Hii biashara nzuri sana changamoto zake sio kubwa sana ukilinganisha na baadhi ya biashara nyingine mambo yakibuma unasubiri kodi iishe unakusanya vifaa vyako unaenda fungua pengine maisha yanasonga.
Changamoto ni kubwa kwenye kila biashara. Hii nayo haiko nyuma
1) Umeme ndo uti wa mgongo wa hii biashara. Itakulazimu kuwa na Generator ambapo, ili kuingiza faida na kuwa constant itabidi siku Generator linatumika uongeze bei kidogo.
Hii itafanya watu kutega siku zenye umeme ndo wanakuja.
2) kama ushawahi kumiliki ps3/Ps4 na sasa Ps5 unajua kabisa umuhimu wa kua na accesories original. Nazungumzia sana Pas/Controllers/ Joystick inategemea wewe unaziitaje.
Hivi vidubwana kuharibika ni rahisi sana, hii husababishwa na aina ya uchezaji wa mtu na pia yapo magemu ambayo hutumia force nyingi hasa kwenye kurotota Log. Hapa utajikuta kila baada ya muezi miwili unanunua Controller kama tatu.
3) Latest Games. Hamna MTEJA serious atakuja eneo lako leo, umuwekee FIFA 19 alafu kesho arudi. Wengi wanapenda tittle kubwa, tittle recent.
Sikuizi mambo yamekua marahisi kidogo kuna option kadhaa, unaweza cheap console yako, au ukaweka PSN account ukanunua Game alafu ukainstall kwenye Playstation zote (hii ina changamoto kidogo)
Hapa inakufaa uwe mpenzi wa magemu ili uweze kufuatilia kwa ukaribu Game ipi ni mali na ipi sio. Ukiwa umeingia huku kwa sababu tu umeskia kuna 40,000 daily utajikuta unaangukia pua. Wewe utakua mpaka leo una Fifa 18 na wakati watu wanangoja kucheza Fifa 23 miezi kadhaa ijayo.
4) Uwekezaji sahihi. Bila akili kila biashara ni bure. Jaribu kuchunguza kwanza wenzako walioko kwenye hii industry wamefanya kwa kiasi gani? Je mtaa unaofungua hapajawahi kufunguliwa game center? Kama ndio, kwa nini ikafungwa? Je mtaa unaokaa kuna vijana ambao wana passion na hii kitu? Je, kuna kipi cha kuongeza ili kuipa biashara yako heshima?
Hii ni changamoto kubwa sana. Je wateja wako watakaa kwenye benchi la mbao ambalo baada ya mda atachoka makalio? Au utamuwekea sehemu comfortable ya kukaa akitaka kucheza hata masaa kumi na mbili acheze? Hapa ukikosa akili ya ubunifu basi umeumaliza mwendo kijana. Umelala yoooo
5) INTERNET hapa sihitaji kuielezea kwa undani sana. Ila kama biashara yako iko nje ya maeneo ambayo unaweza kupata internet ya fiber ambayo ni unlimited na unapata kwa gharama nafuu mpaka 60,000 tu kwa mwezi andika pain kama unataka kuchezesha kisasa. Kudownload game moja la PS4 huchukua mpaka GB 30 inategemea na tittle. Kucheza online kwa lisaa huchukua wastani wa GB 1-4 inategema na load time. Hapo una console 4, hujakutana na mteja anaecheza kwenye “Party” utajua hujui.
LENGO LA HII COMMENT SIO KUMTISHA MTU. NI KUWASHA MWANGA GIZANI. ILI UNAPOINGIA KWENYE HII BIASHARA UJUE KABISA PALE PANA SHIMO ACHA NIRUKIE HUKU.
OTHERWISE NI BIASHARA SAFI SANA HASA KAMA UNA PASSION NAYO.
Kwa mawasiliano zaidi kuhusu hii na biashara za aina kama hii
Wasiliana nami PM
(Kwa ushauri tuu, siuzi wala sitoi huduma yeyote kwa malipo. Natoa ushauri tuu)