Nimefanya hiyo biashara mwaka jana.iko na faida na hasara zake aghalabu changamoto ni nyingi.
Kwa kuwa mimi nafanya kazi Zanzibar nilinunua kila kitu hapa.sasa kilichonikuta
Ili bidii nimpatie jamaa yang tv na magem anisafirishie mpaka morogoro mana kazi zilinibana sikupata chance ya kuvisafirisha.
Nilimuamin jamaa kwa kuwa yeye ndo kazi zake na ila alichonifanya nimuachie Yehova.
Mimi niliamua kuanza na tv tano na ps2 tano.
Kila tv nilinunua 70000tsh@1
Dek za ps nazo 70000tsh@1
Mikono ya ps 9000tsh@1
Flash gb 8 7000tsh@1
Memory za dek 3000tsh@1
Waya sauti 2000tsh@1
Switch cable 30000tsh
@1 zidisha mara 5.
Usafiri inategemea.
Sasa hapa kodi inategemea pamoja na mabench na meza.
Lazima upate maeneo yenye watoto wengi"uswahilini"
Umeme makubaliano yenu. Ukipata luku yako ni mali.
CHANGAMOTO
TV sehemu ya picha na saut isiwe ya kashata.tv itakua inabagua magemu rangi
Magemu ya baiskel na ngumi yanauwa sana mikono(pad).so inabidi uwe mwangalifu.na bei isiwe sawa na magem ya mpira
Kama ukifungua asubuh kuna uwezekano wa kutupiwa lawama na wazaz. Watoto hawaendi shule wanashinda kwenye magemu.
Nimefunga biashara baada ya kuandamwa na wenyeviti wa mitaa nifungue jion.ili vijana wao waende shule.
Magemu ni muda na ukifungua jion hupati faida. Nikashindwa
FAIDA
NIKIFUNGUA MAPEMA NA WATOTO WAKIWA WENGI NAPATA HADI TSH 25000