Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Biashara ya Michezo ya Video (Video Games): Jifunze Uendeshaji, Changamoto na Faida Zake

Habari zenu wana JF,

Naomba kufahamishwa hapa kwa mwenye ufahamu kuhusu hii biashara ya Play Station Game kuanzia mtaji, vifaa, na maeneo rafiki kwa biashara hii.
Tafta mtaa wenye population kubwa na ambao hakujawahi kuwekwa huduma ya playstation
Hapo anza na playstation 2 bei yake ndogo lakni Ps 3 hyo bei yake used ambayo haijatumika sana ni laki 8 so tafta eneo zuri tuu
upo pand zipi?
 
Mkuu. Hope sijachelewa kukujibu hapa. Mimi binafsi nafanya hii biashara na ki ukweli inalipa kama uko makini na unajua kuhusiana na games za watoto. Binafsi nilianza na mtaji wa TZS 2 milion. Mimi ninachezesha Play Station 3 na Xbox One. NIna Play Station 3 tatu na X box 1. MAuzo kwa siku ni kati ya TZS 25,000 mpaka 35,000 (weekend ndio kunakuwa na hela zaidi). Play Stations zangu nimezi 'chip' kule kariakoo..zina games ndani, games latest na nilipata hii service kariakoo. Biashara hii inategemea na maeneo ila all in all, inalipa sana ukichukulia watoto wanapenda video games na wengi wao hawawezi ku afford kununua. Changamoto pia zipo ila ndio part ya biashara. Ukitaka maelezo zaidi nitakupatia..all the best mkuu, karibu kwenye ujasiliamali
Kwani PlayStation ndo nn maana hata sielewi mi nikajua kama zile za madesktop wanacheza Zuma na FIFA sssa mnaniambia kuna PlayStation 1 ,2 cjui 3 hata sielewi
 
Hata mm cna ufahamu juu ya hivi vitu mkuu,pole ila naona kuna wajuzi humu watakujuza bila shaka.
Games za virtual unaweza kucheza
Unaweza kucheza katika mifumo ifuatayo
>Computer
>Smartphone
>Gameboy
>PlayStation
>Online n.k
Kwa hiyo PlayStation inakuweza kucheza games kupitia runinga yako ni system
N.B ni uwelewa wangu
 
Biashara hiyo haina tofauti na ya Bangi Defender Kila siku nje kwani wazazi wa watoto hushindwa kuvumilia
Hahahaha kwel inahitaj uwe na roho mbaya coz kunamadogo weng utawasababishia misala kwa familia zao
 
Kwani PlayStation ndo nn maana hata sielewi mi nikajua kama zile za madesktop wanacheza Zuma na FIFA sssa mnaniambia kuna PlayStation 1 ,2 cjui 3 hata sielewi
Ni video games, tofauit kidogo na computer. Usitake niambia hujawahi come across hizi games at all. Itabidi utafute mkuu, very user friendly kwa gamers
 
Hii biashara ni nzuri. Playstation2 bado inalipa maana kwa hali ya uchumi wateja wanamudu. Fungua tu sehemu za mtaani maana wateja wakuu vijana wadogo chini ya miaka 20. Kama uko dsm zingatia kuweka mazingira mazuri yenye hewa ya kutosha bila kusahau kuweka feni. Viti vizuri na screen nzuri flat angalau 24". Mweke kijana mtulivu na ikiwezekana baada ya mwezi au zaidi baada ya kuona mwelekeo wa biashara mpangie kiasi cha kukuletea kila siku kama daladala vile. Kinachobaki ndo mshahara wake. Changamoto ni kama hivyo serikali kukuandama endapo utakuwa unafungua mapema kabla ya watoto kutoka shule au kufunga usiku mkali sana. Binafsi naona hiyo changamoto haiathiri chochote maana hata usipozuiwa na serikali ujue wateja hupatikana wengi kuanzia mchana kwa hiyo hakuba haja ya kushindana na serikali kufungua asubuhi. Changamoto mbaya ni pad kuharibika mara kwa mara. Hapo ni kujitahidi tu kuwa makini ktk utunzaji na kununua pad original ambazo angalau huchukua muda mrefu hadi kuharibika. Kama huchezeshi mwenyewe tegemea kupata visingizio ya kwamba "leo bro hakukuwa na wateja kabisa". Kuepuka hilo nimeshasema endesha kwa mfumo wa biashara ya daladala. Kwa kuanzia waweza anza na PS2 tatu zikiwa na screen zake. Ni biashara nzuri ambayo huwezi kosa Tsh 20000 hadi 25000 kwa siku na ambayo haina mambo mengi ya kushughulikia. Wateja ni wa uhakika. Mimi nimefanya biashara hiyo kwa miaka zaidi ya miwili kabla ya kuamua kuiacha maana usimamizi wangu umesuasua baada ya kutingwa na biashara zingine. PS2 zikiwa complete na TV 24" ninazo ninaziuza kwa bei nafuu. Niko Dsm piga 0757528827 ukizihitaji.
 
