Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Mkuu naomba kujua Kuchipiwa ni nini
Ni kama unavyoona radio tu! Zamani ukinunua zile radio original zenyewe, zilikuwa zinachangua DVD! Kama DVD ni fake, haita-play! Na hizi PS ndivyo zilivyo!!

Sasa chipped console ni zile ambazo wanaziingiza chip (like modifying) ili hatimae ziweze ku-play hata hizi games unazoweza ku-download online or hata ku-duplicate
 
Changamoto ni kubwa kwenye kila biashara. Hii nayo haiko nyuma

1) Umeme ndo uti wa mgongo wa hii biashara. Itakulazimu kuwa na Generator ambapo, ili kuingiza faida na kuwa constant itabidi siku Generator linatumika uongeze bei kidogo.
Hii itafanya watu kutega siku zenye umeme ndo wanakuja.

2) kama ushawahi kumiliki ps3/Ps4 na sasa Ps5 unajua kabisa umuhimu wa kua na accesories original. Nazungumzia sana Pas/Controllers/ Joystick inategemea wewe unaziitaje.
Hivi vidubwana kuharibika ni rahisi sana, hii husababishwa na aina ya uchezaji wa mtu na pia yapo magemu ambayo hutumia force nyingi hasa kwenye kurotota Log. Hapa utajikuta kila baada ya muezi miwili unanunua Controller kama tatu.

3) Latest Games. Hamna MTEJA serious atakuja eneo lako leo, umuwekee FIFA 19 alafu kesho arudi. Wengi wanapenda tittle kubwa, tittle recent.
Sikuizi mambo yamekua marahisi kidogo kuna option kadhaa, unaweza cheap console yako, au ukaweka PSN account ukanunua Game alafu ukainstall kwenye Playstation zote (hii ina changamoto kidogo)
Hapa inakufaa uwe mpenzi wa magemu ili uweze kufuatilia kwa ukaribu Game ipi ni mali na ipi sio. Ukiwa umeingia huku kwa sababu tu umeskia kuna 40,000 daily utajikuta unaangukia pua. Wewe utakua mpaka leo una Fifa 18 na wakati watu wanangoja kucheza Fifa 23 miezi kadhaa ijayo.

4) Uwekezaji sahihi. Bila akili kila biashara ni bure. Jaribu kuchunguza kwanza wenzako walioko kwenye hii industry wamefanya kwa kiasi gani? Je mtaa unaofungua hapajawahi kufunguliwa game center? Kama ndio, kwa nini ikafungwa? Je mtaa unaokaa kuna vijana ambao wana passion na hii kitu? Je, kuna kipi cha kuongeza ili kuipa biashara yako heshima?
Hii ni changamoto kubwa sana. Je wateja wako watakaa kwenye benchi la mbao ambalo baada ya mda atachoka makalio? Au utamuwekea sehemu comfortable ya kukaa akitaka kucheza hata masaa kumi na mbili acheze? Hapa ukikosa akili ya ubunifu basi umeumaliza mwendo kijana. Umelala yoooo

5) INTERNET hapa sihitaji kuielezea kwa undani sana. Ila kama biashara yako iko nje ya maeneo ambayo unaweza kupata internet ya fiber ambayo ni unlimited na unapata kwa gharama nafuu mpaka 60,000 tu kwa mwezi andika pain kama unataka kuchezesha kisasa. Kudownload game moja la PS4 huchukua mpaka GB 30 inategemea na tittle. Kucheza online kwa lisaa huchukua wastani wa GB 1-4 inategema na load time. Hapo una console 4, hujakutana na mteja anaecheza kwenye “Party” utajua hujui.

LENGO LA HII COMMENT SIO KUMTISHA MTU. NI KUWASHA MWANGA GIZANI. ILI UNAPOINGIA KWENYE HII BIASHARA UJUE KABISA PALE PANA SHIMO ACHA NIRUKIE HUKU.

OTHERWISE NI BIASHARA SAFI SANA HASA KAMA UNA PASSION NAYO.

