Mdogo wangu anafanya hii biashara Ana TV mbili na PS 4 mbili kwakweli anapiga hela sana siku akiingiza hela mdogo Hadi analalamika ni 15,000/=.ameanza mwaka Jana November kuna kipindi alienda shule akaweka mtu na alikuwa anatumiwa hela zake vizuri tu.Dogo ni mcheza Mpira pia na anajua kucheza hizo PS haikua ngumu kwake kupata wateja maana marafiki zake na team mates ndo walianza kumsupport.
Pia fremu ipo barabarani na inaonekana sana mtu akipita hata kwenye daladala anapaona na anaweza kufika kirahisi.
Haruhusiwi kufungua asubuhi kwa ajili ya wanafunzi huwa anafungua kuanzia saa Saba mchana Hadi saa tano usiku,wikiendi anafungua kuanzia asubuhi.
Alifuata kibali Cha kuchezesha game kwa mwenyekiti wa mtaa akapata so hasumbuliwi sana.
Biashara inaenda vizuri anataka kuongeza screen na PS nyingine moja aweke na vinywaji na bites anawauzia wanaokuja kucheza Ni biashara nzuri sana kwake kwasababu anaipenda na anajua so hakosi hela ya vocha na vitu vingine.