Ninachoweza kukuhakikishia ni kwamba ukijipanga vizuri, biashara ya PS haina hasara. Hakikisha unapata eneo zuri lenye watu wengi hasa vijana (uswazi, chuo, etc).
Hakikisha unaanzia chini lakini unaimprove biashara yako routinely..yaani kama ulianza na PS2 & PS3 jitahidi baada muda fulani una'upgrade eneo, games na vifaa. Wateja wanapenda kuona improvement, hata ikiwa ni kwa kiwango kidogo cha msingi ni kufanya maboresho.
Kingine ni kuhakikisha unaweza kanuni na taratibu ambazo unaamini kwamba zitasaidia kuiwezesha biashara yako kurun smoothly. Katika hilo hakikisha unaweka utaratibu wa kutoruhusu wanafunzi kuingia katika Playstation wakiwa wamevaa uniform hasa muda masomo (hii ni lazima uiweke hata kama utakuwa hufanyi hivyo mara zote, itakusaidia sana). Kanuni zibandikwe ukutani ili kila mhusika aweze kusoma na kuelewa.
Kwenye kukusanya fedha za wateja, hakikisha unakuwa na daftari ambalo utakuwa unarekodi Jina, Muda, na Kiasi kilicholipwa na mhusika. Kumbuka msemo unaosema 'Mali Bila Daftari, Hupotea Bila Habari'!!
La mwisho na muhimu zaidi, pindi unaanzisha biashara yako utapata challenge sana kutoka kwa wazazi na watendaji/wenyeviti wa mitaa/Kata, Be Strong..don't quit! Lakini, hakikisha baada ya kipindi fulani unairasimisha biashara yako kwa kuichukulia leseni na kuanza kulipa kodi TRA. Ninakuhakikishia hakuna 'mshenzi' yeyote atakayekuja kuigusa biashara yako, na ofcourse itafika mbali na kuwa kubwa zaidi huko mbeleni.
Ni ushauri tu, unaweza kuchukua unayoona yanafaa na kupuuzia ya kupuuzwa. Otherwise nikupongeze kwa enthusiasm yako na Mungu akubariki sana.
Tukutane Kazini!
Sent using
Jamii Forums mobile app