ps3.png

Mchanganuo wa mtaji wa biashara ya gaming centre

PS3 tatu 1,200,000
CD tatu (FIFA 18) 300,000
tv tatu 500,000
stabilizer 100,000
meza na viti 200,000
CCTV camera 100,000
Leseni 100,000
Chumba miez minne 400,000
usafiri, mchoraji, feni, extension n.k 100,000
JUMLA YA MTAJI 3,000,000


UTOZAJI =
MTEJA ITABIDI ALIPIE 2,000 ACHEZE SAA ZIMA AU 500 KWA MECHI MOJA

Faida = mapato - matumizi

Ni muhimu kujua ya kwamba makadirio haya nimefanya kwa dhana ya kwamba matumizi yatakuwa makubwa sana na mapato yatakuwa ya kawaida sana

MAKADIRIO YA KAWIDA KWA MAPATO KILA MWEZI
Masaa 5 * tv 3 * 2,000 kwa saa * siku 30 = 900,000

TOA: MATUMIZI KILA MWEZI
Mshahara wa muhudumu 100,000
matumizi ya mhudumu(chakula,vocha,usafiri) 100,000
tra + ulinzi 100,000
umeme+kubadilisha pads mbovu 100,000
savings ya kodi ya pango 100,000
JUMLA YA MATUMIZI 500,000

FAIDA 400,000/= kwa mwezi
4,800,000/= kwa mwaka


Hela yako itarudi ndani ya miezi 8

N.B: HIZI GAMES NI ADDICTIVE SANA KAMA MADAWA YA KULEVYA, WATOTO WENGI HUDIRIKI KUTOROKA MASHULENI, KUIBA PESA NYUMBANI KWAO AU KUUZA VITU VYA NYUMBANI ILI WAJE KUCHEZA GAME, PANGISHA FREMU MAENEO YA BIASHARA, USIPANGISHA FREMU ZA BEI RAHISI MAENEO YA MAJUMBANI AMBAKO UTAKUWA ADUI WA FAMILIA ZINAZOKUZUNGUKA
 
Mchanganuo wa mtaji wa biashara ya gaming centre iwapo ofisi itafunguliwa kila siku asubuhi mpaka jioni.

Ni muhimu kujua ya kwamba makadirio haya nimefanya kwa dhana ya kwamba matumizi yatakuwa makubwa sana na mapato yatakuwa ya kawaida sana.

PS3 tatu 400,000 x 3 = 1,200,000
CD tatu (FIFA 18) 100000 x 3 = 300,000
TV tatu 500,000 x 3 = 1,500,000
Stabilizer 100,000
Meza na viti 200,000
Leseni 100,000
Chumba miez minne 100,000 x 3 = 400,000
gharama nyingine mfano, extension, tangazo la biashara n.k 100,000
JUMLA YA MTAJI 3,900,000

Faida = mapato - matumizi

MAPATO KILA MWEZI

Masaa 6 * tv 3 * 2,000 kwa saa * siku 30 = 1,080,000

TOA: MATUMIZI KILA MWEZI

Mshahara wa muhudumu 100,000
matumizi ya mhudumu(chakula,vocha,usafiri) 100,000
tra + ulinzi 100,000
umeme+kubadilisha pads mbovu 100,000
savings ya kodi ya pango 100,000
Matumizi megine 80,000
JUMLA YA MATUMIZI 580,000

Tutafute Faida sasa
Mapato ya Mwezi 1,080,000
Matumizi ya mwezi 580,000
Faida Kwa Mwezi 500,000

Hela yako uliyoweka mtaji itarudi ndani ya miezi 8 tu na utaanza kupata faida.
 
Thanks broo nilikuwa na hio project but nina swali vip niki employ desktop na nisitumie ps

Sent using Jamii Forums mobile app
Dah, Pc ni old school siku hizi nimeona ps ndo zinabamba, Anywat mtaji wako utakuwa
desktop tatu 600,000
stabilizer + extensions 100,000
meza na viti 200,000
leseni 100,000
Chumba miez minne 400,000
JUMLA YA MTAJI 1,400,000

however hapo utachezesha kwa buku na sio buku 2
 
Dah, Pc ni old school siku hizi nimeona ps ndo zinabamba, Anywat mtaji wako utakuwa
desktop tatu 600,000
stabilizer + extensions 100,000
meza na viti 200,000
leseni 100,000
Chumba miez minne 400,000
JUMLA YA MTAJI 1,400,000

however hapo utachezesha kwa buku na sio buku 2
desktop 3 za games 600,000?
 
Ni bora kununua hizo PS3 ni rahisi sana kuliko kununua Desktop za Games mana Computer za gemes ni garama kubwa sana ndio maana Chief-Mkwawa amebakia na mshangao hiyo desktop moja ya games inaweza kufika bei ya hizo PS 3 zote tatu
 
desktop 3 za games 600,000?

mtaani naona bado games ni zile zile za mortal kombat 4, virtual cop, need for speed 2 na demorash, kwa haraka haraka i think pc zinzorun hizo games ni way too cheap, Ila kama ni kuchezesha fifa 18 hapo budget ya cpu nzuri na gpu za maana haikwepeki
 
Back
Top Bottom