Huo sio umafia ni upuuzi.
Siku nilipojua kwamba mawe yanawekwa ktk mchele ili kuzidisha kilo,na mchele unapakwa mafuta ili ung'ae kuonekana ni mpya,nilijiskia aibu sana kuwa mbongo.
Kuna vitu vya kijinga vinatughalimu sana hasa mbele huko ktk masoko ya watu makini,nimekumbuka story ya wanunuzi wa pamba kukuta mawe ktk marobota[emoji2961][emoji2961][emoji2961]
Mchele haupakwi mafuta ili ung'ae. Mchele unapakwa mafuta ili kuzuia usipate fungus kama utakaa muda mrefu store na ukapata unyevunyevu.
Usipopaka mafuta, kuna hali hutokea ukikaa store muda mrefu unatengeneza kama vumbi hivi ambalo litatengeneza wadudu kama funza ambao watakuja kuzaa wadudu fulani hivi wadogo size kama ya sisimizi wanaharufu mbaya kama jasho la beberu la mbuzi.
Wale wadudu wakikaa humo kwenye mchele wanautemea ile harufu ya mbuzi mchele unakuwa unanuka kama ulilaliwa na beberu la mbuzi, ukipika ile harufu ndio utaipata kwenye ladha muda wote.
So usiozungumze jambo bila kufahamu ukweli wake kutoka eneo husika kwa wahusika.
Kuhusu mawe, kwann ununue mchele ambao umeshapakiwa kwenye mifuko?
Unakoboa mpunga kiroba kimoja unautest kwa kuutafuna utaona ladha yake.
Mbegu nzuri ni ile ya Zambia ambayo imelimwa sana Kyela na Kamsamba, hizi mbegu za kisasa kama "Saro 5" ni takataka na hazina ladha kabisa.
Jambo lingine mashine za kisasa huwa zinatenga Pumba,Mawe,Chenga na Mchele visiwe pamoja. So ukiona mchele wako una mawe jua kuna mtu kaumimina kwa mkono ila sio kutoka gunia la mpunga maana mashine inayatoa mawe yenyewe na kuyatupa kando.
So nadhani haya maelezo yatakupa mwanga kidogo.