dodoma?
 
Ukikamilisha aliyokushauri Shakel empire unatakiwa kujisajili eneo utakalokuwa unauzia mbao mfano kama utauzia Dodoma nenda ofisi ya Tanzania Forest Service Agency ((TFS) Dodoma) watakusajili kwa Tsh 256,000/= pamoja na form ya maombi Tsh 5000/= (Renewable 01 July yearly). Baada ya hapo hakikisha mbao unazonunua zimevunwa halali i.e. unaweza kupata mbao kwa njia tatu:

1. Kuvuna katika msitu wa serikali (Hapa lazima uwe umeruhusiwa kuvuna (utakuwa na lesseni ya uvunaji))
2. Kununua kwa wananchi wenye mashamba ya miti (Uwe na vibali/barua ya mtendaji)
3. Kununua kwa wafanyabiashara maeneo tofauti (Uwe na nyaraka za kununulia i.e delivery note, Invoice na uthibitisho wa source ya mbao mfano leseni ya uvunaji)

Ukiwa navyo hivi vitu nenda ofisi ya TFS iliyo jirani na uliponunulia mzigo wataukagua halafu utapewa kibali cha kusafirishia (TP) mbao zako ambayo inalipiwa kwa gari ya tani 7 ni Tsh 6500/= na zaidi ya tani 7 ni Tsh 13,000/=. Pia utatakiwa kulipia ushuru wa halmashauri ambao hutofautiana halmashauri moja hadi nyingine either kwa pieces or ujazo (CBM).
Mkuu DIBEGU nakutakia kila la kheri katika hii FURSA na wana JF wengine wanaweza kujazia ili ufanye kazi kwa ufanisi.

Nashukurun kwa maelezo yako kwani yamenipa mwanga sana,kwa utalamu wako kati ya hizo njia tatu za ununuaji ni ipi ambayo ni rahisi na inaleta faida nzuri zaidi?
 
Katika mkoa wa iringa mbao zinapatika mafinga;makambako na njombe ambayo sasa ni mkoa;kila size ya mbao ipo ni wewe tu;mzigo wa kujaza gari kubwa yaan semi trailer unagarimu takriban milion 16;na mzigo wa kawaida ni milion kumi;kwasasa masoko mazuri ya mbao yanapatikana mwanza na dodoma;dsm yapo ila kwa unayeanza siyo mazuri sana;kwahiyo kama una mtaji ni vyema uanze kutafuta masoko kisha uanze kununua na kuuza:
Nashukuru sana mkuu kwa maelezo yako, vp kwa huo mzigo mkubwa wa semi trailer kwa utalaamu wako ukisafirisha kuuza Dodoma utakuwa na faida nzuri? Na vp kuhusu garama za usafiri hadi Dodoma?
 
Nashukurun kwa maelezo yako kwani yamenipa mwanga sana,kwa utalamu wako kati ya hizo njia tatu za ununuaji ni ipi ambayo ni rahisi na inaleta faida nzuri zaidi?

Mkuu njia ya kwanza, kununua serikalini, inalipa kuliko njia zingine ndo maana unasikia kuna malumbano sana kuhusu uvunaji ktk mashamba maana unaweza kukuta waombaji ni 2000 ila wanapata 300 na katika hao 300 ndo kuna kina Straight corner, DIBEGU, Mawaziri, Wabunge, Madc, Wakurugenzi, na akina yakhe wote. Nakumbuka kigezo cha kwanza ni usajili wa Saw Mill vingine vinafuata, na kuna kuuza kwa mnada, taarifa sahihi unaweza kuzipa katika mashamba husika (Sao hill, Rondo, Mtibwa, Kawitire, Rongai, West Klm, Meru, Buhindi, etc).

Njia ya pili inafuata na mwisho njia ya tatu ambayo inafaa kwa mlaji.
 
Nashukuru sana straight corner.
 
Back
Top Bottom