Biashara ya nafaka ina umafia mwingi. Kwa wanaotarajia kuanza kuuza nafaka chukueni tahadhari

Wewe unadhani watu tunaandika humu ni mazuzu? Wale jamaa wanakuruhusu uukague mchele kwa juu ni mali safi na kati kati ni mali safi ununue sasa uufikishe dukani ndio utajua hujui.

Hata karanga ukiingia kichwa kichwa unauziwa zenye changarawe na ni ma fundi wazuri wa kufanya umafia ktk namna ambayo hutaielewa.

Suliuhisho ni kulima mwenyewe ndio uuze.
 
Hali ya janjajanjs ikiendelea hivi, Tanzania itaipiku Nigeria kwenye tasnia ya utapeli
Watu humu wqnajifanya wajuaji wakati hawajawahi hata kuuza pipi.

Mtu anakuambia ukomae na hiyo hiyo wwkati umechoma milioni mbili kwa awamu mbili tofauti.

Kama unataka kuwajua vizuri wauza mchele walivyo wezi wewe nenda mashineni umeshikilia kiroba watakupigania kama wapiga debe, na hao ni madalali, picha kamili ni kwenye mchele wenyewe. Hiyo biashara ingekuwa nyepesi madalali wasingejazana mashineni kwa wingi kuliko idadi ya wateja
 
Yaani Wateja wakienda Dukani wanaulizia mchele wa Mbeya, wauzaji ili wauze wanasema "Mchele wa Mbeya".

Sasa sijaelewa mwenzangu unaongelea mchele gani wenye ubora mzee?
Mchele upo wa aina nyingi sana kulingana na mbegu, changamoto mchele mtamu ukiulima unakuwa mwepesi alafu unatoa magunia kidogo yaami ndivyo ulivyo. Ila kuna mwingine ni mzito alafu wali wake hauna radha
 
Haya mambo omba yasikukute ndio maana wengi wanaogopa kuingia au wameacha kabisa issue za biashara. Ni challenges kwa kwenda mbele, japo ukiipatia biashara utajiri ni kufikia tu
 
Sukari inachanganywa na mchele ili wapige faida.
 
Shambani kuna mpunga sio mchele
 
Unadhani kulima rahisi?
 
Kwa kifupi kila aina ya biashara inahitaji uzoefu na elimu ya hiyo biashara husika.
Matapeli wapo kwenye kila aina ya biashara,huwa kazi yao ni kuvizia watu ambao ni wageni kwenye hiyo biashara ili wawaingize mjini.
Cha msingi ni kutulia na kujifunza biashara husika unayotaka kuifanya bila kukurupuka.
 
Ushawahi kufanya biashara ya Mbao wewe? Omba Mungu sana yasikukute๐Ÿ˜€๐Ÿ˜ƒ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜

Vipi kuhusu Malimbichi? We dalali uliyenidhulumu Mahindi yangu ya Gobo niliyohangaika nayo miezi 4 huku Makete Mungu anakuona.
Hivi hakuna uwezekano wa kufanya biashara bila kuhusisha dalali? Hawa watu nawachukia kama nyoka.
 
Uko sahihi. Kuitwa mfanyabishara ni uzoefu siyo kuwa na fedha za kununulia mali. Infact kwenye biashara uzoefu ni kitu kigumu kupata kuliko mtaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