Biashara ya mahindi ni nzuri sana kama ukiuzia nje ya nchi,mfano kenya au sudan kusini, ikiwa uko mikoa ya arusha au manyara ni bora zaidi, ila sasa! Ni hadi uunge chain na wafanyabiashara wazoefu,wakubali kukupa ushirikiano na kukupa hints kadha wa kadha,otherwise hawa ndiyo ma mafia wenyewe,nipo kwenye circle ya biashara hiyo,ila kwa angle tofauti,kuna jamaa alijiingiza kibabe kwenye game bila kusajiliwa kwenye chama cha wafanyabiashara ya nafaka huko arusha, kilichomkuta alijuta, mzigo wa tani 30 ulizuiliwa mpakani namanga,akaambiwa yana aflatoxin,marufuku kuingia kenya, alipambana kuhonga na nini lakini hakufanikiwa kuuingiza,, ipo hivi=mfanyabiashara wa mazao anayeuzia kenya anapaswa kuwa na namba za askari wa barrier zote kutokea arusha mpaka sokoni kenya,na pale border vilevile, kwa hiyo mzigo ukifika kabla haujafika barrier askari wanajua mzigo wa fulani unakuja,border vilevile,na wanakuwa kwenye payrol yako,unakuwa unawatoa kwa chochote kitu, sasa kama hujulikani wale wazoefu wakijua unapeleka mzigo, simu zinapigwa kote, zuieni huo mzigo! Baba hupiti!! Ukivuka barriers zote safari yako inaishia namanga, utatoboka hela hadi mzigo unakupiga hasara takatifu, pale border mwishoni watakuja wafanyabiashara wazoefu, wakukatishe tamaa kabisa, kisha wakuambie uwauzie wao kwa bei ya hasara, ukikubali(probably utakubali tu) wao wanayanunua, na kuyavusha kiulaini kabisa,unarudi home na hasara yako.