Kwa mawasiliano zaidi kuhusu hii na biashara za aina kama hii
Wasiliana nami PM

(Kwa ushauri tuu, siuzi wala sitoi huduma yeyote kwa malipo. Natoa ushauri tuu)
Asante sana mkuu nitakucheki oneday. Natamani kufanya hii biashara
 
Nisha nunua kila kitu hapa nawawazia wasumbufuu tu, wakuja kunipigia kelele, kuhusu watoto wao,!!
 
Biashara moja ya kiboss sana.
Tafuta ps3 tatu na ps4 moja na ps2 moja. Then tv 4 za inch 32 kwaajili ya ps3 nanps4 na tv moja inch 22 flat kwaajili ya ps2.
Chukua kibali ambacho ni 20k kwa miaka miwili. Anza kula faida ya 20k j3 hadi j5 then 30k to 40k alhamisi na ijumaa. 50k jmos na jpili.
Mkuu hiki kibali nakipatia sehemu gani!?
 
Kwa ansehitaji PS4 nauza hii bei laki 6 location kimara mwisho
IMG_20220216_124905_527.jpg
 
Hivi kuna ukweli wowote kwamba ps4 fat inaweza kuhimili mishindo(ikiwemo kufanya kazi kwa muda mrefu) kuliko ps4 slim?
 
Eneo gani hilo ambalo watu watakuletea hela kucheza ps2 leo 2022? Embu tufanye research ndogo. Aheei uanze na ps4 mbili itakupa mileage kuliko kuweka ps2.
Hio ps2 yako itakua ni asset ambayo haina maslahi
Hio PS2 nazan anaweza weka game kama blur, au need for speed watoto wengi wanacheza, wakubwa sio sana
 
Wakuu nahitajo ps 4 pro. kama naweza elekezwa pa kuipata kwa bei nzuri ni vizuri
 
Siyo deal mbaya.

Changamoto ni pad kuharibika mara kwa mara.

Zinahitajika Fifa na Pes kila mwaka au miezi sita.

Umeme.

Wizi.
Habari mkuu
Nilikuwa natafuta Ps3 used, ila nimekutana na hii jamaa ananiambia inavipengele hivi
Ushauri wako tafadhali
Screenshot_20220329-071327~2.jpg
 
Habari mkuu
Nilikuwa natafuta Ps3 used, ila nimekutana na hii jamaa ananiambia inavipengele hivi
Ushauri wako tafadhali
View attachment 2167776
Kuna ishu fulani hivi ikiwa inatokea mtu unaweza hisi tatizo ni switch ila actually motherboard ndo inakua na shida.

Yaani ukiwa unacheza utashangaa ghafla inazima, inablink kidogo rangi nyekundu na njano kisha inabaki kijani. Ukizima ile switch ya nyuma ukiwasha inawaka na unaweza kucheza hata siku nzima isifanye hivyo.

Hapo ni mwanzoni. Tatizo likikomaa utakuta inajizima frequently na style ya kujizima ni hiyo taa kublink. Tatizo hili linazikumba sana PS 3 Fat na Fat sehemu ya switch ni ya ku-touch so it is unlikely switch kua mbovu.

Kama tatizo linafanania na nilichoandika hapa achana na hiyo PS kwakua kwanza utengenezaji wake utaliziba tatizo kwa labda miezi sita au zaidi kisha litaanza upya. Na ikifikia siku ikajizima na taa ikaganda kwenye rangi ya njano hiyo game ndiyo haiponi tena hata ufanyeje hiyo rangi inaitwa YLOD (Yellow Light Of Death)

So kujizima kunaweza kukutrick ukahisi labda ni switch ila actually ishu inakua siyo switch. Storage siyo tatizo as ukinunua hard drives (external) inakaa vizuri tu, utakua na gharama ya kuweka system na kuweka games.

Kwa Dar game za 3 ni 5000 ( Game moja) sijajua ulipo so yaweza kua chini zaidi au juu kidogo.

Ushauri wangu kama ni lazima ununue hiyo game, uliza kama ni fat au slim, akisema tu ni Fat temana nayo huna haja ya kujua huku mbele.
 
Back
Top Bottom